Wednesday 9 October 2013

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Rais Kikwete Asaini ama Asisaini...? Makala ya Ushauri Wangu kwa Mkuu wa Nchi.

Ndugu. kila inacholetwa u jadili tu. Atakayesema wewe mkenya naye ana haki ya kusema vile. wewe toa maoni yako yanafaa sana

From: Maurice Oduor <mauricejoduor@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; afya-club@googlegroups.com
Sent: Wednesday, October 9, 2013 9:09 AM
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Rais Kikwete Asaini ama Asisaini...? Makala ya Ushauri Wangu kwa Mkuu wa Nchi.

Mtume !!!!!   Suala haswa hapa ni nini? Mbona Kikwete asipige muhuri, katiba ijadilive halafu kisha makasoro yarekebishwe? Hapo pana tatizo gani nduguzanguni?

Tusianze jameni kujadili masuala makubwa kwa hoja zisizo za maana.

Let us take this, have it signed by the President then we amend it. Tusongeni mbele jameni step-by-step.

Mie nashauri tu wala staki kuingilia. Nikijatoa maoni zaidi maskini nindaambiwa mie Mkenya sina slahi kwenye katiba ya Tanzania.

Courage



2013/10/7 Yusuph Kalyango <kalyangomy@gmail.com>
Heko mh.HK.
Kwa maoni na ushauri wako huu,nakupongeza.
 Ongera sana kwa kuanza kudhihilisha sasa kuwa wewe ni MD,MPH,MBA.
  Namwomba Mwenyezi Mungu azidi kukufunua na kukuongoza uwe na mawazo
chanya ambayo kiukweli kwa nchi yetu ndiyo jawabu mujarabhu na si
"majoriti" inayokuwa imepatikana kwa ufisadi,hila na ghirba ambayo
inajivisha joho lisilo lake kwani kama si kila raia wa nchi hii basi
zaidi ya robo tatu wanaamini na kujua wao ndio "mainoriti" . Tena
Mainoriti ya kwelikweli hasa.

On 10/7/13, Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com> wrote:
> Rais Kikwete Asaini ama Asisaini Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
> Mabadiliko ya Katiba?
>
> *Imeandikwa na Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.*
>
> Kama Ningemshauri Rais Kikwete hata kidogo tu kwenye hili la Sheria ya
> Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, ningemshauri
> aisaini sheria hiyo; ushauri wangu unazingatia lengo moja kubwa –
> kutengeneza muafaka wa kitaifa, na kwa maana hiyo makundi yote ndani na nje
> ya Bunge ni muhimu ili afanikishe kutupatia lengo hilo. Pia, ili kupata
> muafaka na kundi moja ni busara kulinda ulichonacho mkononi kabla ya kile
> kilicho angani, kama wanavyosema wazungu kwenye semi zao kuwa 'one bird in
> hand is worth more than a thousand on a tree.' (inayotafsirika kama 'ndege
> mmoja mkononi ana thamani kubwa zaidi ya alfu moja mtini!').
>
> Tayari Rais Jakaya Kikwete, kama Mkuu wa Nchi, anakuwa na jukumu la
> kimaadili na la kiuongozi kuhakikisha anatufikisha salama kama watanzania
> kwenye mchakato huu. Hatumtegemei asiwasikilize wapinzania na wadau wengine
> wote, hapana. Kuwasikiliza andiyo uongozi. Ni lazima awasikilize wote na
> atafute usawa kwenye mizania ya haki ili kuwe na muafaka wa kitaifa kwenye
> zoezi hili nyeti. Na binafsi nichukue fursa hii kumpongeza kwa kuwa
> msikivu, mvumilivu na mwenye kujenga madaraja na watu wote, badala ya uzio
> wa ukuta.
>
> Kufanikisha mchakato wa kuandika katiba linapaswa kuwa jukumu la kwanza la
> kimaadili la watanzania wote tunaoishi leo. Kwa viongozi wote hii ni
> dhamana kubwa kwao. Kuwa makini na waangalifu, kuwa na maadili ya kiuongozi
> na wakweli wakati wote, kuwa wavumilivu na wenye subira kwa wenzetu ni
> tabia ambazo zitatufikisha salama, hivyo tuzikumbatie.
>
> Majuzi hapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
> Mrisho Kikwete, akilihutubia taifa, pamoja na mambo mengine alizungumzia
> sintofahamu iliyojitokeza kwenye mchakato wa majadiliano na hatimaye
> kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya
> Katiba ya mwaka 2013.
>
> Mkuu wa Nchi, pamoja na kufafanua mambo mengine alisema:
>
> *"Nimeambiwa kuwa Kanuni za Bunge hazina sharti hilo hivyo Kamati
> haistahili kulaumiwa. Kama hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe
> Bungeni ili Wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo
> watu wataendelea kulauminiana isivyostahili. Hivyo basi, kuligeuza jambo
> hili kuwa ni suala la kukataa Muswada au kususia vikao vya Bunge au kufanya
> maandamano sidhani kama ni sawa."*
>
> Mhe. Dkt. Kikwete, katika hotuba yake alishauri kuwa suala hili lirudishwe
> Bungeni ili wabunge walizungumze. Mimi nimejiuliza tu kuwa linarudi katika
> sura ipi? Na je kurudi inamaanisha nini? Kwamba, mchakato ulikosewa –
> japokuwa Mhe. Rais anaweka wazi kwenye hotuba yake kuwa haukukosewa. Sasa
> kwa nini tunarudi nyuma – jibu hapo ni moja tu kuwa tunatafuta muafaka wa
> kitaifa wa kutupeleka kupata katiba mpya. Hili ni lengo la kila mwenye
> akili timamu. Nalikubali na nampongeza Rais wetu kwa uamuzi huu mzuri. Je,
> kurudi inamaanisha tunaanza upya ama tunaanzia wapi?
>
> Hoja ya makala yangu ni kushauri namna gani suala hili linarudi Bungeni na
> linarudi kwa muafaka wa kitaifa ambao ni nia ya wazi ya Mhe. Rais, kwa
> mujibu wa hotuba yake. Kwa kuwa hoja ya muswada huu ilipitia hatua zote za
> lazima za kikanuni, na kwa kuwa kuna kundi la wabunge walishiriki
> kikamilifu hata kufikia muswada ule kupita, na kwa kuwa imebakia sehemu
> moja ya 'Bunge' tu kukamilisha kazi ya kutunga sheria, ambayo ni Rais,
> ushauri wangu ni kuwa Rais aisaini kwa faida ya kuondoa uwezekano wowote
> ule wa kutengeneza matabaka ya wabunge 'walio wengi' (majority)
> kutokufurahishwa na hatua hiyo, kwa kitu ambacho wanaamini kilikuwa sahihi
> na kiliiva ipasavyo.
>
> Pili, kwa kuwa kulikuwa na wabunge 'walio wachache' bungeni (minority) na
> kwa kuwa katika demokrasia yoyote ile yenye afya nzuri maoni na sauti za
> wachache ni lazima yasikilizwe kwa umakini zaidi hata ya wale walio wengi;
> na kwa kuwa kupitishwa kwa sheria ile haimaanishi kuwa ni lazima ilikuwa
> sahihi kwa asilimia 100; na kwa kuwa tayari Mhe. Rais amechukua jukumu lake
> la kiuongozi la kuliunganisha tena Bunge letu, ili liwe na sura ya umoja na
> mshikamano wa kitaifa, ni busara kurudi mezani na kusikilizana na kisha
> kuleta mapendekezo ya vipengele vinavyowakosesha usingizi na amani
> wapinzania kwa njia ya 'muswada wa mabadiliko ya sheria' (ambayo itakuwa
> imekwishasainiwa sasa na Rais).
>
> Kuna swali litahitaji majibu kama uamuzi wa kuchukuwa njia inayoendana na
> ushauri wangu itafuatwa. Kwamba, ni namna gani tutarudi kuchukuwa maoni ya
> wazanzibari, yanayolalamikiwa na wapinzania, ilhali sheria itakuwa
> imeishasainiwa na kutakuwa kumeletwa vifungu tu vinavyohitaji kufanyiwa
> marekebisho? Maoni yatakuwa kwenye vifungu hivyo tu ama kwenye 'Sheria ya
> Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013' yote?
>
> Na kama Mhe. Rais akiamua kufuata njia nyingine, na pekee iliyopo, nje ya
> hii ninayoipendekeza mimi, ni kuacha kusaini Sheria hii iliyokwisha
> kupitishwa. Kama akifuata njia hii kuna mambo mawili yanaweza kutokea;
> kununa kwa wabunge walio wengi na walioipitisha na kuharibika kwa ratiba
> nzima ya mchakato wa katiba, maana ifahamike wazi hapa kuwa bila kuwepo kwa
> sheria hii, Bunge la katiba halitoweza kuitishwa.
>
> Madhara ya kuvurugika kwa ratiba ya mchakato wa katiba ni pamoja na
> kuchelewa kukidhi malengo ya kuwa na katiba mapema kabla ya kufikia muda wa
> kuanza chaguzi za serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hali
> hii ya kukwamisha zoezi itaweza kutufikisha kutenda dhambi ya kurefusha
> ratiba, kama walivyofanya Kenya – ambapo waliongeza mwaka mzima mbele ya
> ratiba yao ya uchaguzi, jambo ambalo halina uhalali wa kikatiba wa kuwa na
> muhula wa miaka 'mitano' ya uongozi zaidi ya 'utashi binafsi na uchu wa
> kuendelea kuwepo madarakani miongoni mwa sisi wabunge tuliopo sasa, tuhuma
> ambayo tutapaswa kuikiri  kama ilivyo, 'guilty as charged.'
>
> Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB ni Mbunge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa
> Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
>
>
> --
> "Vision is the ability to see the invisible!"
> Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
> P.O.Box 22499,
> Dar es salaam.
> Tanzania.
> Phone No: +255 754 636963
>                 +255 782 636963
> website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
> Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
> Skype ID: hkigwangalla
> Blog: blog.hamisikigwangalla.com
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> KARIBU MABADILIKO MPYA: Jukwaa hii sasa linapatikana katika mwuonekano wa
> Kisasa: www.forums.mabadiliko.com tafadhari tembelea na jisajili huko
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forum" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

KARIBU MABADILIKO MPYA: Jukwaa hii sasa linapatikana katika mwuonekano wa Kisasa: www.forums.mabadiliko.com tafadhari tembelea na jisajili huko

For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment