Friday 25 October 2013

Re: [wanabidii] KUREJESHA MABILIONI AU BLA BLA ZA SIASA

Well done ndugu Mutabaazi Lugaziya


2013/10/25 mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>

Kwa Mh. ZZK,

 

Habari za Uswisi, natumai umeamka salama.

 

Naomba utusaidie,

 

Nimekusikia kwa muda mrefu ukizungumzia kurejeshwa kwa fedha zilizo Uswisi na kwingineko, kunakoitwa kwenye "Safe Havens". Lakini msingi wa "jihad"hii ni taarifa zilizotolewa na Benki ya Taifa ya Uswisi kuhusu kuwepo kwa hela zenye utata zilizoingizwa kwa watu ambao walitajwa. Hawakuwa wengi.

 

Madhumuni ya ulizo hili ni hili:

 

Nchi ya Uswisi ni nchi iliyokubaliwa na "League of Nations"UN ya wakati huo, kuwa iwe nchi "neutral"ambayo itatumika kumaliza migogoro yoyote, endapo mahali pengine popote duniani jambo hilo halitawezekana. Na nchi hizo zikakubaliana kwamba atakayeichokoza Uswisi atakuwa amechokoza dunia. Kwa msingi huo, ndio maana nchi ya Uswisi haina jeshi, lakini haiguswi. Na ndio maana hao wanaotubia wakapata nafasi ya kupeleka hela zetu kuzificha huko. Ukijumlisha na "usiri"wa hifadhi za amana kati ya mabenki na wateja wao, Uswisi ikawa ndio mahali ambako wezi hawa wanadhani hela yao haitaguswa.

 

Kwa taratibu hizo za kibenki, benki yaUswiwi haiwezi kutoa taarifa za wahifadhi halali. Kinachofanyika, kama mimi MJL ni Waziri, Rais, Mkurugenzi ambaye kikawaida sina akaunti wala hela yoyote kule, halafu ghafla bin vuu inafunguliwa akaunti, muda mwingine bila mimi kuwepo, inatumbukizwa fedha dolari milioni kadhaa, hawa ndio huripotiwa, na kuzitaka nchi husika kufanya uchunguzi katika muda ambao unakuwa umewekwa(kikawaida haizidi miezi 6.) Katika muda huo, akaunti hizo huwa zimefungwa kusubiri uchunguzi.

 

Nchi husika hutakiwa kumteua mtu atakayeshirikiana na mamlaka za Uswisi ili kufanya uchunguzi wa pamoja. Muda huo ukiisha, kama nchi kwa dhati inafuatilia fedha hizo, na kawa haijakamilisha uchunguzi, huomba kuongezewa muda.

 

Kwa hiyo, taarifa zilizotolewa na benki ya Uswisi, zilitaja akaunti na majina. Hii ya kuongelea akaunti za watu wanaodunduliza kidogo kidogo, sio taarifa iliyoletwa na serikali ya Uswisi. Watu waliotajwa wanajulikana na mamlaka husika kwa majina na akaunti zao na hela walizoingiziwa na makampuni ya mafuta na gesi. Watu hawa wanaitwa "Politically Exposed Persons"- yaani watu walio karibu na watawala.

 

Sasa naomba kujua, na bila shaka na wengine wanapenda kujua pia.

 

Je unadhani serikali "seriously" inashughulikia suala hili kwa dhati, iwapo imeshindwa kuishughulikia Kagoda tuliyoambiwa na iko hapa hapa nchini, sembuse hao ambao hatujaambiwa?

 

Je hii orodha katika harakati zako umeiona?

 

Je hao ndio unaowafuatilia?

 

Na kwa utaratibu niliousema, kwa vile muda umepita mwingi, je bado mamlaka za Uswisi zimehodhi hizo akaunti? Kwa maombi ya nani?

 

Je umeulizia uwezekano wa kutumia njia mbadala (zilizopo) yaani kutumia asasi za kiraia kuomba wananchi wasaidiwe kuwabana wanaowaibia?

 

Au na wewe katika kutucheza "shere?"

 

Nitaandika makala ya kisomi kuhusu namna ya kushughulika na wezi hawa muda si mrefu. Lakini Mheshimiwa "in-between tusaidie kwa haya!

 

MJL

 

Cc. Dr. H.Kigwa-mnapoibana serikali Bunge lijalo, muibane mkijua utaratibu unaotumika kufuatilia fedha hizo.

 

 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment