Wednesday 12 June 2013

[wanabidii] Katiba Mpya!

Naililia nchi yangu Tanzania. Sijaishi upande wa visiwani nikajua fika matatizo waliyonayo wenzetu hawa kuhusiana na mfumo wa utawala tulio nao. Ninachojua Zanzibar siyo koloni la Tanganyika. Natafakari, naona kama kuna kosa vile lilifanyika. Kama Tanganyika ilifutwa kutoa nafasi kwa nchi ya muungano inayoitwa Tanzania, kwanini pia tusifikilie kuondokana kabisa na hizi serikali ndani ya serikali!! Hivi Muungano huu ni wa nani? Kama si wa wachache, kwanini tusitangaze tu uwepo wa serikali moja ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania yenye kuongozwa na serikali moja na si mbili wala tatu!!. Tupeni basi nafasi tupige kura kama kusikilizana kwa kawaida imeshindikana. Hapo tutapata maoni sahihi ya kila upande. Hivi Tume ya Katiba kwanini wanapata kigugumizi kutoa pendekezo hili kama kweli muungano huu tunaupenda sote? SITAKI kufikia mahali kulazimika kuomba uraia wa Tanganyika au Zanzibari kama tokeo la shinikizo la mabadiliko toka kwa watu wachache wenye uchu wa madaraka!! Najaribu kutafakari!!! 

0 comments:

Post a Comment