Tuesday 18 June 2013

[wanabidii] UCHOCHEZI VS UHALISIA

SABABU ZA KUPIGWA MAWE AU KUHARIBIWA MALI WANAHABARI WA VYOMBO VYA HABARI VYA CHAMA NA SERIKALI HIZI HAPA:
 
Katika vurugu zilizotokea hivi karibuni huko Mtwara, mmoja wa waathirika wa vurugu hizo alikuwa Mwandishi habari na ripota mkongwe wa TBC1, Kassim Mikongoro. Mwanahabari huyu alinusurika kupopolewa mawe na wananchi wenye hasira lakini raia walifanikiwa kuiteketeza kabisa nyumba yake kwa moto!
 
Sababu zilizopelekea nyumba ya nguli huyu wa habari kuchomwa moto ni tuhuma kwamba alikuwa akiripoti kwa kupotosha habari zinazohusu mgogoro wa gesi kati ya serikali na wananchi, kwa kuegemea zaidi upande wa serikali na kuwakandamiza wananchi. Hakuna ubishi kwamba mara nyingi wanahabari wanaoripotia vyombo vya chama na serikali wanaipendelea sana serikali kwa kutia chumvi au kupotosha habari kwa lengo la kumfurahisha mwajiri (serikali na chama).
 
Matokeo ya kupotosha au kutia chumvi habari, ni kujenga chuki kati ya mwandishi na wananchi. Na wananchi wakishagundua kwamba mwanahabari fulani sio mwenzao, watachukua hatua yoyote watakayoona inafaa dhidi ya huyo mwanahabari. Hii hali hupelekea mwanahabari kuishi kwa mashaka na wasiwasi, hasa ukizingatia kwamba wanahabari wanaishi miongoni mwa wananchi. Hawaishi ndani ya mageti makali pamoja na hao mabwana wanaowatumikia ili kupata ulinzi wa kutosha.
 
Ushahidi wa haya ninayosema ni hizi ripoti mbili tofauti zinazohusu story moja, ambapo moja imeripotiwa kwa uhalisia na nyingine imetiwa chumvi na kupotoshwa kwa makusudi. Tangu bomu lilipuliwe juzi kila mtu anafahamu ni nini kilichotokea. Sasa iweje habari zipotoshwe wakati ukweli umeishajulikana tangu juzi (ijapokuwa mtuhumiwa bado hajakamatwa)? Tafakari!
 
 
HABARI YA KWELI – Mwananchi (17/06/2013) – Gazeti Huru
 
 
HABARI YA UCHOCHEZI – Habari Leo (18/06/2013) – Gazeti la Chama na Serikali
 

0 comments:

Post a Comment