Wednesday 12 June 2013

[wanabidii] Kauli ya CCM kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa;

Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la 
katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani, utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment