Tuesday 8 October 2013

Re: [wanabidii] Rais Kikwete Asaini ama Asisaini...? Makala ya Ushauri Wangu kwa Mkuu wa Nchi.



Sawa kabisa, Rais Kikwete asaini muswada wa Katiba ili Tume ya Warioba imalize muda wake mara tu wakikabidhi rasimu hiyo kwa Bunge la Katiba, Bunge hilo lenye asilimia 75 ya wajumbe kutoka CCM ambao ni wabunge. Bunge hilo ambalo wajumbe wake 166 wanatokana na makundi maalum ambayo yatapeleka majina yao kwa Mh. Rais ambaye hatalazimika kuchagua wajumbe kutoka majina hayo aliyopelekewa.

Katika mchakato wa Bunge la Katiba, ikipigwa kura mara mbili bila kupata mshindi basi ikipigwa mara ya tatu basi asilimia 75 haitafuatwa na badala yake itaangaliwa walio wengi (simple majority)

Huo ndio muafaka wa Taifa, na Katiba hiyo itakuwa ni Katiba ya Wananchi, na hata wenzetu wa Zanzibar wataifurahia kwa vile mchakato wa kutafuta maoni na marekebisho ya sheria uliwafikia na wakashiriki sawa sawa. Tukifika hapo tutakuwa tumepata mwafaka wa Kitaifa na Katiba ya Wananchi, na siyo Katiba ya CCM kama watu wasioelewa mchakato ulivyo wanavyodai.



Wasalaam


2013/10/8 Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>

Rais Kikwete Asaini ama Asisaini Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

Imeandikwa na Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.

Kama Ningemshauri Rais Kikwete hata kidogo tu kwenye hili la Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, ningemshauri aisaini sheria hiyo; ushauri wangu unazingatia lengo moja kubwa – kutengeneza muafaka wa kitaifa, na kwa maana hiyo makundi yote ndani na nje ya Bunge ni muhimu ili afanikishe kutupatia lengo hilo. Pia, ili kupata muafaka na kundi moja ni busara kulinda ulichonacho mkononi kabla ya kile kilicho angani, kama wanavyosema wazungu kwenye semi zao kuwa 'one bird in hand is worth more than a thousand on a tree.' (inayotafsirika kama 'ndege mmoja mkononi ana thamani kubwa zaidi ya alfu moja mtini!').

Tayari Rais Jakaya Kikwete, kama Mkuu wa Nchi, anakuwa na jukumu la kimaadili na la kiuongozi kuhakikisha anatufikisha salama kama watanzania kwenye mchakato huu. Hatumtegemei asiwasikilize wapinzania na wadau wengine wote, hapana. Kuwasikiliza andiyo uongozi. Ni lazima awasikilize wote na atafute usawa kwenye mizania ya haki ili kuwe na muafaka wa kitaifa kwenye zoezi hili nyeti. Na binafsi nichukue fursa hii kumpongeza kwa kuwa msikivu, mvumilivu na mwenye kujenga madaraja na watu wote, badala ya uzio wa ukuta.

Kufanikisha mchakato wa kuandika katiba linapaswa kuwa jukumu la kwanza la kimaadili la watanzania wote tunaoishi leo. Kwa viongozi wote hii ni dhamana kubwa kwao. Kuwa makini na waangalifu, kuwa na maadili ya kiuongozi na wakweli wakati wote, kuwa wavumilivu na wenye subira kwa wenzetu ni tabia ambazo zitatufikisha salama, hivyo tuzikumbatie.

Majuzi hapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akilihutubia taifa, pamoja na mambo mengine alizungumzia sintofahamu iliyojitokeza kwenye mchakato wa majadiliano na hatimaye kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.

Mkuu wa Nchi, pamoja na kufafanua mambo mengine alisema:

"Nimeambiwa kuwa Kanuni za Bunge hazina sharti hilo hivyo Kamati haistahili kulaumiwa. Kama hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili Wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulauminiana isivyostahili. Hivyo basi, kuligeuza jambo hili kuwa ni suala la kukataa Muswada au kususia vikao vya Bunge au kufanya maandamano sidhani kama ni sawa."

Mhe. Dkt. Kikwete, katika hotuba yake alishauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili wabunge walizungumze. Mimi nimejiuliza tu kuwa linarudi katika sura ipi? Na je kurudi inamaanisha nini? Kwamba, mchakato ulikosewa – japokuwa Mhe. Rais anaweka wazi kwenye hotuba yake kuwa haukukosewa. Sasa kwa nini tunarudi nyuma – jibu hapo ni moja tu kuwa tunatafuta muafaka wa kitaifa wa kutupeleka kupata katiba mpya. Hili ni lengo la kila mwenye akili timamu. Nalikubali na nampongeza Rais wetu kwa uamuzi huu mzuri. Je, kurudi inamaanisha tunaanza upya ama tunaanzia wapi?  

Hoja ya makala yangu ni kushauri namna gani suala hili linarudi Bungeni na linarudi kwa muafaka wa kitaifa ambao ni nia ya wazi ya Mhe. Rais, kwa mujibu wa hotuba yake. Kwa kuwa hoja ya muswada huu ilipitia hatua zote za lazima za kikanuni, na kwa kuwa kuna kundi la wabunge walishiriki kikamilifu hata kufikia muswada ule kupita, na kwa kuwa imebakia sehemu moja ya 'Bunge' tu kukamilisha kazi ya kutunga sheria, ambayo ni Rais, ushauri wangu ni kuwa Rais aisaini kwa faida ya kuondoa uwezekano wowote ule wa kutengeneza matabaka ya wabunge 'walio wengi' (majority) kutokufurahishwa na hatua hiyo, kwa kitu ambacho wanaamini kilikuwa sahihi na kiliiva ipasavyo.

Pili, kwa kuwa kulikuwa na wabunge 'walio wachache' bungeni (minority) na kwa kuwa katika demokrasia yoyote ile yenye afya nzuri maoni na sauti za wachache ni lazima yasikilizwe kwa umakini zaidi hata ya wale walio wengi; na kwa kuwa kupitishwa kwa sheria ile haimaanishi kuwa ni lazima ilikuwa sahihi kwa asilimia 100; na kwa kuwa tayari Mhe. Rais amechukua jukumu lake la kiuongozi la kuliunganisha tena Bunge letu, ili liwe na sura ya umoja na mshikamano wa kitaifa, ni busara kurudi mezani na kusikilizana na kisha kuleta mapendekezo ya vipengele vinavyowakosesha usingizi na amani wapinzania kwa njia ya 'muswada wa mabadiliko ya sheria' (ambayo itakuwa imekwishasainiwa sasa na Rais).

Kuna swali litahitaji majibu kama uamuzi wa kuchukuwa njia inayoendana na ushauri wangu itafuatwa. Kwamba, ni namna gani tutarudi kuchukuwa maoni ya wazanzibari, yanayolalamikiwa na wapinzania, ilhali sheria itakuwa imeishasainiwa na kutakuwa kumeletwa vifungu tu vinavyohitaji kufanyiwa marekebisho? Maoni yatakuwa kwenye vifungu hivyo tu ama kwenye 'Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013' yote?

Na kama Mhe. Rais akiamua kufuata njia nyingine, na pekee iliyopo, nje ya hii ninayoipendekeza mimi, ni kuacha kusaini Sheria hii iliyokwisha kupitishwa. Kama akifuata njia hii kuna mambo mawili yanaweza kutokea; kununa kwa wabunge walio wengi na walioipitisha na kuharibika kwa ratiba nzima ya mchakato wa katiba, maana ifahamike wazi hapa kuwa bila kuwepo kwa sheria hii, Bunge la katiba halitoweza kuitishwa.

Madhara ya kuvurugika kwa ratiba ya mchakato wa katiba ni pamoja na kuchelewa kukidhi malengo ya kuwa na katiba mapema kabla ya kufikia muda wa kuanza chaguzi za serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hali hii ya kukwamisha zoezi itaweza kutufikisha kutenda dhambi ya kurefusha ratiba, kama walivyofanya Kenya – ambapo waliongeza mwaka mzima mbele ya ratiba yao ya uchaguzi, jambo ambalo halina uhalali wa kikatiba wa kuwa na muhula wa miaka 'mitano' ya uongozi zaidi ya 'utashi binafsi na uchu wa kuendelea kuwepo madarakani miongoni mwa sisi wabunge tuliopo sasa, tuhuma ambayo tutapaswa kuikiri  kama ilivyo, 'guilty as charged.'

Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB ni Mbunge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).



--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment