Saturday 8 June 2013

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Taifa Stars Yetu Kwenye ' Mama' Wa Mechi Zote Usiku Huu!

Mungu yu mwema na atatuwezesha tufike Brazil.Heri nawatakia na ushindi tumeshaupata .Amen
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

From: zittokabwe@gmail.com
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 08 Jun 2013 07:45:57 +0000
To: <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Taifa Stars Yetu Kwenye ' Mama' Wa Mechi Zote Usiku Huu!

Nipo Marrakech toka juzi kuwapa nguvu na moyo mashujaa wetu. Watanzania kama 60 Hivi wamekuja hapa kutia nguvu. Vijana wa kiafrika wanaosoma hapa Morocco wamejitokeza kuja kutushangilia.

Vitimbwi

Wapinzani wetu wameanza vitimbwi Jana kwa kutuchelewesha kuanza mazoezi kwenye uwanja tutakaochezea mechi. Kwa mujibu wa kanuni za FIFA timu ngeni hutakiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja ule ule utakaochezewa mechi kwa muda ule ule. Jana tumefika uwanjani tumekuta timu mwenyeji ndio anafanya mazoezi na askari wao wakatuzuia kuingia. 

Kundi la vijana kama 20 wa Kitanzania wakavamia geti, wakamkamata askari na kfungua geti kwa nguvu. Tulipoingia kwa nguvu ndio wakaona duh Hawa watanzania wanamaanisha. 

Tulipoanza mazoezi wakazima taa za uwanja. Taa ziliwashwa baada ya Kelele na intervention ya bwana Magori ambaye ndie mkuu wa msafara.

Morali.

Vijana wana Morali kubwa sana. Timu inayoanza ni timu ya kushambulia haraka na kufunga. Mbele watakuwa Samatta, Kiemba, Ulimwengu na Ngasa. Lengo moja tu kuwafunga magoli ya haraka na mwanzo ili kuwachanganya. 

Wapinzani

Wamejizatiti sana. Kikosi kilichokuja Dar kimefumuliwa. Wameleta wachezaji wao Wote wanaocheza Ulaya. Hata hivyo wananchi wa Morocco wamegawanyika sana kuhusu mechi ya leo. Mitaani wanatwambia wafungeni tu hao! Nadhani kuna sintofahamu kubwa kufuatia nchi yao kufanya vibaya katika michuano hii.

Nini?
Ni dhahiri Sisi Tanzania tunapenda mafanikio bila kuwekeza. Timu hii ni nzuri sana lakini hatukuwekeza kama Taifa kuijenga. Mafanikio ya mpaka sasa ni juhudi za wachezaji, mwalimu na bahati ya mungu. Hivyo ushindi kwetu ni mwendelezo huo huo. Laiti kama tungekuwa tuna ari kidogo ya kuwekeza kwenye soka Tanzania ingekuwa mbali sana.

Tunashinda?
Nafasi ya ushindi ni kubwa sana. Tumejiandaa tuwezavyo. Vijana wapo vizuri kisaikolojia na nidhamu nzuri sana. Thomas na Mbwana wana uchu wa magoli kupita kiasi. Nahodha Kaseja yupo fiti sana. Erasto Nyoni, Kapombe, Aggrey Morris, Yondani wapo imara kuwazuia waarabu Hawa. Frank na Salum 'sureboy' watashika vizuri kati kati.

Dua zenu ni muhimu sana. Taifa letu linahitaji jambo la kujivunia. Taifa Stars wanalileta jambo hilo. Cross your fingers and 'Tanzania Gooooo' 

Zitto

Marrakech, Morocco 

Sent from my BlackBerry 10 smartphone.
From: Maggid Mjengwa
Sent: Saturday, 8 June 2013 05:42
To: mabadilikotanzania; wanabidii
Reply To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: [Mabadiliko] Taifa Stars Yetu Kwenye ' Mama' Wa Mechi Zote Usiku Huu!

Stars Yetu Kwenye ' Mama' Wa Mechi Zote! Usiku Huu

Ndugu zangu,

Taifa Stars yetu inaingia uwanjani kupambana na Morocco. Ni ' Mama' wa mechi zote.

Tafsiri yake?

Ni mechi muhimu sana kuwahi kuchezwa na Stars kuwania tiketi ya kucheza mashindano makubwa kabisa ya soka hapa duniani; Fainali za Kombe la Dunia.

Matokeo ya mechi ya usiku huu kwa kiasi kikubwa sana yataamua hatma ya safari ya Stars yetu kwenda Brazil.

Tukishinda ina maana kubwa hata kisaikolojia kwa wachezaji wetu na wapinzani wetu pia. Kwetu kutakuwa na momentum ya ushindi kwa wachezaji wetu watakayokwenda nayo kwenye mechi mbili zilizobaki; moja nyumbani na nyingine ugenini.

Na Ivory Coast watakuwa na presha kubwa sana. Itatusaidia zaidi sisi. Tukifungwa usiku huu , basi, mbele ya njia yetu ya kwenda Brazil kutakuwa kumejitokeza mlima mkubwa sana na mgumu kuupanda. Sare pia itatuweka mashakani. Kinachotakiwa ni kushinda tu.

Niliwaona Morocco walipokuwa Dar. Stars wasibweteke na ushindi ule dhidi ya Morocco wakadhani kuwa Morocco ni wepesi. Wakumbuke ni Morocco hawa waliotoka sare na Ivory Coast.

Morocco niliowaona pale Neshno Stadium ni wazuri. Walikuwa na mpango kwenye mechi. Moja ya mpango wao ilikuwa kucheza kwa kuitafuta droo. Bahati mbaya kwao, kuwa Samatta na Ulimwengu waliwavurugia sana mpango wao na wakawa katika hali ya kuchanganyikiwa uwanjani.

Morocco tutakaokutana nao leo ni wengine kabisa. Ni Morocco wanaowajua akina Samatta na Ulimwengu. Ni Morocco watakaoingia uwanjani wakiwa na mpango mwingine kabisa wa mchezo. Na sisi lazima tuwe nao wa kwetu. Na si wa kuitafuta droo. Mpango wa KUSHINDA MECHI. Kupambana kwa dakika zote za mchezo hata tukiwa nyuma ya goli moja.

Ni muhimu ni kujitahidi kufunga goli ndani ya dakika 15 za mwanzo ili kupunguza presha ya mashabiki wa Morocco dhidi yetu.

Naam, mechi ya leo ni ' Mama' wa mechi zote. Watanzania kwa Umoja wetu tuwaombee na kuwashangilia Stars. Kwa nguvu zote.

KILA LA HERI STARS, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment