Thursday 10 October 2013

Re: [wanabidii] MGOGORO WA WASAFIRISHAJI SERIKALI ILAUMIWE

Monica,
Serikali haiwezi kufufua reli kwa kuwa viongozi wengi wa serikali (mafisadi) ndio wamiliki wa malori hayo. Wafufue reli malori yao yakose kazi ya kufanya na kuwakosesha biashara ya usafirishaji? Hapana. Reli ya Kaskazini na Kati zimeuliwa makusudi na watawala ili magari yao yatumika kusafirisha mizigo kwenda bara. Chezea mafisadi wewe!



On Thursday, October 10, 2013 2:20 PM, Monica Malle <moninaike@hotmail.com> wrote:
Nimekuwa najiuliza maswali mengi tangu mgogoro wa serikali na wsafirishaji uanze. Serikali inabidi ilaumiwe kwa kuwaachia wasafirishaji watumie malori makubwa kusafirisha mizigo. Kwanini wasiboreshe na kutengeneza miundo mbinu ya reli ikawa ndio njia kuu ya usafirishaji badala ya kuachia secta muhimu kama hii kwa uchumi wa nchi kuendeshwa na watu binafsi? Madhara yake ndio hayo sasa wasafirishaji wanakuwa na kiburi kwababu wanajua wao ndio wameshikilia uchumi. Nadhani muda umefika sasa serikali ufufue reli ya kati kubeba mizigo na kukarabati ile ya dar - Tanga hadi Arusha ili bidhaa nyingi zisafirishwe kwa njia ya reli na hii itaondoa ukiritimba wa wasafirishaji na pia itakuwa na unafuu kwa wanaosafirsha mizigo yao na mwisho nafuu kwa mtumiaji wa mwisho.
Mh. Magufuli wacha malumbano na wasafirishaji kwa sasa wameshika mpini wewe umeshika makali yatakukata, la muhimu fufua reli zifanye kazi ndio ubora wa kazi yako utaonekana. 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment