Tuesday 11 June 2013

Re: [wanabidii] TGNP Yaweka Bayana Matokeo Utafiti Vijiji vya Shinyanga, Mbeya na Morogoro


Muhimu pia kwa Gender NGO National Coordinator kama TGNP kuunda a National Volunteer System. Hii mimi ninaidai sana. ili tujikwamue na mengi yanayowezekana kutupeleka pabaya. inawezekana kabisa wanakijiji au kitongoji kugharimia kisima chao wakauza maji. Sehemu nyingine water table ni high, maji yapo ila ni kujajengea na kuyahifadhi badala ya kuyachafua tutegemee GVT ije iyahifadhi ili tusiyachafue.

Kuna vijana wengi wasomi ambao hawana ajira; kuna wastaafu wenye academic na practical field experience ambao wana nguvua za kufanyakazi. TGNP ina watumishi mbalimbali na foreign volunteers na inaweza ikawapata foreign volunteers wenye ujuzi mbali mbali. Hawa na local volunteers (salaried) wakafanyakazi na CBO/NGOs za maendeleo vijijini na extension staff wa Kata, wilaya katika kuhamasisha maendeleo ki-sector.

Shinyanga ikiwa ya-kwanza Tanzania na Morogoro Region kuwa na visima vya maji vya handpump chini wa wadachi (DHV). Dodoma na kuwa na visima ya windmill kupampu maji. Maeneo haya Shinyanga (Shy) na Morogoro yalikuwa ya kwanza kutoa lesson learnt katika hand pump wells, hayawezi kuwa na tatizo la maji sana kama operation na maintenace ingekuwa imeboreshwa, replacement ya gandpumps na kuongeza visima.
Hizo 'white elephants' za pampu zinaweza zikafufuliwa na kuwekwa pampu mpya. Zipo zinaonekana Morogoro vijijini ambako DHV wamefanyakazi na kiwanda cha pampu na spare za pampu kuanzishwa Morogoro mjini (The International Clean Water and Sanitation Decade 1980-1991) na mafundi baiskeli vijijini kufundishwa repair ya handpumps. Mradi wa maji (Kikwete ) shinyanga wa mamilioni uliong'olewa mambomba ukitoa maji lake Victoria kilometa mamia kwenda Shy.

Mradi wa maji wa Bulenya Mwamapuli (kunywa na kumwagilia) mashamba (nakumbuka Norad funded na Norconsult studies); miradi na misitu ya forest conservation ya kururisha uoto asili na uhifadhi misitu ile asili inayoitwa 'Ngitiri' (Norad funded project). Yote hii documented ni juhudi za GVT na donors zilizofanyika shy ktk land conservation. Mama akitembea siku nzima na mkokoteni kubeba mapipa ya maji kutumia punda. punda anachoka mnakuta punda kalipindia limkokoteni la mapipa ya maji, kagoma kwenda kakaa anakula majani. kazi ya kutwa nzima imeharibika mama amekaa chini analia. ILO walisaidia masuala ya mikokoteni (animal traction/power) kusaidia kupunguza mzigo wa mama kkt kubeba maji (Tanga, Shy, Makete) ni maeneo ya mradi huu wa awali wa kupunguza mzigo mama kwa kutumia mkokoteni wa kuvutwa na ng'ombe. Huko shy ndio unakuta handpump imetolewa nati zimefungiwa mkokoteni au zimetiwa ktk kirungu cha kubondana vichwa.

Wanapotafuta madini ya dhahabu na mengineyo (Shy, Mara, Mwanza) huchimba mpaka kwenye handpumps. Tunakuwa hatuna recall wakati mwingine na kufanya miradi ambayo tunarudia makosa yaleyale bila ya kuwa na sustainability. maji sasa ni economic good, no free water. Water user Associations zinaundwa kulinda miradi yao, kuuza maji, kuongeza vizimba au kuchimbisha visima zaidi angalau kaya itemee mita 400 kufikia kituo/kizimba, kisima protected au handpump well. Tulinde au tuharibu, tuchafue tupate tabu zaidi. na huu uchimbaji madini ulioingia ndio unaharibu mizitu na vyanzo vya maji. Penye kinyesi cha mifugo wafugaji wakitumie-Shamba darasa ifanye kazi yake vizuri. Mikoa kama Arusha ina visima vya mkoloni ktk estate farms za zamani. Hizi boreholes ni za kufufua.

Vijiji kama Naitolia Monduli-kimefufuliwa na serikali, kisha na mtu binafsi tajiri wa USA. wanakijiji wanakiendesha kwa kipato cha kuuza maji-kujiuzia wao na wageni na wanaweza kukarabati mpaka kwa milioni 4 kunapotokea uharibifu. Na ndio maana kunaonekana ktk TV wafugaji kutoka maeneo mengine kujazana naitolia Kata ya Mswakini kwenda kunyweshea hapo. Tembo kutoka Manyara na Tarangine hupita hapo ni njia yao toka pande moja kwenda nyingine na kuna tented camp na hunywa maji ktk cattle trough na kuharibu mashamba ila wananchi wamekataa WMA (tatizo na ni route ya wanyama toka mbuga moja kwenda ingine). Herla zinazotokana na water scheme hiyo ya kufufua borehole ya shamba la mkoloni Mr stein zinaleta mtafaruku kuanzia pale naitolia kuondolewa chini ya Kata ya Makuyuni kupelekwa Mswakini. Vurugu zote hizi ukizipekua ni MAJI na hela za MAJI (an economic good, hata maji ya Irrigation-yanalipiwa na kulipia irrigation water ni toka ukoloni ikaondolewa baadae). Hao wahamiaji na mifugo Naitolia-nao wanaweza kufufua boreholes ktk maeneo yao vijijini kwao wasibweteke kupenda rahisi. Mbona mzungu alichimba borehole nyingi huko kulikuwa bread basket ya kuzalisha mazao ya chakula na Wizara ya Maji-Idara Mkoa na wizara wanazijua kwa number zake na location ya GPS zilipo? Ni kila mfugaji kuuza au kutoa mbuzi au kondoo na mwingine kuchangia hela tu kisima kinasafishwa, kuwekwa solar pump kupata maji badala ya kutembea kutwa na kuacha mifugo ife kwa kukosa maji. Ni kutumia ubongo wetu vizuri na kujituma sio kusubiri vishuke.

Kubidiisha jamii badala ya lawana ili pia tuache kubakana kisha kula rushwa na kuua kesi zake wakati tumeshaumizana kisaikolojia na kupeana HIV na kuisambaza kuongeza umasikini ni jukumu letu. watu wanatumia mwanya wa maji, mwendo mrefu-kubaka. Kujitolea kumlea yatima kumbe nia ni kumbaka etc.tabia hizi chafu zinakua.

Huduma ya bure ya Maji na Afya zilipatikana zama hizo kutokana na kulipiwa huduma hizo na mashirika ya nchi za nje (donors) ambao nchi zao waannchi wakitoa kodi ambazo sisi tunalipiwa huduma huku bongoland. sasa hao Russians, Chinese, Denish, Swedish, Britisn, wa USA, Canada  hawatupi tena. WHO, UNICEF wanagharimia miradi michache kutuchangia-Neglected diseases (matende, trachoma etc) an huduma ya mama na mtoto lakini sio vyote bure. Hata school health wanayochangia mzazi anatakiwa asaidie kulima shamba la shule ili uji upatikane kwa school feeding program wapate kula ufaulu uongezeke. Serikali inawapa dawa ya minyoo kila mwaka (de-worming program). Morogoro na tuchakachue mito kutafuta madini, kutupa taka mitoni, kukata miti milima ya Morogoro ipo uchi, maji yatakosekana mitoni na ardhini. Ile sauti ya maji tota water falls hakuna tena Moro tunachakachua mazingira.

Na kama hatutoweka sera ya kilimo na ufugaji endelevu, kuondoa wafugaji wanaohamia Milimani, mitoni na maeneo chepechepe (wetland) kwa kulinda KURA zetu, tusipoangalia GVT na Mwananachi Mwenyewe anachangia vipi kuunda matatizo anayoyapata na kwenda grassroots kana NGOs za maendeleo na haki kuenenda nao kuelimisha na kuwaelekeza, kuwahimisha kufanya itakiwavyo-hatutokuwa tunasaidia kitu bali kuwa kama wanasiasa wa makelele tu. Ndio maana hata kule ambapo NGO za kisheria pamoja na juhudi za TGNP walikofundisha SHERIA ya ARDHI, kusaidia kuunda kamati husika na kuzipa mafunzo zikafanya vema, baada ya muda wa sasa tunawaona hao hao wananchi waliopata mafunzo wanapambana kugombea ardhi na kuchomeana nyumba, kukata mazao mashambani-mpambano. Kuzingatia maadili na yale mliyopanga wenyewe na mafunzo mliyopata-utata. Ubinafsi au umimi umetutawala. Tu vipofu sehemu kubwa hata kama tunamacho. re-inventing the wheel always hatujifunzi kutokana na yale ya nyuma na wepesi lawama. Tuiendelee kubaka watoto wetu. Musa umefika pia kwa zile NGo za sheria pamoja na TGNP waliofundisha sheria ya ardhi na haki ya mwanamke ktk ardhi
kufanya 'impact evaluation' ya mradi ule ili kuona effect yako au kukumtokea nini baada ya miaka kadhaa kupita baada ya mafunzo-watakuta vurugu balaa kama vile hakukufundishwa kitu!

Siku hizi rushwa ya ngono ipo mpaka kwa vijana sio wadada tu. Kazi za hotelini, viwandani, kuzoa taka nazo ziopo hivyo na uchafu. tatizo tu akina kaka hawajitokezi ila yamo tunayakuta.

Private sector ya wamiliki local ipo pia corrupt na uchafu, dhuruma mishahara midogo, haitolewi kwa wakati, visingizio ili akufukuze asikulipe mshahara; matibabu -nil ukipata ajali; protective gear hupati labda ujinunulie-uje nazo ndio akuajiri. Kampuni sub-contracted kuvuna miwa au kuleta mchanga katika ujenzi kwa malori; kufagia au kufanya usafi, upishi-Ndio dhuluma zaidi kuliko kampuni kuu ya mwekezaji. Uhonge-ndio miwa ikatwe na kubebwa au kahawa yako, pamba ipimwe upewe risiti ya malipo. Ni balaa ndani yetu wenyewe kuonyeana bila ya kumuangalia mgeni (China, European). na hawa wakija-tunawafundisha jinsi ya kutuibia ili wewe upate zaidi. nao wanafanya-ukiwa Roma fanya kama waroma walivyo. hata mita za umeme za kuiba umeme-tunawafundia.

Mimi inanikera nionapo mahala kuna kila kitu na tunauwezo wa kujibidiisha. Au, kulikuwepo na juhudi tumeharibu. Tunamifugo hata kuku kuuza kuchangia. Maana kuku mmoja jongoo kwa sasa ni elfu 10 plus unauza kuchangia ili upate maji ya kisima kilichoboreshwa usichote kutoka kibwawa kichafu. Mbuzi mmoja per kaya na tajiri wa mifugo mingi-ng'ombe mmoja- atanywesha miaka 10 plus maji ya borehole na kuchangia anyweshapo kwa ajili ya diesel na O&M. mama atatembea mwendo mfupi na watoto kusoma badala ya kusaka maji. nani haioni faida hii bali kuona mifugo 50% ikifa kwa kukosa maji ambapo angetoa ng'ombe mmoja tu sasa amekosa 50 wamekufa? tuna vichwa kweli?

--- On Tue, 11/6/13, misangocharles@yahoo.com <misangocharles@yahoo.com> wrote:

From: misangocharles@yahoo.com <misangocharles@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] TGNP Yaweka Bayana Matokeo Utafiti Vijiji vya Shinyanga, Mbeya na Morogoro
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, 11 June, 2013, 6:23

Jambo nadhan umeona makala yako leo
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 10 Jun 2013 07:49:11 +0300
To: Ahmad Michuzi<amichuzi@gmail.com>; <albertgsengo@yahoo.com>; Subi Nukta<subi@wavuti.com>; Sigfred Kimasa<kingkif07@gmail.com>; Emmanuel Shilatu<pbuyegu2@gmail.com>; Seria Tumainiel<seria.tw@gmail.com>; Jestina George<jestinageorge@googlemail.com>; Josephat Lukaza<josephat.lukaza@gmail.com>; <johnbukuku@gmail.com>; John Badi<badijohn30@yahoo.co.uk>; Othman Michuzi<othmanmichuzi@gmail.com>; <uwazi@hotmail.com>; Henry Mdimu<mdimuz@gmail.com>; Maggid Mjengwa<mjengwamaggid@gmail.com>; zainul mzige<zainul.mzige21@gmail.com>; Bashir Nkoromo<nkoromo@gmail.com>; Fredy Njeje<mbeyayetu@live.com>; <znzkwetu@gmail.com>; Francis Dande<dande15us@gmail.com>; Cathbert Kajuna<cathbert39@gmail.com>; francis godwin<francisgodwin2004@yahoo.com>; <father.kidevu@gmail.com>; wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] TGNP Yaweka Bayana Matokeo Utafiti Vijiji vya Shinyanga, Mbeya na Morogoro

TGNP Yaweka Bayana Matokeo Utafiti Vijiji vya Shinyanga, Mbeya na Morogoro

Na Thehabari.com

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP), umetoa mrejesho wa utafiti shirikishi uliofanywa na kikosi cha

waraghbishi kutoka mtandao huo katika baadhi ya vijiji kutoka mikoa ya Shinyanga, Mbeya na Morogoro-huku

matokeo yakionesha kuibuka kwa changamoto kadhaa katika maeneo yote ya utafiti.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuelezea matokeo ya utafiti, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu

Mallya alisema miongoni mwa masuala makuu yaliyojitokeza katika utafiti huo shirikishi na uraghbishi ni

pamoja na changamoto za uwekezaji na mgawanyo mbaya wa ardhi kwa wananchi hususan Kata ya Mshewe Mbeya

Vijijini.

Mallya alisema masuala mengine ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa huduma za maji safi na salama, Ukosefu

wa huduma bora za afya, uongozi mbovu na rushwa maeneo mbalimbali, pamoja na unyanyasaji wa wanawake na

wasichana karibu maeneo yote yaliofanyiwa utafiti.

Akifafanua zaidi alisema utafiti ulibani kuchukuliwa kwa maeneo ya ardhi yenye rutuba Kijiji cha Mshewe

mkoani Mbeya hali inayosababisha wananchi kukosa ardhi ya kutosha kwa kilimo na makazi hivyo kulazimika

wao kuwa vibarua katika mashamba ya wawekezaji ili kujikimu kimaisha. Hali hiyo pia imechangia wanaume

kulazimika kutoa rushwa ya pesa ili kupata kazi katika mashamba.

"Wanawake na wasichana wamekuwa wakifanya vibarua katika mashamba ya wawekezaji kwa ujira mdogo kati ya

shilingi (2,500/- na 3000/- tu kwa siku). Wakati huo huo wanakumbana na ukatili katika ajira hiyo ikiwemo

rushwa ya ngono, hali ambayo inasababisha  ongezeko la  magonjwa ambukizi yakiwemo VVU na Ukimwi.

Alisema licha ya Sera ya Taifa ya Maji kuweka lengo la kupatikana kwa maji katika umbali kwa mita 400; 

bado maji safi na salama ni changamoto kubwa kwa wakazi wa Kishapu na Mshewe kwani hakuna huduma za maji

safi na salama hali inayotishia maisha na afya zao.

"Mfano Kijiji cha Ilota- Mshewe, licha ya uhaba mkubwa wa maji wananchi wanasaka maji katika eneo

hatarishi huku wakichangia maji kidogo yasiyo safi na salama pamoja na mifugo. Cha kusikitisha  wananchi

wamechanga pesa kwa ajili ya maji kwa muda mrefu bila mafanikio. Katika vijiji vya Isoso na Lubaga Kata ya

Kishapu, ukosefu wa maji umesababisha wanawake na wasichana kutembea umbali mrefu na mazingira hatarishi

ambayo yamesababisha ongezeko la mimba za utotoni, ubakaji kwa wanawake na wasichana na vipigo."

Alisema tatizo hilo limeongeza umasikini wa kipato kutokana kutumia muda mwingi na rasilimali kusaka maji.

Kilio chao kikubwa ni kupata vyanzo mbadala vya maji hasa kutoka zi wa Victoria. Aidha aliongeza utafiti ulibainia huduma mbovu za afya kwani katika Kijiji cha Ilota Mkoa wa Mbeya wananchi wamekiri kutokuwepo na zahanati hali inayosababisha wanawake wajawazito kujifungulia majumbani, huku Kata ya Kisaki Morogoro vijijini, tatizo kubwa likiwa ni ukosefu wa dawa na wahudumu wa afya zahanati za vijiji vya Gomero, Station na Nyarutanga licha ya uwepo wa majengo mazuri bila wahudumu, dawa wala vifaa tiba kwa ajili ya uchunguzi. Eneo hilo pia wananchi huchangia gharama kubwa za usafiri wa gari la wagonjwa (shs 70,000) kwenda Morogoro hususan wanawake wanaokwenda kujifungua.

Alisema suala la viongozi kutowajibika na vitendo vya rushwa limejitokeza karibu maeneo yote ya utafiti
ikiwemo uwepo wa usiri wa taarifa za mapato na matumizi, viongozi kutowashirikisha wananchi katika masuala

ya maendeleo, viongozi ngazi za vijiji kuruhusu video za ngono kuoneshwa maeneo yao na kutotekeleza ahadi

zao kwa wananchi.
 
"Unyanyasaji wa kijinsia umejitokeza kama suala mtambuka  katika maeneo yote. Mfano tatizo la maji

linasababisha vipigo kwa wanawake, ubakaji, elimu duni kwa wasichana, mimba za utotoni na ukosefu wa

kipato. Kwa upande wa uwekezaji/ardhi, wanawake na wasichana wamekumbana na rushwa ya ngono, ajira isiyo

na staha pamoja na kipato kidogo na kwa upande wa afya, wanawake wamekuwa wakidaiwa fedha na vifaa wakati

wa kujifungua na hata kujifungulia katika mazingira hatarishi," alisema Mallya.

Aidha alisema lengo kuu la utafiti huo ilikuwa kujenga mifumo mbadala dhidi ya mfumo dume, uliberali mamboleo na mifumo yote kandamizi, huku akidai maafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuendeleza kampeni ya Haki ya Uchumi: Rasilimali Ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni ambayo imewezesha kujenga nguvu za pamoja na kuongeza uelewa wa masuala ya kijinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

_____________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment