Wednesday 16 October 2013

Re: [wanabidii] Sheria ya Mabadiliko ya Katiba: Kuna Mgongano wa Kimaslahi ama ni Maslahi ya Umma Yanalindwa?

Mh. Dr. Hamis suala la Katiba ni letu sote, unfortunately wote nyie wabunge tuliowaamini kutuwakilisha mnalipeleka kivyama. Ningefurahi mantiki tu ndio ingewaongoza na sio itikadi. Kwangu mm wote (majority na minority) mliongozwa na itikadi katika kujadili na kupitisha hii sheria. Namshukuru Mh. Rais kwa kuona kuwa Tanzania ni kubwa kuliko nyie mnaoona kila kitu kisiasa.
Kila nchi ina mambo ya kitaifa yanayovuka itikadi za vyama. Hapa kwenu bungeni hakuna kitu kama hicho?
Ww ni msomi na mtaalam pia but niliona mchango wako haukureflect upeo mkubwa ambao najua unao.
Naamini Mh. Rais atatumia busara zile zile alizotumia na kuweka maslahi mapana ya Taifa katika kuusaini au kutousaini muswada maana Katiba inampa mamlaka ya kufanya moja kati ya hayo.

On Oct 16, 2013 5:51 PM, "Dr. Hamisi A. Kigwangalla" <hkigwangalla@gmail.com> wrote:

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba: Kuna Mgongano wa Kimaslahi ama ni Maslahi ya Umma Yanalindwa?

Na Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.

Wiki iliyopita niliandika makala iliyokuwa inachambua ni nini iwe njia ya kupita kufikia kukamilisha mchakato wa kukamilisha 'sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013' kwa muafaka wa kitaifa. Kufuatia nia safi ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete, kupitia hotuba yake adhimu kwa Taifa ya mwezi uliopita, wengi tulibaki tukijiuliza ni nini kifuate?

Mhe. Rais anataka muafaka wa kitaifa na anataka kutuunganisha watanzania wote ili tufike salama kwenye kukamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya. Hili, narudia tena, kwa yeyote yule mwenye akili timamu na mwenye kulitakia mema Taifa letu atalikubali, na kwenye hili asirudi nyuma kamwe. Akijaribu kurudi nyuma kwa hakika nafsi yake itamsuta na kwa Mungu atapaswa kujibu. Mzigo wa Taifa hili uko mikononi mwake. Hautui mpaka dhamana tuliyompa imuondoke.

Sisi kazi yetu ni kumshauri na kuonesha tunachokitamani, na yeye atapima na kuamua.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Ibara ya 62 na 63, Bunge lina sehemu mbili, Rais wa Jamhuri na wabunge, na kwa maana hiyo sheria ama jambo lolote lile haliwezi kuwa limekamilishwa bila kupitia moja ya sehemu hizi. Sheria tunayoizungumzia hapa imepitia hatua ya kwanza ya kupitishwa na wabunge, inasubiri uamuzi wa sehemu ya pili sasa, Rais wa Jamhuri. Anaweza kuamua lolote kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri wa muungano, kusaini ama kutokusaini. 

Katika makala ile nilijaribu kuchambua kwa ufupi sana, nini kitatokea kama angechukua njia ipi. Binafsi, nilijitahidi sana kuepuka kuonesha msimamo wangu mkali kwenye jambo hili, kwa kuheshimu mamlaka ya Rais na kuepuka kuonekana najaribu 'kumteka nyara' fikra zake.

Ukweli utabaki kuwa ukweli tu kwamba, niliegemea zaidi kwenye njia ya muafaka wa kitaifa na ambayo itatuacha wabunge wote na watanzania 'washindi'. Staili hii ni ya kimarekani. Inaitwa 'win – win situation'. Sikuweka msimamo wa chama changu ila nilisema ukweli tupu.

Nimepata maoni na maswali mengi sana kutoka kwa wasomaji, nikaamua nijibu baadhi ya hoja hapa. Kwanza, nisisitize kuwa mchakato wa kupitishwa kwa sheria ile bungeni ulikamilika ipasavyo na hakukuwa na mapungufu yoyote yale kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni na tamaduni zilizopo. Wengi wanataka kuaminishwa ama wanajilazimisha kuamini kuwa sheria haiwezi kutungwa na kupitishwa na Bunge bila kupelekwa kwa 'wadau'. Si kweli, maana si lazima. Hili ni jambo la busara tu ndani ya kamati husika kuamua kukusanya 'maoni' na 'ushauri' wa watu ambao wanaaminika kuwa ni 'wadau' ama walengwa wa sheria inayotungwa. Napigia mstari tena, kuwa ni 'busara' tu na hivyo si hitaji la lazima la Katiba, Sheria ama Kanuni.

Vyombo vyenye kazi ya kutunga sheria ni Rais kwa upande mmoja na Wabunge kwa upande wa pili. Wabunge walikwishamaliza kazi yao, bado tunasubiria Rais naye afanye ya kwake.

Lakini nikiri pia kuwa kuna vipengele vya sheria ile iliyopitishwa na Bunge vinaweza kuwa na mapungufu; hili si kitu sana, kwa maana hakuna sheria iliyowahi kutungwa na ikategemewa kuwa kamili ("perfect") kama msahafu wa quran ama biblia. Na ndiyo maana ikawepo fursa ya kufanya marekebisho kwenye sheria. Na labda niseme tu hapa kwamba, huu ni moja ya msingi wa ushauri wangu kwa Mhe. Rais kwenye makala yangu iliyopita. Kwamba akikamilisha mchakato wa kutungwa na kupitishwa kwa sheria hii kwa kusaini na kisha kuelekeza serikali kupeleka bungeni mapendekezo ya marekebisho kwa njia ya 'hati ya dharura' atakuwa ameliokoa Taifa na kila kitu kitaenda kwa ratiba kama ilivyo.

Kilichotokea Bungeni ni kwamba, wapinzani walisusia mchakato wa kutunga sheria ile ilhali wakijua fika kuwa hakuna kilichoenda mrama zaidi ya kuwa na mapendekezo yao ambayo walishindwa kuyapenyeza kwa njia ya 'ushauri na ushawishi' (Consultation and consensus building) katika hatua za awali na walijua kuwa kwa kuwa wao ni wachache wasingefanikiwa kuyapitisha bungeni. Wakaamua kutengeneza hoja za maksudi za kususia mchakato ili hapo baadaye wapewe fursa ya kusikilizwa na Rais ili washinikize yapite ama sivyo 'wataliteka nyara' Taifa kwa vitisho vya kuhamasisha uasi wa wananchi dhidi ya serikali.

Kuna wasomaji waliniandikia wakisema kuwa ni heri ya wale wabunge waliotoka nje ya bunge kuliko ya wale waliobaki ndani ya bunge 'wakitukana!' Kutukana ndani ya bunge ni jambo linalokatazwa. Hivyo hakuna aliyebaki na kuanza kutukana.

Lakini, tabia ya kususia kikao cha bunge si ya kiuongozi na ni kosa la kikatiba. Kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwenye kuisimamia na kuishauri serikali, na kwenye kutunga sheria. Kuwepo ndani ya Bunge ni kutekeleza jukumu la kwanza la msingi la Mbunge yeyote yule la kikatiba la 'uwakilishi'. Kusema lolote ama kutosema ni mambo ya upili. Kuwa na hoja ya msingi ama 'pumba' ni mambo ya nafasi ya tatu kabisa kwa umuhimu, ukizungumzia demokrasia ya uwakilishi bungeni.

Kwa maoni yangu, mchakato wa mashauriano na maridhiano ungepaswa uwe unafanyika mwanzoni kabla hatujaingia bungeni kujadili sheria na hatimaye kuingia kwenye tofauti kubwa namna hii. Niwashauri wenzetu wa upinzani na hata wa CCM bungeni kuitumia vizuri nafasi ya Waziri Mkuu pale Bungeni, maana yeye ni msimamizi mkuu wa shughuli za serikali Bungeni. Mashauriano, maridhiano na mapatano yataleta utangamano na mshikamano wa kitaifa, tuyakumbatie. Hili Taifa ni letu sote, hatuna sababu ya kuhitilafiana kiasi hiki kama kweli kuna hoja za msingi.

Kwa namna mchakato ulivyoenda na kwa kuzingatia hapa tulipofikia, njia pekee iliyopo si ya kuonesha namna gani wabunge walio wengi waliupitisha muswada huu bungeni bila umakini. Siwaoni wabunge wa CCM wakifurahishwa na wakiridhia mtazamo ama uamuzi wenye msingi huu.

Namna pekee ya busara itakayotoa ushindi kwa kila kundi ni kutambua kazi ya wabunge walio wengi walioupitisha muswada ule na pia kutambua mapungufu yaliyopo – mfano lile la kuiua tume ya mabadiliko ya katiba kabla ya mchakato kufikia mwisho. Hili kiukweli lina mantiki ndani yake; tukiwa kwenye bunge la katiba hakutokuwa na serikali, sasa ni nani atakayejibu na kuweka sawa hoja za wabunge? Hili kwa kweli wabunge tuliopitisha muswada ule hatukuliona vizuri. Hivyo basi,  jambo hili na mengine ya namna hiyo yasipuuzwe, yapelekwe bungeni kama marekebisho.

Kama Rais akiamua kuchukua njia ya kutoisaini sheria hiyo na hivyo kuirudisha bungeni ikiwa na maoni yake itakuwa fedheha kubwa kwa wabunge wa CCM, chama tawala anachotokea,  na wale wachache wa upinzani walioshiriki kuupitisha muswada huu. Siwezi kuamini kama anaweza kuwafedhehesha wabunge wake kiasi hicho. Najua kuna wasomaji wataguna kwenye hili, lakini haiondoi ukweli kwamba hili halina sura nzuri kwenye siasa na uongozi wa Taifa letu. Hata kama tunamtaka Rais wetu asimame kitaifa namna gani, lakini si kwa gharama ya kuwafedhehesha wabunge wake. Ni busara kutafuta njia ya kuyaunganisha mapendekezo ya wapinzani kwenye sheria hii kimkakati bila kuleta 'stalemate'.

Rai yangu kwa watanzania wenzangu ni kuwa, kuweni makini sana na sisi wanasiasa, kuna nyakati baadhi yetu huyageuza maoni na malengo yao ya kisiasa kuwa ya umma. Mitazamo ya kisiasa ya kundi moja la kisiasa si lazima iwe sahihi zaidi ya kundi jingine. Tusishabikie bila kujua ukweli wa mambo maana tutaliangamiza Taifa kisha tuje kujuta wakati maji yalikwisha mwagika. Na sisi wanasiasa tuwajibike ipasavyo (tuwe 'responsible') kwa Taifa hili maana yakiharibika hapa wanaopoteza zaidi ni wananchi! Hii ni dhamana yetu, tuitendee haki.

Dkt. Hamisi Kigwangalla ni Mbunge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).  Anapatikana kwa simu na +255782636963 na Email: hkigwangalla@gmail.com


"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment