Sunday 16 June 2013

[wanabidii] Olle Mjengwa anavyoichambua mechi ya Taifa Stars Vs Ivory Coast ….!



Ni dhahiri Ivory Coast ni timu bora Afrika kwa sasa. Wakati huo huo ni ya 13 kwenye ranki za FIFA.

Karibu wachezaji wote kwenye kikosi cha Ivory Coast wanacheza kwenye vilabu vikubwa barani Ulaya.

Wanavyocheza Ivory Coast…

Kwa kawaida Ivory Coast huwa wanacheza fomesheni ya 4- 2- 3 -1, lakini pia wana uwezo wa kubadilisha fomesheni yao kuwa 4-4-2 kutegemeana na kikosi cha siku hiyo.

Ivory Coast wana wachezaji wengi wenye kujituma uwanjani, kama vile Yahya Toure na Lacina Traore. Na kwa vile wana wachezaji wengi wenye uwezo wa kukaba vizuri kama Gosso Gosso na Zakora, timu ya upinzani hupata shida sana kuishika mipira. Pia kwa kuwa Ivory Coast wana wachezaji wenye uzoefu wa kupiga pasi nyingi, inawasaidia kumiliki mpira kwa muda mwingi wa mchezo.

Na kwa vile wana wachezaji wenye kasi sana kama vile Kalou, na kama tulivyoona leo, Ivory Coast walikuwa wakianzisha mashambulizi ya haraka kila walipoupata mpira kwenye nusu ya lango lao. Ikumbukwe kwamba, Ivory Coast leo hawakucheza na kikosi chao bora chenye majina kama Cheik Tiote, Eboue na Gervinho.

Pamoja na kufungwa na kufungashwa virago kuondolewa kwenye safari ya kwenda Brazil, Taifa Stars wamejitahidi sana. Ni kwa vile , kama nilivyosema hapo juu, kuwa Stars wamecheza na timu nambari moja barani Afrika kwa sasa kwa mujibu wa ranki za Fifa. Na nyuma ya Ivory Coast kwenye ranki za Fifa kuna mataifa makubwa katika soka, kwa mfano, Mexico ya 17, Ufaransa ya 18 na Uruguay ya 19 , na huku Brazil ikiwa ya 22. Hivyo, Ivory Coast kwa sasa ina uwezo wa kuzifunga timu nyingi za Ulaya na Marekani ya Kusini.

Kwa Taifa Stars kupachika magoli mawili dhidi ya Ivory Coast kwa jioni moja ichukuliwe kama ni mafanikio makubwa.

Jioni Njema…

Olle Bergdahl Mjengwa,
Iringa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment