Sunday 16 June 2013

[wanabidii] Maandalizi Ya Kwenda Kombe La Dunia Urusi Na Qatar Yaanze Usiku Huu...!


Ndugu zangu,

Leo jioni baada ya kufungwa 4-2 na Ivory Coast, basi, mpira ulivyoisha tu,  ukweli nilikwenda kulala kwa saa nzima.

Nimeamka na mawazo mapya juu ya namna ya kwenda mbele. Kwenye jukwaa hili nimeshiriki majadiliano kwa kujenga hoja hii;

Zitto,

Nakubaliana nawe; kuwekeza kwenye mpira. Usiku wa leo na tuyaanze maandalizi ya safari ya Urusi 2018 na Qatar 2022.
Napendekeza, kuwa hata humu mtandaoni tuanzishe kitakachoitwa ' Bongo Football Flava  2013- 2022' , ama kwa kifupi ' BFF- 2013- 2022'
Madhumuni?

1. Ni kuhakikisha tunafanya mageuzi ya kimsingi ya soka kwenye nchi yetu kuanzia soka la watoto, vijana na wakubwa. Kwa wanaume na wanawake.
2. Kuhakikisha mpira unatangulia kwanza na siasa inafuata nyuma. Hivyo basi, ' Mpira Kwanza, Siasa Baadae'
3. Kuboresha viwango vya  Ligi zetu za nyumbani na hivyo, kuboresha viwango vya  timu zetu za taifa.
Malengo?
1. Kuhakikisha kutoka sasa hadi mwaka 2022 nchi yetu iwe imefanikiwa sio tu kushiriki, bali kutwaa mataji kwenye mashindano ya kimataifa kwa ngazi za vilabu na timu za Taifa kama vile Cecafa, Afcon na mengineyo. Mashindano ya  vijana, wakubwa, kwa wanawake na wanaume.

Mbinu?

1.Kuwajengea uwezo makocha wa ndani kwa ngazi zote kupitia mafunzo ya ndani na nje ya nchi.
2. Kuwajengea uwezo waamuzi wa mchezo wa soka kwa ngazi zote.
3. Kujenga vikosi imara vya timu za vijana U 17, U 21 na U 23
4. Kuanzisha kiwanda cha kutengeza mipira na Serikali kupitia Wizara husika itoe mipira bure mashuleni na kwa vilabu vya watoto na vijana chini ya miaka 23.
5. Kujenga viwanja vingi vya mazoezi na vya mashindano vyenye ubora.

... Mawazo zaidi yanakaribishwa...
Maggid,
Iringa.
0754 678 252

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment