Saturday 26 October 2013

Re: [wanabidii] RAIS KIKWETE ANAWEZA KUONDOKA KABLA YA CCM 2015

mimi nadhani yeye ametoa tu mawazo yake baada ya kuona upepo wa kisiasa hata kama 
pia amechangia katika anguko la CCM.
Elias 
 
Elias Mhegera
Media & Information Officer 
Tanzania Human Rights Defenders Coalition 
Tel: 255-0754-826272
        255-0715-076272
Email: mhegeraelias@yahoo.com 
             mhegera@gmail.com 
The only thing we have to fear is fear itself 


On Saturday, October 26, 2013 10:21 AM, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Ndugu zangu 

Nimesoma habari kadhaa asubuhi ya leo vikikariri kauli ya rais kikwete ambaye ni mwenyekiti wa ccm kwamba ccm inaweza kuongoka mwaka 2015 .

Kauli hii nyepesi haiwezi kupita hivi hivi bila kuambiana ukweli .

Huyu raisi kikwete anayeitabiria CCM kuanguka mwaka 2015 anaweza kuanguka yeye mwenyewe aondolewe kwa kuondolewa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa CCM taifa na rais wa Jamhuri kwa ujumla tena na wabunge wake wenyewe maana amechangia zao la CCM la sasa yeye kama mwenyekiti hata kama ameifanyia nini CCM na TAIFA kwa ujumla .

Tunakumbuka kuanzia mwaka 1995 alipokatazwa kugombea urais na wakubwa wa CCM alianza kutengeneza mtandao wa kumwingiza madarakani mwaka 2005 – Kwenye mbio hizi tunaona propaganda na ubaguzi uliotumika dhidi ya wana CCM wenzake haswa salim ahmed Salim aliyeitwa Majina ya kibaguzi baguzi .

Mwaka 2005 kuelekea 2010 rafiki yake kipenzi aliachia ngazi kama waziri mkuu kesi hiyo mpaka leo haijulikani iliishia wapi na hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani au hata kusikia ameshinda au kushinda kesi .

Mwaka 2010 makundi ambayo yaliasisiwa na kikwete mwenyewe yanaendelea kimpango wao , baadhi yao walienda kuanzisha chama cha CCJ lakini wakaacha baada ya kupewa uwaziri na nafasi nyingine ndani ya CCM ,ubaguzi ule ulioanza miaka hiyo unaendelea kutafuna ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla .

Mwalimu JK – Bila CCM imara nchi itayumba 

Na ndio sasa tunaona CCM Si imara kama ilivyokuwepo miaka kadhaa iliyopita sasa hivi nchi inayumba kuanzia ubaguzi wa kidini , mkoa , ukabila , uchama na rangi yote haya yamekuwa ni fahari kwa baadhi ya makundi ya watanzania kuongelea na kusifiana .

MCHAKATO WA KATIBA 

Mara kadhaa rais kikwete amekutana na viongozi wa vyama vya upinzani ikulu kwake yeye na kwa wenzake wanaomshauri vibaya anaona Sifa na ni democrasia kitu ambacho sio kwamba amekubali kusaliti CCM yake kwa vyama vya Upinzani huko Ukulu .

Hivi vyama vya upinzani viliondoka vyenyewe bungeni kwa kususa na waliobaki walipiga kura kwa kukubaliana sasa iweje rais ambaye ni mweyekiti wa chama kilichopigia kura rasimu bungeni awaite na wabadilishe mambo ina maana hakubaliani na ule wingi wa wabunge wake ?

MWISHO .
Nasema na nasisitiza kwamba kabla ya mwaka 2015 rais kikwete anaweza kungoka yeye mwenyewe kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na wabunge wake mwenyewe ndani ya bunge kama akiendelea na hizi tabia tabia zake .

Tunashukuru kwa yale aliyoyatendea taifa hili lakini kwa hali ilivyosasa hivi yeye ashike nafasi yake la sivyo yeye ndio ataondoka ikulu kwa aibu 


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment