Thursday 24 October 2013

Re: [wanabidii] Ni kweli mchanga wenye madini unasafirishwa

Utabebwa sana sisi vitu vya muhimu ni kuongelea biashara za watu na vyama vya siasa.
Waandishi wa habari wala rushwa haiwezekani hawayaoni haya!
Nchi ya walalamikaji wabinafsi waroho na wapenda utajiri bila jasho. Hii ndo Tanzania ya leo

On Oct 21, 2013 3:41 AM, "Yona Maro" <oldmoshi@gmail.com> wrote:
Ndugu zangu ,

Kuna watu kadhaa wamewahi kulalamika kuhusu mchanga wenye madini kusafirishwa nchi za nje haswa katika bara la asia katika nchi ya india na china kwa ajili ya matumizi ya viwanda vya huko .

Mara ya kwanza nilisikia kuhusu hili nilivyofanya ziara katika migodi ya bulyanhulu , northmara , buzwagi na mengine inayomilikiwa kwa asilimia kubwa na wawekezaji kutoka nje ya nchi haswa ulaya ya magharibi .
Kwenye ziara hizi ukiuliza utaambiwa ule ni uchafu tu na hata serikali inajua kinachosafirishwa kwamba ni uchafu tu , lakini kama ni uchafu tunajiuliza kwa nini usiharibiwe au kwa nini unapelekwa nchi za nje ?

Tukiachana na hayo ya sehemu zinazojulikana kabisa kusafirisha mchanga huo kuna sehemu ambazo hazijulikani rasmi lakini zinasafirishwa mchanga tena kwa kiasi kikubwa kupelekwa nchi za mbali kwa ajili ya utendaji wa kazi mbalimbali .

Moja ya eneo hili ni maeneo ya mkoa wa kagera ambapo wataalamu wetu toka chuo Fulani kikubwa nchini walishindwa kugundua aina ya mchanga huo , mwingine uko maeneo ya songea ambao inasemekana kuna wanasiasa wameingia mkataba na kampuni moja ya kutengeneza simu inayotumia mchanga huo , maeneo ya morogoro , iringa na Dodoma pia kuna mchanga huu .

Kuna eneo lipo karibu na kijiji cha nyumbani kwa raisi wa Tanzania pale msoga , kuna mchanga wa thamani pale na mgunduzi wake yuko amejichokea baada ya utafiti huo lakini wajanja wameshajichukulia na kumiliki hiyo ardhi na kuna kiwanda ambacho si rasmi sana kwa ajili ya mchanga huo .Hapa ni eneo ambalo shule ya maana hamna ya maana iko mbali huko Bagamoyo , huduma za maji za shida ingawa kuna mradi wa maji unaopeleka maji dsm karibu tu .

Wakati tunaendelea na mchakato wa katiba mpya ni vizuri wadau wakumbuke suala la ardhi na mali zinazopatikana chini ya ardhi ya Tanzania , hili lisipopatiwa ufumbuzi sasa linaweza kuleta vurugu huko mbeleni .

--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment