Saturday 5 October 2013

Re: [wanabidii] Papara za Kugawa Vitalu Vipya vya Gesi asilia: Tumerogwa, ujasiriamali binafsi ama Uzalendo uliopitiliza?

Nafikiri  ndugu Godfrey Mbanyi anachosema tumekishuhudia wengi. Kumbuka Dr. Slaa alivyoshambuliwa bungeni alipoleta hoja ya wizi wa fedha za EPA. Waziri muhusika alipinga kwa nguvu zote na wabunge wengi wa CCM walionekana kushabikia badala ya kufikiri na kutoa maamuzi bila kupoteza muda. Ilichukua muda mwingi kukubali na kutoa maamuzi.

Mfano mwingine ni hoja ya kutaka mabadiliko ya Katiba ilivyopingwa sana na waziri Kombaine na kutetewa na wabunge wa CCM kwamba Tanzania kwa sasa hahitaji kubadilisha katiba na kwamba iliyopo inatosha.Leo hii hao hao ndo wanajifanya machampioni wa hoja za mabadiliko ya katiba. Hii ndo bongo bwana! hivi huwa hamjui kwamba tunakumbukumbu kama hizo. Hoja hata kama ni ya msingi kiasi gani kitu kinachoangaliwa ni nani na anatoka chama gani ili tumsupport na ikibidi tumtukane kama si wa chama chetu. Hadi wapiga kura tunabaki tukijilaumu kwa uamuzi wetu mbovu wa kuwapeleka watu bungeni wasiokuwa na uwezo wa kuchambua hoja bali matusi


2013/10/5 Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
Jovias, Zitto alikuwa kwenye mkutano nje ya jiji la Dar es salaam lakini tutaonana na tutashirikiana kuhakikisha hawagawi vitalu vingine zaidi, walivyogawa vinatosha...tujenge uwezo wetu wa kisheria na kitaasisi kwanza


2013/10/5 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Hivi sie wasomi wa mabadiliko tunamatatizo ya uelewa. Saizi tunashupaa vile Dr. Hamis kaandika lakini hii kitu ilishaingia humu mabadiliko tupunguzeni ubigwa wa kujadili watu tujadili vitu vya msingi.

Kama kuna kitu cha msingi kakiongelea tukiangalie, SASA nyie wabunge tusaidieni hili. Jana nilisoma Dr. ulikuwa unajaribu kuwasiliana na mheshimiwa ZITTO sijui kama mliwasiliana. Ila kwa ufupi inaonyesha wabunge wetu kama mna meno basi bunge la tanzania halina meno.

Huu upuuzi umpitiliza kiasi. Ndugu yangu kakak Kamala utakuwa umeelewa nilipoongelea wasi wangu wa watanzania kuwa na uwezo wa kutumia ubongo.

Haitoshi kulalama tu humu nyie wabunge u have to do something about it. Huu si muda wa kutafuta kuonyesha uwezo wa kujua mambo bali muda wa kugeuza giza kuwa mwanga there is no better opportunity to serve Tanzanians than this time tusaidieni kututoa kwenye shimo hili badala ya upuuuzi wa NDIOOO MIA KWA MIYA.

Nape hii ndo kazi bora ya chama chako?


2013/10/4 godfred mbanyi <mbanyibg@yahoo.com>
Dr. HK,

Hoja nzuri, lakini mbona wenzenu wa Upinzani wakiuliza mambo kama haya ambayo ni nyeti kwa Taifa , wewe na nduguzo wa CCM mnawazodoa, kuwazomea na kuwakejeli???
Una utashi wa kweli katika hili??
Nauliza tu Mheshimiwa!!!


--------------------------------------------
On Fri, 10/4/13, Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Papara za Kugawa Vitalu Vipya vya Gesi asilia: Tumerogwa, ujasiriamali binafsi ama Uzalendo uliopitiliza?
 To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, afya-club@googlegroups.com
 Date: Friday, October 4, 2013, 11:36 AM




 Papara za Kugawa Vitalu Vipya vya
 Utafiti wa Gesi Asilia Bila
 Sera, Sheria na Kanuni: Tumerogwa, Ujasiriamali Binafsi ama
 Uzalendo
 Uliopitiliza? (I)

 Na Hamisi Kigwangalla,
 MB.

 Wakati wa kipindi cha bunge la
 bajeti, Prof. Sospeter
 Mwijarubi Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini, aliliarifu
 bunge kuwa serikali
 ilikamilisha kazi ya kuipitia mikataba ya gesi asilia mnamo
 mwezi Novemba 2012 na
 akasema kuwa "kukamilika kwa kazi hiyo kumeiwezesha
 serikali kubaini maeneo
 yanayohitaji kuboreshwa katika mikataba hiyo. Pia, matokeo
 ya uchambuzi wa
 mikataba hiyo yatasaidia katika uundaji wa sera, sheria na
 kanuni za usimamizi
 wa sekta ndogo za mafuta na gesi asilia itakayokidhi matakwa
 ya watanzania." Kanuni
 hii ilinithibitishia jambo moja, kuwa hatuko sawa katika
 njia tunayopita
 kuelekea kufanya uvunaji wa raslimali hii adhimu na urithi
 wetu wa bure; kwamba
 hatuna sera, sheria na kanuni, sasa tunaendeleaje kutoa
 vitalu vipya kila siku?


 Ufahamu wangu mdogo kwenye mambo
 haya umeniwezesha kuamini
 kuwa sheria ya petroli (The petroleum (exploration and
 production) act) ya
 mwaka 1980 haikidhi haja ya kuendesha kazi za utafiti na
 uzalishaji wa gesi asilia,
 na hata biashara ya gesi asilia. Hata nilipoisoma ile sera
 mpya ya gesi (draft)
 nilibaini wazi kabisa nayo inakiri kuwa hatuna mfumo
 madhubuti wa kisheria na
 kitaasisi, yaani 'legal and regulatory framework', wa
 kuendesha vizuri sekta
 hii nyeti.

 Prof. Sospeter Muhongo aliwahi
 akinukuliwa akisema kuwa
 tusipokimbia kuanza kuvuna gesi, majirani zetu watatuwahi.
 Kwani gesi inaoza?
 Sasa tunavyokimbia namna hii bila kujua tunafaidikaje si
 tutajikuta tumefika
 kwenye gesi sawa na wenzetu ama tumewawahi lakini
 hatuifaidi, kipi bora sasa? Leo
 hatuna sera, tunajuaje wajibu wa kila mtu kwenye shughuli za
 uvunaji? Ambapo
 gesi inachimbwa, watu wenyeji wana haki na wajibu upi?
 Masuala ya fidia kwa
 wananchi watakaoathirika kwa namna moja ama nyingine
 yamekaaje? Wenzetu wa
 Kenya wamezuia mafuta yao yasichimbwe mpaka kwanza wawe na
 sera, sisi
 tunakimbilia wapi?

 Wakati tukikiri kuwa hatuna sera,
 sheria na kanuni mpya na
 za kisasa zinazoweza kukidhi mahitaji ya Taifa ya uvunaji na
 uwekezaji kwenye
 sekta hii nyeti, hivi majuzi Wizara ya Nishati na Madini
 imetoa tangazo la
 kualika wawekezaji kwenye 'mkutano na maonesho ya pili ya
 Tanzania ya mafuta na
 gesi 2013' utakaofanyika Dar es salaam ukumbi wa Mwalimu
 Nyerere International
 Convention Center kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi huu
 (oktoba), ambapo mzunguko
 wa nne wa kugawa leseni za vitalu vya gesi kwenye bahari kuu
 na kaskazini mwa
 ziwa Tanganyika (The 4th Tanzania offshore and
 North Lake Tanganyika
 licensing round) utazinduliwa.

 Katika tangazo hilo lililotolewa na
 Wizara ya Nishati na
 Madini kupitia shirika letu la uendelezaji petroli nchini
 (Tanzania Petroleum
 Development Corporation, TPDC) vitalu saba vyenye ukubwa wa
 wastani wa kilomita
 za mraba 3000 kila kimoja vitagawiwa kwenye bahari kuu kwa
 mtindo wa kuwapa
 wawekezaji leseni za utafiti kwa asilimia 100 na vitalu
 viwili vitabaki kuwa
 mali ya serikali chini ya shirika lake la TPDC ambapo
 atatafutwa muwekezaji mshirika
 wa kufanya naye utafiti wa pamoja. Vitalu vikigawanywa kwa
 mtindo wa kuwaachia
 wawekezaji jukumu la utafiti (exploration) maana yake ni
 kwamba kuanzia siku ya
 kwanza ya utafiti wanaanza kurekodi gharama zao na
 wakimaliza na kufanikiwa
 kugundua gesi, wanapoanza zoezi la kuivuna na kuiuza sasa
 hiyo gesi wanaanza
 kukata asilimia si chini ya 70 ya mauzo yote kama gharama
 zao. Asilimia 30 tu
 inayobaki ndiyo itagawanywa kwa Tanzania kupata asilimia 60
 na wawekezaji
 kupata asilimia 40. Hii kwa lugha ya kitaalamu wanaita ni
 'production sharing
 agreement (PSA).' Hapa kuna maswali mengi sana ya
 kujiuliza, nani anafanya kazi
 ya kuzihakiki gharama wanazoingia hawa wawekezaji ili
 watakapokuja kuanza kuzikata
 tuwe na uhakika kuwa ndizo gharama halisi walizotumia?

 Na katika vile vitalu viwili
 ambavyo anapewa TPDC mkataba
 utakuwa tofauti kwa kuwa kuanzia mwanzoni shirika letu
 wenyewe litaingia kwenye
 utafiti hadi uzalishaji na hatimaye mauzo. Na hapa kwa
 hakika tutarajie kuwa na
 mgao mkubwa zaidi wa faida kwa kuwa tutakuwa tumeshiriki
 toka mwanzoni. Na hata
 kama mbia wetu akisema ameweka gharama fulani tutaweza
 kuzihakiki maana na sisi
 tumo. Pia hata uhamishaji wa utaalamu na teknolojia
 (technology transfer),
 kujenga uwezo wetu wa kiuendeshaji wa zoezi hili la uvunaji
 wa raslimali za
 gesi asilia na mafuta na hata wa kifedha ni jambo
 litakalofanyika kirahisi
 katika mtindo huu, na siyo ule wa kuligeuza taifa letu
 shamba la bibi kwa
 kuwaachia mabeberu waje wavune tu. Huu ndiyo mfumo wa
 kufuatwa na nchi yoyote ile
 yenye watu wazalendo, wanaojitambua na wanaojua biashara. Na
 ambao wako 'serious'
 dhidi ya vita ya kupambana na umaskini. Wanaoguswa na shida
 za wananchi za siku
 hadi siku, wanaoongozwa na utaifa na si na njaa za matumbo
 yao.

 Leo kampuni ya Statoil ya Norway
 aliyegundua visima vya gesi
 huko kwenye bahari kuu ya Tanzania ni kampuni inayomilikiwa
 na serikali yao kwa
 zaidi ya asilimia 67, na imeitajirisha nchi yao. Pia kampuni
 kama Petronas ya
 Malaysia, National Gas Company ya Trinidad and Tobago
 zinafanya kazi kwa
 kufuata 'model' ya Norway.

 Kwa nini sasa TPDC isiwe
 'Statoil' ya Tanzania? Hili ni
 swali lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni
 moja. Namtaka Prof.
 Sospeter Muhongo, ambaye amekuwa akijinasibu kwa usomi wake
 awajibu watanzania.
 Aoneshe uwezo wake. Awaambie watanzania elimu yake
 imetusaidia nini kuleta
 majibu ya swali hili.

 Swali lingine lenye kunitatiza na
 naamini pia watanzania
 wengi linawatatiza ni kwamba, ni kwa nini tunaharakisha
 namna hii kuingia
 kwenye ugawaji wa vitalu vya gesi ilhali hatuna sera, sheria
 na kanuni mpya? Waziri
 huyu msomi na mtafiti haoni hatari ya hizi papara zetu
 kweli? Haoni hatari ya
 kumaliza kugawa vitalu vyote kisha kurudi kinyume nyume sasa
 kuanza kuomba
 mikataba na wawekezaji irekebishwe kufuata sera, sheria na
 kanuni mpya? Na hapo
 wanasheria watakuwa wameishaweka vipengele vya kutuzuia
 kufanya hivyo
 (stability clauses) kwenye mikataba na hatimaye kuishia
 kuwapigia magoti
 kuwabembeleza tu?

 Kila siku tunazungumzia uwazi
 kwenye sekta hizi za raslimali
 ya gesi, mafuta na madini na Tanzania imesaini mkataba wa
 kimataifa wa uwazi
 kwenye sekta hizi (Extractive Industries Transparency
 Initiative), hivi kuna
 uwazi kweli hata kidogo tu kwenye haya maamuzi ya Prof.
 Muhongo na maluteni
 wake pale Wizara ya Nishati na Madini? Kwanza wanapata wapi
 uhalali (legitimacy)
 wa kusaini mikataba kwa kutumia sheria ambayo wao wenyewe
 wanakiri imepitwa na
 wakati na ndiyo maana wameanzisha mchakato wa kutunga sera,
 sheria na kanuni
 mpya?

 Hakuna atakayebisha kuwa ili tuwe
 salama ni lazima twende
 kwa hesabu sana, kwanza tuwe na mfumo thabiti wa kisheria na
 kitaasisi (strong legal
 and institutional framework); sasa leo hii ndiyo
 tunahangaika kuandika sera, na
 kusomesha raslimali watu kwenye sekta hizi, ni lini wataiva
 na kuanza kutumika
 - miaka zaidi ya mitatu ni lazima ipite!

 Prof. Muhongo hivi anazo kweli
 takwimu za kodi tulizopata
 kutokana na migodi mikubwa ya uchimbaji wa dhahabu? Hana
 taarifa kuwa tulianza
 kupata kodi pale Rais Kikwete alipoamua kuingilia kati na
 kuanzisha mazungumzo
 na wawekezaji hawa kufuatia tume ya Jaji Bomani ndipo
 tuliposhuhudia wakianza
 kulipa kodi ya kampuni (corporate tax) ya asilimia 30? Kabla
 ya hapo kila siku
 walikuwa wakisema hawafanyi faida na hivyo hawapaswi kulipa
 kodi. Leo kuna
 kampuni ngapi za uchimbaji wa dhahabu zimefunga migodi yao
 bila kulipa hata
 shilingi moja na nyingine kulipa miaka miwili hadi minne ya
 kurashia rashia tu
 kwa 'soni' ili kujijengea mazingira rafiki ya kupewa
 kitalu kipya wavune tena
 dhahabu? Wakati wimbi la kuingia kwa wawekezaji hawa wakubwa
 kwenye migodi ya
 dhahabu linashika kasi, kisingizio cha kuwaondoa kwa nguvu
 wachimbaji wadogo na
 wananchi wenyeji wa maeneo hayo kwenye maeneo yao (kama
 wageni kwenye nchi yao)
 kilikuwa tuwakaribishe wawekezaji watalipa kodi, watajenga
 shule na hospitali,
 wataongeza ajira nchini n.k. Hivi ni shule ngapi zimejengwa
 kwa mfano na
 Resolute pale kwetu Nzega? Wananchi wenyewe wameweza kujenga
 shule ngapi kwa
 pesa ya kilimo cha jembe lao la mkono tu? Sheria mpya ya
 madini ilipokuja
 imetusaidiaje sisi kama Taifa? Tumekuwa na sheria nzuri
 lakini haina meno
 kwenye mikataba ya zamani.

 Wawekezaji hawakuleta maendeleo
 yoyote ya kupigia mfano,
 ambayo hata leo unaweza kuonesha. Hakuna tofauti kati ya
 Nzega iliyokuwa na mgodi
 mkubwa wa dhahabu na Igunga ambayo haikuwa na mgodi mkubwa
 kama ule katika
 kipindi hicho hicho – inakuwa bora hata Mwadui ya
 Williamson Diamonds kule
 Shinyanga ina utofauti na vijiji jirani na hata mjini
 Shinyanga kwa wakati ule!
 Wawekezaji kwenye sekta ya dhahabu hawakuleta maendeleo kwa
 wenyeji
 wanaowazunguka wakidai kuwa hawawajibiki kimkataba kufanya
 hivyo. Je, tumejipangaje
 kwenye sekta ya gesi? Kwa nini tusitulie kwanza,
 tukatengeneza sera ya
 kuwahudumia wenyeji ( a policy on local content initiatives)
 ili 'tuwawajibishe'
 wawekezaji, tujue wenyeji watafaidikaje na nchi
 itafaidikaje, na wao
 washirikishwe kwenye mchakato huo ili twende pamoja?

 Kama ilivyo kwa mambo yote
 yanayoendelea kwenye gesi, na
 kama ilivyokuwa kwenye ile sekta ya madini, usiri wa maksudi
 ama wa kutojua
 umegubika namna ya wenyeji kufaidika. Tunaambiwa watanzania
 wataajiriwa, watauza
 bidhaa zao kwenye makampuni ya madini na uchumi wa maeneo
 hayo utakuwa kwa
 kasi, mchanganuo wa kina wa namna haya yatakavyotekelezeka
 umeandikwa kwenye
 sera, sheria ama kanuni ipi? Mkakati wa kuwawezesha wazawa
 wafanikishe haya kwa
 viwango vinavyotakiwa uko wapi? Maana haya makampuni huja na
 'viwango' vyao vya
 nyanya na vitunguu na vinginevyo, sasa je sisi tumejiandaa
 vipi kuwawezesha
 wenyeji wafaidike na soko hili jipya na la uhakika?

 Je, tuna sera gani ya kutunza na
 kutumia mapato yanayotokana
 na gesi? Kwa sasa, kwa ufahamu wangu, hatuna. Kwa nini
 tusijipange tukatunga
 sera, sheria na kanuni safi za kutuongoza, tukajenga mtaji
 wa raslimali watu ya
 kutosha, tukawekeza mtaji kwenye TPDC yetu ndipo tukaingia
 sasa kutafuta 'wabia'
 wa kusaidiana nao kutafiti na hatimaye kuwekeza, siyo wa
 kuwapa vitalu 'wawekeze!'.
 Watanzania tunatamani tuwe na TPDC inayofanana na Statoil.
 Je, Prof. Muhongo
 yuko tayari kutupa hiyo?

 Tukikamilisha mchakato wa kujenga
 mfumo thabiti wa kisheria
 na kitaasisi kwa njia ya kidemokrasia ya uwazi na shirikishi
 tutakuwa tumewapa
 uhalali akina Prof. Muhongo na wenzake sasa kufanya maamuzi
 ya utekelezaji
 yanayofuata sera, sheria, kanuni na mikakati iliyowekwa.


 Kwa nini tusijipange kuifanya TPDC
 yetu kuwa 'Statoil' (mwekezaji)
 kwenye nchi nyingine huko tunakoelekea? Kama tungeliamua
 vema huko tutokako, STAMICO
 leo ingekuwa tajiri na ingekuwa inachimba dhahabu kama
 Ashanti Goldfields Corporation
 ya Ghana. Tusikosee tena kwenye gesi.



 Tuna haraka gani, na ya nini? Ya
 kwenda wapi? Kuhakikisha tu gesi imechimbwa – na kwamba
 sisi kufaidika ama
 kutofaidika siyo ishu? Kwani kuna umaarufu gani tunaupata
 kwa kugawa vitalu vya
 gesi vyote leo? Na mwani ni lazima wavigawe vyote hao
 waliopo wizarani leo? Tunatunga
 sera, sheria na kanuni mpya ili zije zitumike kwenye nini
 wakati vitalu vyote
 tunagawa leo kwa kutumia sheria ya kizamani? Haya ni maswali
 yanayohitaji
 majibu kuntu. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo akipenda
 anaweza kuja kutukata
 kiu yetu ya kujua. Atuelezee kwa kina. Na kama anataka nchi
 hii imkumbuke kwa
 kushiriki kuijenga afanye uamuzi sahihi - asimamishe ugawaji
 wa vitalu vipya
 vya gesi, akamilishe mchakato wa kujenga mfumo wa kisheria
 na kitaasisi ndipo
 aendelee. Ila kama anataka alaumiwe na vitukuu na
 vining'ina vyake mwenyewe
 aendelee na hii papara yake.



 Dkt. Hamisi
 Kigwangalla (MB) ni Mbunge
 wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala
 za Mikoa na
 Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


 --
 "Vision is the ability to see the invisible!"
 Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
 P.O.Box 22499,
 Dar es salaam.
 Tanzania.
 Phone No: +255 754 636963
                 +255 782 636963

 website: www.peercorpstrust.org
 or www.hamisikigwangalla.com
 Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org
 or info@hamisikigwangalla.com

 Skype ID: hkigwangalla
 Blog: blog.hamisikigwangalla.com 






 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to
 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment