Emmanuel. Uko sahihi kama nilivyo sahihi. Na ndiyo Mazingira. Unaweza kupatana na adui yako baada ya kumsamehe. Kinachotafutwa hapa ni kusameheana. Kama Kagame ameharakisha kuwasamehe aliowasamehe Sasa ni zamu yao nao kusema wanayomdai Kagame halafu wamsamehe pia. Tanzania ilikuwa na wakimbizi 1994-1996 kutoka Rwanda. Wengi walikuwa wahutu. Swali moja la kujiuliza Walikimbia nini kama walikuwa wanaua? Bila kuwasikiliza ukamsikiliza Kagame tu utaishia kumuonea huruma na kuwaonea huruma watutsi kumbe na wahutu wanastahili kuonewa huruma maana genocide ilikuwa ya pande mbili. Kama Habyalimana au serikali yake ingedumu baada ya kuuawa tungekuwa tunasikia kuwa watutsi waliua wahutu. Kikwete ameona kama ilivyokuwa kwa MPLA na UNITA na FRELIMO sawa na unavyoeleza kuwa ililazimika (KIKwete) kishaona kuwa inalazimika hawa kuongea. Tunaweza kumkubalia au kusubiri kila mmoja aseme sasa ni lazima waongee, labda baada ya miaka kadhaa. mafuvu yatakuwa yameongezeka ya pande mbili. Kikwete alilenga kuepusha hilo. Si jambo dogo kuwa sasa sauti moja imesema Kagame aongee na FDLR. Sauti hiyo moja ina tatu au nne nyuma yake. Tusubiri tuone
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment