Wednesday 12 June 2013

[wanabidii] Salamu za Rais Kikwete kwa msiba wa Timothy Apiyo, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Mzee Timothy Apiyo kilichotokea usiku wa jana, Jumatatu, Juni 10, 2013, katika Hospitali ya Millpark, Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Kikwete amesema kuwa kifo cha Mzee Apiyo kimeinyang'anya taifa la Tanzania mmoja wa watumishi wa umma hodari na wazalendo waliotumikia umma wa Watanzania kwa uaminifu na uadilifu.

Katika salamu zake kwa Balozi Ombeni Y. Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Rais Kikwete amesema: "Nimepokea 
kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Mzee Timothy Apiyo ambacho nimejulishwa kilitokea usiku wa jana katika Hospitali ya Millpark, Afrika Kusini."

"Kwa hakika kifo cha Mzee Apiyo kimelinyang'anya taifa letu mmoja wa watumishi wa umma hodari, wazalendo ambao walitumikia umma wa Tanzania kwa bidii, uaminifu na uadilifu mkubwa,"amesema Rais Kikwete na kuongeza:

"Katika nafasi zote ambazo alizishikilia katika utumishi wa umma ukiwamo Ukatibu Mkuu na Ukatibu Mkuu Kiongozi, Mzee Apiyo alionyesha umakini wa kiwango cha juu ulioongozwa na ushikiliaji wa kuigwa wa misingi ya utumishi wa umma."

Amesisitiza Rais Kikwete: "Kwa hakika, Mzee Apiyo ataendelea kuenziwa kama mfano wa kuigwa wa utumishi uliotukuka wa umma."

"Kutokana na kifo hiki, nakutumia wewe Katibu Mkuu Kiongozi salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa familia nzima ya Mzee Apiyo ambao wameondokewa na Baba, Babu na Mhimili wa familia. Napenda kukujulisha kuwa niko nawe na familia nzima ya Mzee Apiyo katika kuomboleza msiba huo. Naelewa machungu yenu katika kipindi hiki kigumu. Nawaombea huruma ya Mwenyezi Mungu muwe na subira ya kuweza kuwavusha kipindi hiki. Aidha, naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweka peponi roho ya Marehemu Timothy Apiyo. Amen."

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

11 Juni, 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment