Saturday 8 June 2013

[wanabidii] MATATIZO YA WAKAZI WA WAZO HILL NA KAMPUNI YA SARUJI TPCC (WAZO HILL TEGETA)

MUHTASAI WA MTATIZO YA KAZI A AZO HILL NA KAMPUNI Y SARUJI TPCC (WAZO ILL TEGETA)

 

TAREHE: 01-03-2013

MHE: RAIS JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE.

 

Mhe. Raisi,

Huu ni muhitasari wa matatizo wanayopata wakazi wa Wazo Hill kutokana na mgogoro kati yao na kiwanda cha Saruji Wazo Hill (TPCC). Wakazi hawa wako katika maeneo matatu tofauti.

1.    Wakazi wa eneo la Msikitini

2.    Wakazi wanaoishi kwenye nyumba zilizokua za Saruji Corporation

3.    Wakazi wa Chasimba.

Wakati kiwanda cha Saruji Wazo Hill kilipobinafsishwa kutoka shirika la umma, Saruji Corporation kwenda kwa mwekezaji  Tanzania Portland Cement Company (TPCC), mwekezaji alinunua sehemu tu ya kiwanda na maeneo mengine yalibakia chini ya umiliki wa Saruji Corporation. TPCC walinunua kiwanda eneo la uzalishaji na maeneo yaliokua na malighafi tu kama ilivyoainishwa kwenye Memorandum of Understanding (Kiambatanishi N. 12APPENDIX A na barua kutoka kwa Meneja mkuu wa Shirika la Saruji  Tanzania yenye Kumb. TSC-A/A/02 ya tarehe 07/05/2002). Shirika la Saruji Tanzania waliendelea na mpango wa kuyaendeleza maeneo yaliyobaki kwa kushirikiana na wananchi mpaka lilipovujwa rasmi na baadhi ya shughuli zake kukabidhiwa PSRC.

WAKAZI WA ENEO LA MSIKITINI

Mhe. Raisi,

Baada ya Shirika la Saruji Tanzania Kuvunjwa, TPCC wameanza njama za kutaka kupora maeneo ambayo hyakuwa kwenye mkataba wa ununuzi wa mwanzoni likiwemo eneo hili la msikitini. Matatizo ya eneo hili yalikua anashughulikiwa na uongozi wa mtaa wa wazo na kata na Meneja Mkuu wa Shirika la Saruji Tanzania kuanzia mwaka 1992 kama inavyoonyeshwa kwenye kiambatanisho namba moja hadi namba 11.

No. 1           Muhutasari wa mkutano wa wananchi wa eneo la msikitini na uongozi wa kiwanda, Katibu Kata na Katibu Tarafa. katika mkutano huo wananchi walikubaliana na uongozi wa kiwanda mbele ya Katibu Kata, katibu tarafa na mwenyekiti wa kijiji cha Wazo walipwe fidia ya  mali zao na nyumba na wapewe viwanja eneo la Block F ndio wahame kwenye eneo.

No. 2           Orodha ya wananchi wa Wazo waliolipa fidia na kiwanda cha saruji kutokana na makubaliano ya mkutano wa tarehe 12.2.1992. Wananchi hawakupewa viwaja vya Block F kama ilivyokubaliwa.

No. 3           Barua ya kamishina wa Ardhi kwa uongozi wa kiwanda kutowahamisha wakazi hao mpaka wapatiwe viwanja Block F.

No. 4           Barua ya katibu Tarafa kumwonya asibomolee wakazi mpaka wapewe viwanja Block F.

Baada ya Ubinfsishaji:

Kiwanda kilipobinafsishwa, mnunuzi alichukua kiwanda na maeneo ya malighafi tu kama ilivyoelezwa hapo awali. Wananchi walifanya mkutano na uongozi wa Shirika la Saruji Tanzania wakiomba wapewe maeneo hayo kwa makazi na shughuli za kijamii.

No. 5           Muhutasari wa kikao cha kamati ya wakazi wa msikitini na serikali ya mtaa na Meneja  Mkuu wa Saruji Corporation.

No. 6           Barua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kumb. D/MTP/MGE/1/50 ya tarehe 2.5.2002 kuomba  rasmi maeneo hayo ka ajili ya kupima viwanja vya huduma za jamii.

No. 7           Barua ya mkurugenzi wa saruji Corporation kukubali ombi la manispaa kupima viwanja vya matumizi ya jamii Kumb. TSC.A/A/02 ya tarehe 7/5/2002

No. 8           Barua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kwa Meneja Mkuu wa kiwanda cha Saruji TPCC kumtaka arejeshe hati miliki No. 42336 kwa Mkurugenzi wa Ardhi ili igawanywe.

No. 9           Mkurugenzi wa Saruji Corporation anamfahamisha Mkurugenzi wa Manispaa kwa hati ipo TPCC.

No. 11         Kiwanda cha Saruji Wazo (TPCC) kwa kupitia mwanasheria wao wanarejesha hati miliki namba 42336 kwa kamishina wa Ardhi.

Kwa vielelezo hivi ni nadhihirisha kwamba kiwanda cha Saruji Wazo (TPCC) sio wamiliki wa eneo la msikitini  baada ya ubinafsishaji wa kiwanda. Eneo hilo ni mali ya Serikali.

WAKAZI WA NYUMBA ZILIZOKUA ZA SHIRIKA LA SARUJI TANZANIA.

Kama ilivyoelezwa awali kampuni iliyonunua kiwanda cha Saruji Wazo (PTCC) ilichukua kiwanda na eneo la malighafi tu. Nyumba za saruji Estate zilibakia chini ya milki ya Shirika la Saruji Tanzania. Aidha wafanyakazi wa Kiwana cha Saruji  Wazo (TPCC) walitakiwa kulipa kodi ya pango kwa Saruji Corporation hivyo baadhi waliamua kuhama kwenye nyumba hizo na Saruji Corporation waliamua kupangishia nyumba zilizoachwa wazi kwa raia ambao sio wafanyakazi wa Kiwanda.

Baada ya shirika la Saruji Corporation kuvunjwa nyumba hizo zilihamishiwa PSRC kwa utaratibu wa kuuziwa wananchi na wapangaji walio kuwepo waliendelea kutambuliwa na mawasiliano yaliendelea vizuri kama viambatanishi vilivyopo hapa vinavyoonyesha.

Matatizo yalianza mwaka 2009 wakati kiwanda cha Saruji Wazo (TPCC) walipotoa notisi ya kuwafukuza wakazi hao ndani ya nyumba hizo wakati wakijua wao sio wamiliki.

Mhe. Raisi,

·         Mwaka 2009 mwezi Novemba Kampuni ya Saruji Wazo Hill ilituandikia Notice ya kutoka kwenye nyumba hizi kwa kisingizio kuwa wao ndio wenye hati miliki.

 

·         Mwaka 2010 mwezi Januari Kampuni ya Saruji Wazo (TPCC Ltd) ikatuandikia barua nyingine ya kutulazimisha kuingia nae mkataba/ kuishi kwenye hizi nyumba  jambo ambalo hatukufanya.

 

 

·         Mwaka 2010 mwezi wa Nne kampuni ya Saruji ikatuma Kampuni ya Majembe kuja kututoa ndani bila hata kibali cha Mahakama, lakini zoezi hilo lilishindikana baada ya RPC Kinondoni  kuingilia kati.

 

·         Mwezi wan ne mwaka 2010 wapangaji wakaamua kufungua kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.

 

SABABU ZA MSINGI ZA WAPANGAJI KUTOKUKUBALIANA NA AMRI ZA KAMPUNI YA SARUJI.

1.    Kampuni ya Saruji Wazo Hill (TPCC Ltd) ni mpangaji wa nyumba zilizokuwa Shirika la Saruji Tanzania ambaye ana nyumba namba1, na 3.

 

2.    Kampuni ya TPCC mwaka 2001 ilizirudisha nyumba nyingine kwa Shirika la Saruji Tanzania na kuagiza wafanyakazi wake waingie mkataba binafsi na Shirika la Saruji Tanzania.

 

 

3.    Sisi wapangaji tunayo mikataba halali na yakisheria na lililokuwa shirika la Saruji Tanzania.

 

4.    Memorandum of Understanding kati ya Serikali na Mwekezaji haikuzijumuisha nyumba hizi ndani ya mkataba (zilibaki kuwa mali ya serikali.)

 

 

5.    Kupitia gazeti la Serikali nyumba hizi zilirudishwa kwa wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) instrument ya Transfer.

 

6.    Wakala wa Majengo ya Serikali alituma Maofisa wake, wakishirikiana na wale wa Kampuni kuhakiki wapangaji, na kuthamini majengo pamoja na kujaza fomu maalumu na picha za wapangaji wote kupelekwa TBA.

 

 

7.    Baraza la Mawaziri lilishaagiza Kampuni ya Saruji (TPCC Ltd) na mamlaka husika kutenganisha hati miliki ya Kiwanda na ilie ya Makazi.

 

8.    Zoezi la kutenganishwa hati hizo lingekamilika nyumba hizi zilitakiwa kuuzwa kwa utaratibu wa kiserikali baada ya uuzaje wa zabuni ya wazi kushindikana mara mbili mwaka 2005.

Mhe. Rais, ni sababu hizi za msingi zilizofanya wapangaji kukimbilia  mahakamani kumzuia Kampuni kutuondoa ndani kwani Kisheria yeye sio mwenye nyumba  wetu, ila yeye anakaidi amri halali za serikali na anataka kupora mali ya Serikali

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment