Wednesday 9 October 2013

Re: [wanabidii] “Kwa Heri Dr. Hashim Msafiri Twakyondo...Umefundisha Wengi”

Inna illah wainaaillah rajuun, allah amweke mahala pema, amin

On 10/9/13, lesian mollel <aramakurias@yahoo.com> wrote:
> rip mwalimu msafir
>
>
>
>
>
> On Wednesday, October 9, 2013 4:13 PM, James Patrick <mimiwewetz@gmail.com>
> wrote:
>
> ----- Forwarded Message -----
>
>
> This message is eligible for Automatic Cleanup! (mimiwewetz@gmail.com) Add
> cleanup rule | More info
>
> Roho ya Marehemu ipumzike kwa amani,
>
> Alinifundisha  wakati akiwa head of Computer Science 2001 na baadae master
> 2010 ( he was Guru on Free Open Source Software - FOSS)
>
>
>
>
> 2013/10/9 Mwema Felix <mwema.felix@gmail.com>
>
> Poleni sana familia, ndugu, jamaa, marafiki na familia ya chuo kikuu cha
> DSM.
>>Apumzike kwa amani.
>>
>>
>>
>>2013/10/9 Mathew Mndeme <mathewmndeme@gmail.com>
>>
>>Ijumaa  ya tarehe 4/10/2013 wiki iliyopita tulikua
> kwenye kikao cha kazi ambacho kilihusisha wahadhiri wote wa kitivo chetu na
> kilifanyika hadi jioni kabisa. Alikuwepo mmoja wa wahadhiri waandamizi
> ambaye
> wengi wetu tulikua hatujaonana naye kwa muda mrefu wala kumuona kwenye
> vikao.
> Mwaka jana alikua amechukua likizo ndefu kwa ajili ya kazi za kitaaluma na
> baadaye nadhani alikua ana mambo mengine nje ya eneo la kazi na nje ya nchi
> pia, hivyo kutoonekana mara kwa mara. Nakumbuka pale kwenye kikao alikua
> amekaa
> sambamba na nilipokua nimekaa na tulipoona muda umekwenda sana na kikao
> kikiendelea nilimuuliza kikao kinakwenda hadi saa ngapi naye akanijibu
> hajui
> ila muda umesogea sana. Kwa kuwa hali ya chumba cha mkutano ilikua ina joto
> nilipata kiu sana na niliamua kwenda kuchukua maji ambapo naye alinimba
> nimpe
> chupa moja. Nakumbuka kuna kamati ndogo iliundwa kufuatilia jambo fulani na
> yeye alikua mmoja wa waliombwa kutoa mchango wake kwenye hiyo kamati
> kutokana
> na uzoefu na maarifa yake jambo ambalo alilikubali. Baada ya kikao kwisha
> kamati ile ndogo ilikaa kwa dakika chache kujadili lile jukumu. Tulipoagana
> pale eneo la kikao ilikua inakaribia saa kumi na mbili hivi za jioni.
>>>Kesho yake (Jumamosi ya tarehe
> 05/10/2013) asubuhi na mapema tukapigiwa simu na kuambiwa kuwa Dr. Hashim
> Twakyondo amefariki dunia. Kusema ukweli nilishtuka na nilibisha kwanza
> kuwa
> huenda habari sio za kweli huku nikiendelea kuuliza maswali yasiyo na
> mpangilio. Tulipouliza, tukaambiwa kuwa hiyo asubuhi ya Jumamosi alimka kwa
> lengo la kwenda shamba hivyo akaondoka yeye na mke wake na mtoto wao wa
> mwisho
> wa kiume ambaye ndiye alikua anaendesha gari. Alionekana mzima wa afya na
> asiye
> na tatizo lolote. Lengo ilikua ni wapite kwanza gereji kuweka gari sawa
> halafu
> waende shamba. Wakiwa ndio wametoka tu nyumbani eneo la Makuburi akaanza
> kuwaambia kuwa anajisikia vibaya na baada ya muda wakaona kama anaishiwa
> nguvu.
> Wakaamua wampitishie hospitali ya Amana maana ni njia waliyokua wanaipita.
> Ila
> kabla hawajafika hospitalini ikawa ndio keshatangulia kule kifo
> kinapopelekaga
> roho za watu. Ilinisumbua sana na kuwaza huenda Dr. Twakyondo alikuja
> kwenye
> kikao kile kutuaga, na siyo yeye wala sisi tuliogundua hilo. Labda kwa
> baadhi yetu
> ingekua rahisi kupokea habari za msiba ule iwapo tusingekutana naye jioni
> ile
> kwa vile hatukua tumemuona kwa muda mrefu.
>>>Dr. Twakyondo amekitumikia chuo
> Kikuaa cha Dar es Salaam kwa takribani mika 30 akipanda nfazi kutoka
> mkufunzi
> hadi mhadhiri mwandamizi. Pamoja na kazi yake ya kitaaluma, amekua kiongozi
> kwa
> muda mrefu akiongoza idara ya Kompyuta Sayansi kwa miaka trakribani saba na
> baadaye kuwa mkurugenzi wa kitendo cha elemu mtandao cha Chuo Kikuu kwa
> miaka
> sita. Mafanikio haya ni ushahidi tosha kua amefanya mengi ya kukumbukwa na
> kuondoka kwake ni pengo kubwa litakalochukua muda kuliziba.
>>>Tulipokua tunaaga mwili nyumbani
> kwake juzi Jumatatu, watu walikua ni wengi sana, kitu kilichodhihirisha Dr.
> Twakyondo alikua mtu wa aina gani kwenye jamii. Wasifu wake uliposomwa
> yalijulikana mambo mengi aliyokua ameyafanya, kuyafanikisha na mengine ndio
> alikua kaanza kuyafanya hasa kwenye utaalamu wake katika tasnia ya Sayansi
> ya
> Kompyuta. Kwa wale amboa wamepita katika fani hii, na ukweli kuwa Chuo
> Kikuu
> cha Dar es Salaam ndio kitovu cha fani ya Kompyuta katika ukanda huu wa
> Afrika
> Mashariki, wataungana nami kuwa Dr. Tywakyondo alikua ni Mwalimu wa wengi
> na
> alifanya mengi kwa sehemu yake.
>>>Kama ilivyokua kwangu tangu
> niliposikia msiba huu, kila niliyemsikia pale msibani alikua anasikitishwa
> na
> namna alivyoondoka. Wengi walikua na huzuni kuwa ameondoka kwa haraka, kwa
> kushtukiza, na pasi kujulikana ugonjwa na huenda. Kifo kimemshtukiza kama
> kilivyowashtua aliowaacha. Mzee Yusuph Makamba akiwa kama sehemu ya
> wanafamilia/jamaa
> zake alipewa nafasi ya kuongea. Kama kawaida ya ucheshi wake aliongea mengi
> lakini mojawapo alisema kuwa marehemu alikua anajiandaa kuwa mbunge wa
> jimbo
> fulani mwaka 2015. Akasema yeye ndio alikua anaongoza kamati ya fitna
> kuhakikisha hilo linafanikiwa pamoja na marehemu kupata cheo kingine ndani
> ya
> chama. Akasema kuwa Ijumaa kabla hajafariki walikua wamewasiliana kuwa
> walikua
> waonane Jumapili ili ampe taarifa mpya za fitna za kuelekea 2015 na kuweka
> mikakati vizuri zaidi.
>>>Pamoja na hili la siasa, kwa upande
> wa kazi nilikua nina taarifa  kuwa
> marehemu ndio alikua amenza kupitia mchakato wa kupandishwa cheo na kuwa
> uprofesa ambayo ni ngazi ya juu kabisa katika taaluma.
>>>Ninapoombeleza kifo cha Dr. Twakyondo
> na jinsi alivyokua na yale niliyoyosikia wakati wa mazishi yake juu ya
> aliyoyafanya na mipango aliyokua nayo, napata mawazo mengi juu ya maisha
> baada
> ya kifo. Sio tu kwa ajili ya nini kitatokea na kuendelea kwenye roho yangu
> baada ya kufa, bali juu ya wale tunaowaacha na jinsi watakavyoathiriwa na
> kuondoka
> kwetu. Ninapata maswali mengi; Je marehemu alikua amejiandaa kiasi gani
> kuwa
> atakufa? Alikua ameweka mambo ya nyumba yake vizuri kama matayarisho ya
> kuondoka kwake? Katika yale yote aliyojishughulisha nayo, nini kitaendelea
> katika kutokuwepo kwake?
>>>Sina majibu ya maswali haya na wala
> sijajishughulisha kuyatafuta. Lakini kama mwanadamu ninawaza tu kuwa huenda
> Mwalimu wangu hakuwahi kuwaza kuwa kuna kufa karibuni. Huenda alikuangalia
> kufa
> kama tukio la baada ya uzee uliotukuka akiwa kama profesa na mwanasiasa
> aliyestaafu iwapo ni kweli  ndiko
> alikokua anakwenda kama alivyotuambia Mzee Makamba. Wengi wetu huwa
> tunaposikia
> kuwa wengine wamekufa, tunasikitika na kuombeleza halafu tunaishia hapo.
> Tunapojifikiria sana tunaona  kufa kwa
> upande wetu bado ni jambo la baadaye sana na hivyo hatujishughulishi
> kufanya
> matayarisho yoyote ya nini kiendelee baada ya kufa kwetu. Tunawaza huenda
> kufa
> kwetu utatokea baada ya matukio mengine kadha wa kadha kwenye maisha yetu.
>>>Kwa wale wanaamini katika Mungu  na kuwa kuna mwisho wa maisha haya ya
>>> damu na
> nyama, wako wanaojitahidi sana kukesha katika maombi na utakatifu kuwa
> iwapo
> siku ya tukio ikifika basi wakutwe wako tayari na wana wasifu wa
> kuwawezesha
> kuyaendea yale makao mapya na ya milele. Ila sina hakika kama wengi
> wanapiga
> hatu ya pili na kuajiandaa pia namna ya kuziacha familia zetu na mambo
> mengine
> sawa iwapo tutakufa muda wowote. Wengi wetu tunawaza tu juu ya yale
> yatakayotokea kwetu na nini twatakiwa tufanye kuamua hayo...lakini huenda
> hatuwazi kabisa juu ya wale tutakaowaacha na kupunguza madhara ya
> kutokuwapo
> kwetu kwenye maisha yao.
>>>Shuhuda ni nyingi za familia ambazo
> baada ya baba au mama kufariki, ulikua ni mwanzo wa kila kitu kukaa
> kushoto.
> Kumekua ni mwanzo wa watoto kuharibika/kuharibikiwa; imekua ni mwanzo wa
> kifo
> cha biashara, huduma au kampuni ambayo aliyefariki aliwekeza maisha yake
> yote
> kuendeleza; imekua ni mwanzo wa hali ya maisha ya familia kubadilika; Imekua
> ni
> mwanzo wa watoto na mke/mume kuachwa kwenye mateso na masumbufu mengi;
> imekua ni
> mwanzo wa kesi zisizoisha za kugombea mali; Imekua ni mwanzo wa magomvi
> yasiyo
> na kikomo; na mengine mengi. Haya yote yanatokea kwa sababu ya ubinafsi
> wetu
> unaotusukuma kujiwazia mema sisi wenyewe na kufanya bidii kubwa kuziandaa
> roho
> zetu bila kujua kuwa jukumu letu haliishii hapo.
>>>Huenda mawazo yangu haya hayakua
> sahihi kunisumbua kipindi hiki, lakini namna kifo cha Mwalimu wangu Dr.
> Hashim
> Twakyondo kilivyotokea, kinanilazimisha kutokuwaza haya. Pamoja na ugumu wa
> kukubali kuondoka kwake, kifo chake kinaniambia kuwa kuna haja ya kujiandaa
> maana ulimwengu huu sio wetu na hatuna mkataba wa kukaa kwa kipindi fulani
> au
> milele. Hivyo basi pamoja na mipango mizuri tuliyonayo tunalazimika kuwaza
> yatakayoendelea iwapo kuondoka kwetu kutakuja bila taarifa kwetu sisi
> wenyewe
> au kwa wale tutakaowaacha. Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, "twalazimika
> kufanya
> kazi kama vile tutaishi milele na kuishi kwa tahadhari kama vile tunakufa
> kesho".
>>>Kwa heri Mwalimu wangu Dr. Hashim
> Msafiri Twakyondo. Tanzania imejaa wataalamu wengi wa fani ya Sayansi ya
> Kompyuta ambao kwa namna moja au nyingine walikuswa na utumishi wako katika
> Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.
>>>MM
>>>
>>> --
>>>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>>
>>>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>>> ukishatuma
>>>
>>>Disclaimer:
>>>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>>> be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and
>>> Guidelines.
>>>---
>>>You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>>> "Wanabidii" group.
>>>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>>>For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>>
>>
> --
>>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>>Disclaimer:
>>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>---
>>You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>>For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment