Thursday 3 October 2013

Re: [wanabidii] KILIO CHA AJIRA NCHINI SASA NEXT LEVEL

Anayemtaka std 7 (TAKUKURU) ni kwamba ajira/kazi yenyewe inamtaka mtu ambaye haitaji kuwa na uzoefu wa kazi wa muda mrefu. Inawezekana ni ya kufakia, kupika-kuosha vyombo, kupanga mafaili ofisini etc. Ambapo TANAPA inategemea labda wanamtaka mtu mwenye uzoefu wa aina fulani-community development, au mafunzo ya vijana wa village scouts (sijaona hilo tangazo).
Wenzetu wazungu hujitolea kikazi. Utakuta anasomea degree lakini ni volunteer maktaba anapewa kaposho kidogo au volunteer anakwenda jela kutoa ushauri nasaha kwa wafungwa au kuwafundisha kusoma na kuandika au ujuzi wa kuchora. Mwingine anajitolea nursing homes au shule ya watoto wadogo. Wengine hujiunga na volunteer system wakaja makwetu. Akitoka huku kwetu unamsikia kaajiriwa na ILO, USAID, ubalozi wao au international agency yao. Nawe ulimwona alikuwa volunteer TZ sasa yupo ubalozi katka shughuli fulani kama officer.

Tayari ana ujuzi na kapata ajira.Hapa petu bongoland kujitolea si dhima ndani ya damu yetu. Hata unapounda vikundi vya vijana kuwahamasisha wajitolee ili wajitegemee na kuwasaidia kuandikishwa kuwa CBO/NGo rasmi-inapokuja wao kutayarisha shamba lao, walime nyanya, ufuta etc-tatizo. wanataka mpaka kuchimbua visiki waajiri mtu wa kuvichimbua, kubeba mbolea na kumwagia shamba. Wakija vikao wapate posho. Mradi wa kuku kulisha kuku kwa zamu ni tabu. Kuku mmoja wa kienyeji ni elfu kumi hadi zaidi ya hapo lakini tatizo na elimu ya kupata ajira na uzoefu hawana. Wachache wakilipiwa mafunzo ya ujasiriamali au kulipiwa wasome Veta kisha waendeleze kikundi-
tatizo-hawarudi wanatafuta ajira ambapo ndio kikundi kingeboreka. Unakuta raslimali zipo, vifaa vya kulimia (hata power tiller walinunuliwa), mafunzo ya kuendesha vikundi na ujasiriamali walipewa lakini kuendelea ni tatizo. Inakuwa bora mtu ajifanyie pekepeke na kama akifuga au kulima nyanya awe anasafirisha-wenzake watakuja kumuibia. Inafika asubuhi shamba lote limevunwa usiki au mifugo imeibiwa. Vurugu ktk ushirika kutokana na muono finyu na kutokuwa na malengo na kutaka rahisi rahisi hata kama maisha ni magumu, unaona wenzako wanavyochakarika, unaona wanavyoendesha maisha baadhi kwa mafanikio lakini bado wewe unataka vishuke kama mvua.


Kutaka ujuzi-kutatufanya tuone kwamba kusoma tu sio tija na ujuzi na ukipelekwa field practice na chuo chako-hutozembea kujifunza kimatendo kiukweli sio kuishia kukaa ofisini tu. Field practice kama ni kujenga visima-uchezee tope hasa ujenge; kama ni wanyama pori uwafuatilie porini na askari uweze kuonyesha hiyo practical training labda itasaidia kama hukuajiriwa huko nyuma. Hata daktari-kujifunza kutibu magonjwa bila ya kujua jinsi sindano inavyochomwa inakuwa tabu. Ataajiriwa na kuwa anasaidiwa na nurse aliyobobea kazi hapo alianza kama cleaner, akawa nurse attendant sasa nurse midwife anamfundisha kazi medical doctor mwenye degree asiye na uzoefu. Mama anajikamua mtoto yeye anaogopa anatimua mbio; kuchoma sindano ya namna fulani hakieleweki maana kasoma nadharia tu. Na pia housegirl sio mzoefu-atawafanya muugue maradhi daima kwa kuosha sahani za kulia ktk maji aliyofulia nepi za kinyesi cha watoto au aliyotumia kusuuzia tambara la kudekia vyombo!!
Uzoefu muhimu pia ktk ajira.

Elimu ni muhimu sana ila haitoshelezi. Elimu ya kuendesha gari ni tofauti na kuendesha gari la trela na kupanda mlima au kuligeuza ktk mtelemko wewe uliyetoka darasani Veta ktk elimu ya kuendesha magari.
--------------------------------------------
On Thu, 3/10/13, Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] KILIO CHA AJIRA NCHINI SASA NEXT LEVEL
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 3 October, 2013, 13:41

Mzuri

Kila kazi inahitaji mahitaji yake hata huko ulimwenguni siyo
kila kazi inamfaa mtu ambaye hana uzoefu. ILO wenyewe wakitangaza kazi
huwa tunaona wanachotaka.


2013/10/2 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
>
> TANAPA LEO HII INATANGAZA KAZI, KWANZA WANAHITAJI WATU
WENYE UWEZO MKUBWA WA ELIMU (MASTERS), HAIJAISHIA HAPO
WANAHITAJI MTU HUYO ANAYEOMBA KAZI AWE NA UJUZI NA UZOEFU WA
MIAKA ISIYOPUNGUA SABA (7) AKIWA KAZINI KWENYE FANI HIYO NA
PIA AWE ALIKUWA KIONGOZI WA ENEO ALILOTOKA.
>
> HII NI TAASISI KUBWA YA SEREKALI NA ILIPASWA KUWA NDIYO
KIMBILIO LA AJIRA KWA VIJANA WA KITANZANIA WALIOTOKA
VYUONI.
>
> WAKATI HUO HUO TAKUKURU (PCCB) NAO WAMETANGAZA AJIRA
WANAHITAJI VYETI VYA DARASA LA SABA NA HAWAHITAJI
PROGRESSIVE REPORTS AU TRANSCRIPT PEKEE, BALI VITU HIVYO
VIAMBATANE NA VYETI, HAPO WAMEWAWEKA WAPI WANACHUO MAELF KWA
MAELFU WALIO GRADUATE MWAKA HUU.
>
> ANYWAYS, WADAU MNALIONAJE HILI KWA KUTUMIA PERSPECTIVE
YA WANAVYUO??
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility for any legal consequences of his or her
postings, and hence statements and facts must be presented
responsibly. Your continued membership signifies that you
agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to
the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving
emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.




--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment