Tuesday 8 October 2013

Re: [wanabidii] Rais Kikwete Asaini ama Asisaini...? Makala ya Ushauri Wangu kwa Mkuu wa Nchi.

Uko sahihi Mkinga, kwa wasi wasi ni kuhofia kuwaudhi wabunge na siyo wananchi, pia huko nyuma kulikuwa na wale waliopata kuelezea kinachoweza kutokea iwapo hapatakuwa na makubaliano kwenye kufikia mwafaka wa vipengere vya mswaada, kwamba along the way Rais angeliweza kuiamua kuvunja  Bunge kitu ambacho kunaweza ku trigger uchaguzi mpya, eti kwamba hatua hiyo ni gharama kwa Taifa.
Kitu ambacho sifahamu ni kipi cha gharama kuliko kingine, kuwa na Katiba isiyokidhi mahitaji ya nchi na wananchi au kulenga kupata Katiba inayofaa lakini mkaondokana na sura za hao wanaodhani wao ni nusu miungu wa Watanzania, kwa uhai wa Watanzania unategemea na utashi wao.

From: Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; "afya-club@googlegroups.com" <afya-club@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 8 October 2013, 12:29
Subject: Re: [wanabidii] Rais Kikwete Asaini ama Asisaini...? Makala ya Ushauri Wangu kwa Mkuu wa Nchi.

Kwa jinsi mambo yalivyo sasa, sijali sana kwa chochote kitakachofanyika, hata kama Rais atasaini.
 
Kwa namna mambo yalivyo mpaka sasa, ni wazi kuwa hata kama katiba itapatikana, haitachukua muda mrefu kulazimika kuundwa kwa katiba nyingine mpya maana hii itakayotengenezwa sasa inakosa vigezo muhimu vya kuwa katiba ya wananchi.
 
Hata ukisoma makala ya Kigwangala unaona kabisa kuwa hawa watu wanafikiri tofauti kabisa na tunavyofikiria wananchi. Wao mawazo yao ni kuwa katiba inatengenezwa na wabunge, ndiyo maana Kigwangala anasema,
 
'Hoja ya makala yangu ni kushauri namna gani suala hili linarudi Bungeni na linarudi kwa muafaka wa kitaifa ambao ni nia ya wazi ya Mhe. Rais, kwa mujibu wa hotuba yake. Kwa kuwa hoja ya muswada huu ilipitia hatua zote za lazima za kikanuni, na kwa kuwa kuna kundi la wabunge walishiriki kikamilifu hata kufikia muswada ule kupita, na kwa kuwa imebakia sehemu moja ya 'Bunge' tu kukamilisha kazi ya kutunga sheria, ambayo ni Rais, ushauri wangu ni kuwa Rais aisaini kwa faida ya kuondoa uwezekano wowote ule wa kutengeneza matabaka ya wabunge 'walio wengi' (majority) kutokufurahishwa na hatua hiyo, kwa kitu ambacho wanaamini kilikuwa sahihi na kiliiva ipasavyo.
 
Ukisoma kwa kutafakari unaona wazi upeo na uelewa mdogo wa wabunge wetu. Wao wanadhani ndiyo pekee yao wenye mamlaka ya kushiriki kikamilifu katika kuandaa katiba. Halafu pia wanaongelea
 
 ---- kwa faida ya kuondoa uwezekano wowote ule wa kutengeneza matabaka ya wabunge 'walio wengi' (majority) kutokufurahishwa na hatua hiyo, kwa kitu ambacho wanaamini kilikuwa sahihi na kiliiva ipasavyo.......;
 
Kigwangala anazungumzia kutofurahishwa kwa wabunge ambao idadi yao ni 'negligible' ukilinganisha na idadi ya watanzania. Kigwangala haongelei juu ya mamilioni ya Watanzania ambao hawajafurahishwa na sheria inayopunguza ushiriki wa wananchi, anaongelea juu ya wabunge wachache waliopitisha huo mswada ambao nauita ni 'crap', kwa sababu haulengi ushiriki mkubwa na huru wa wananchi katika kupata katiba mpya kadiri ya matakwa yao na kwa namna wanayoiona inafaa.
 
Wabunge hawa waliopo bungeni hawakuchaguliwa na wananchi kwenda kutengeneza katiba ya Tanzania bali walichaguliwa kwa mujibu wa katiba kutuwakilisha katika kutunga sheria za kawaida kwa mwongozo wa katiba tulioitumia katika kuwachagua. Hawawezi kujitwisha jukumu kubwa la kuandaa kanuni na sheria za kupata katiba mpya, jukumu hilo ni la wananchi. Wananchi wanatakiwa kuwachagua wabunge wa bunge la katiba, na bunge hilo ndilo liwe na uwezo wa kuandaa kanuni na sheria za kuongoza mchakato wa upatikanaji katiba mpya. Mimi nilidhani kuwa baada ya CCM kuwepo kwenye madaraka kwa muda mrefu basi kungekuwepo, japo wachache wenye hekima, ambao wangejua wazi kabisa kuwa bunge letu na serikali wamejipa mamlaka ambayo hawakupewa na wananchi. Serikali ilistahili kurudi kwa wananchi ili wananchi waweze kuwachagua wawakilishi wao kwaajili ya kuandaa katiba na siyo kuwatumia wabunge ambao hawakuchaguliwa kwa kazi hiyo. Nina imani serikali ingerudi kwa wananchi kutaka kuwapata wawakilishi wao katika kuandaa katiba, wananchi wangewapata wawakilishi safi na wenye uwezo, siyo hawa wabunge wa JMT ambao wengi wao ni mazao ya rushwa na fedheha nyingi.
 
Msingi Mkuu wa mbunge yeyote yule ni kuwakilisha waliomchagua. Sasa hawa wabunge wa CCM wanaosema kuwa Rais acteue wabunge wa bunge la katiba, watakuwa wanamwakilisha nani, Rais aliyewachagua au wananchi? Kama ni wananchi, ni wananchi gani? Hata kama wabunge hao watakuwa wamependekezwa na makundi bado hilo haliondoi ukweli kuwa wameteuliwa na Rais. Hilo kimantiki litakuwa ni bunge la Rais la Katiba, siyo bunge la wananchi la kutengeneza katiba. Hapa hatustahili kuangalia uadilifu au uungwana wa Rais aliyopo madarakani, tunatakiwa kuongozwa na misingi na matakwa ya bunge la uwakilishi, wabunge wake wanatakiwa kupatikana namna gani? Mbunge ameteuliwa na Rais, bado atakuwa na sifa na haki ya kutamka kuwa anawawakilisha wananchi wa kundi fulani?
 
Ushauri wangu kwangu kwa Rais, haijalishi ana nia njema kiasi gani, au atazingatia mapendekezo ya makundi kiasi gani, asikubali kuwateua wabunge wa bunge la katiba. Akifanya hivyo atakuwa amekiuka kanuni ya msingi ya uwakilishi ambayo mwakilishi ni lazima achaguliwe moja kwa moja na anaowawakilisha.
 
Kuna watu wanaweza kusema kuwa, 'mbona wabunge wa bunge la Jamhuri ya Mwungano wanawakilisha wananchi, na hivyo wana haki ya kupitisha sheria za kuongoza mchakato wa katiba', jambo la msingi ni kuwa hawa hawakuchaguliwa kwa kazi hiyo. Nikikuchagua ukaniwakilishe kwenye jambo moja, haimaanishi uniwakilishe kwa kila kitu. WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MWUNGANO TANZANIA, hakuna hata mmoja aliyechaguliwa na wananchi kwaajili ya kwenda kuandaa katiba ya nchi. Na ndiyo maana ni halali kabisa katika kazi ya kuandaa katiba, hawa wabunge kutokuwa na 'role' yoyote ya pekee.
 
Ushauri kwa Rais Kikwete, kuunga mkono wabunge wengi wasio sahihi hakuwezi kukuondolea fedheha ya kushindwa kusimamia uundwaji wa katiba ya wananchi kwa namna wanayoitaka. Wabunge wa CCM ni sehemu ndogo sana ya Watanzania. Acha kusikiliza kikundi kidogo cha chama chako, wasikilize wananchi. Kama mchakato haukwenda kwa njia iliyo sahihi usione shida kuanza upya kama kuna sababu ya kufanya hivyo. Utajisikiaje kama baada ya kupoteza hela nyingi ya Watanzania, baada ya miaka 10, Watanzania wakaanza tena kuandaa katiba mpya kwa vile tu uliyoisimamia imeonekana haikidhi matakwa ya wananchi kwa sababu tu ulipenda kukiridhisha kikundi kidogo cha wananchi badala ya Watanzania walio wengi?
 
Bart

From: Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; afya-club@googlegroups.com
Sent: Monday, October 7, 2013 9:11 PM
Subject: [wanabidii] Rais Kikwete Asaini ama Asisaini...? Makala ya Ushauri Wangu kwa Mkuu wa Nchi.

Rais Kikwete Asaini ama Asisaini Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Imeandikwa na Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.
Kama Ningemshauri Rais Kikwete hata kidogo tu kwenye hili la Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, ningemshauri aisaini sheria hiyo; ushauri wangu unazingatia lengo moja kubwa – kutengeneza muafaka wa kitaifa, na kwa maana hiyo makundi yote ndani na nje ya Bunge ni muhimu ili afanikishe kutupatia lengo hilo. Pia, ili kupata muafaka na kundi moja ni busara kulinda ulichonacho mkononi kabla ya kile kilicho angani, kama wanavyosema wazungu kwenye semi zao kuwa 'one bird in hand is worth more than a thousand on a tree.' (inayotafsirika kama 'ndege mmoja mkononi ana thamani kubwa zaidi ya alfu moja mtini!').
Tayari Rais Jakaya Kikwete, kama Mkuu wa Nchi, anakuwa na jukumu la kimaadili na la kiuongozi kuhakikisha anatufikisha salama kama watanzania kwenye mchakato huu. Hatumtegemei asiwasikilize wapinzania na wadau wengine wote, hapana. Kuwasikiliza andiyo uongozi. Ni lazima awasikilize wote na atafute usawa kwenye mizania ya haki ili kuwe na muafaka wa kitaifa kwenye zoezi hili nyeti. Na binafsi nichukue fursa hii kumpongeza kwa kuwa msikivu, mvumilivu na mwenye kujenga madaraja na watu wote, badala ya uzio wa ukuta.
Kufanikisha mchakato wa kuandika katiba linapaswa kuwa jukumu la kwanza la kimaadili la watanzania wote tunaoishi leo. Kwa viongozi wote hii ni dhamana kubwa kwao. Kuwa makini na waangalifu, kuwa na maadili ya kiuongozi na wakweli wakati wote, kuwa wavumilivu na wenye subira kwa wenzetu ni tabia ambazo zitatufikisha salama, hivyo tuzikumbatie.
Majuzi hapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akilihutubia taifa, pamoja na mambo mengine alizungumzia sintofahamu iliyojitokeza kwenye mchakato wa majadiliano na hatimaye kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.
Mkuu wa Nchi, pamoja na kufafanua mambo mengine alisema:
"Nimeambiwa kuwa Kanuni za Bunge hazina sharti hilo hivyo Kamati haistahili kulaumiwa. Kama hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili Wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulauminiana isivyostahili. Hivyo basi, kuligeuza jambo hili kuwa ni suala la kukataa Muswada au kususia vikao vya Bunge au kufanya maandamano sidhani kama ni sawa."
Mhe. Dkt. Kikwete, katika hotuba yake alishauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili wabunge walizungumze. Mimi nimejiuliza tu kuwa linarudi katika sura ipi? Na je kurudi inamaanisha nini? Kwamba, mchakato ulikosewa – japokuwa Mhe. Rais anaweka wazi kwenye hotuba yake kuwa haukukosewa. Sasa kwa nini tunarudi nyuma – jibu hapo ni moja tu kuwa tunatafuta muafaka wa kitaifa wa kutupeleka kupata katiba mpya. Hili ni lengo la kila mwenye akili timamu. Nalikubali na nampongeza Rais wetu kwa uamuzi huu mzuri. Je, kurudi inamaanisha tunaanza upya ama tunaanzia wapi?  
Hoja ya makala yangu ni kushauri namna gani suala hili linarudi Bungeni na linarudi kwa muafaka wa kitaifa ambao ni nia ya wazi ya Mhe. Rais, kwa mujibu wa hotuba yake. Kwa kuwa hoja ya muswada huu ilipitia hatua zote za lazima za kikanuni, na kwa kuwa kuna kundi la wabunge walishiriki kikamilifu hata kufikia muswada ule kupita, na kwa kuwa imebakia sehemu moja ya 'Bunge' tu kukamilisha kazi ya kutunga sheria, ambayo ni Rais, ushauri wangu ni kuwa Rais aisaini kwa faida ya kuondoa uwezekano wowote ule wa kutengeneza matabaka ya wabunge 'walio wengi' (majority) kutokufurahishwa na hatua hiyo, kwa kitu ambacho wanaamini kilikuwa sahihi na kiliiva ipasavyo.
Pili, kwa kuwa kulikuwa na wabunge 'walio wachache' bungeni (minority) na kwa kuwa katika demokrasia yoyote ile yenye afya nzuri maoni na sauti za wachache ni lazima yasikilizwe kwa umakini zaidi hata ya wale walio wengi; na kwa kuwa kupitishwa kwa sheria ile haimaanishi kuwa ni lazima ilikuwa sahihi kwa asilimia 100; na kwa kuwa tayari Mhe. Rais amechukua jukumu lake la kiuongozi la kuliunganisha tena Bunge letu, ili liwe na sura ya umoja na mshikamano wa kitaifa, ni busara kurudi mezani na kusikilizana na kisha kuleta mapendekezo ya vipengele vinavyowakosesha usingizi na amani wapinzania kwa njia ya 'muswada wa mabadiliko ya sheria' (ambayo itakuwa imekwishasainiwa sasa na Rais).
Kuna swali litahitaji majibu kama uamuzi wa kuchukuwa njia inayoendana na ushauri wangu itafuatwa. Kwamba, ni namna gani tutarudi kuchukuwa maoni ya wazanzibari, yanayolalamikiwa na wapinzania, ilhali sheria itakuwa imeishasainiwa na kutakuwa kumeletwa vifungu tu vinavyohitaji kufanyiwa marekebisho? Maoni yatakuwa kwenye vifungu hivyo tu ama kwenye 'Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013' yote?
Na kama Mhe. Rais akiamua kufuata njia nyingine, na pekee iliyopo, nje ya hii ninayoipendekeza mimi, ni kuacha kusaini Sheria hii iliyokwisha kupitishwa. Kama akifuata njia hii kuna mambo mawili yanaweza kutokea; kununa kwa wabunge walio wengi na walioipitisha na kuharibika kwa ratiba nzima ya mchakato wa katiba, maana ifahamike wazi hapa kuwa bila kuwepo kwa sheria hii, Bunge la katiba halitoweza kuitishwa.
Madhara ya kuvurugika kwa ratiba ya mchakato wa katiba ni pamoja na kuchelewa kukidhi malengo ya kuwa na katiba mapema kabla ya kufikia muda wa kuanza chaguzi za serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hali hii ya kukwamisha zoezi itaweza kutufikisha kutenda dhambi ya kurefusha ratiba, kama walivyofanya Kenya – ambapo waliongeza mwaka mzima mbele ya ratiba yao ya uchaguzi, jambo ambalo halina uhalali wa kikatiba wa kuwa na muhula wa miaka 'mitano' ya uongozi zaidi ya 'utashi binafsi na uchu wa kuendelea kuwepo madarakani miongoni mwa sisi wabunge tuliopo sasa, tuhuma ambayo tutapaswa kuikiri  kama ilivyo, 'guilty as charged.'
Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB ni Mbunge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: http://www.peercorpstrust.org/ or http://www.hamisikigwangalla.com/
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment