Wednesday 5 June 2013

Re: [wanabidii] MPENZI ANATAKA NYUMA....


Tracy, Mshauri huyo mdada aachane naye huyo bwana kabisa. Maisha sio huyo mtu tu, awe na ujasiri.

Tatizo ni la wanawake, mwanamke anapopenda anaingia mzima mzima anapenda kwa moyo, kichwa, tumbo, miguu, macho anakuwa haoni kingine tena na masikio-kiziwi haoni na kusikia mifano ya wenzake. Hakubali.

Ndio maana mwanamke au msichana akiachwa na boyfriend au mume-anachanganyikiwa kuliko mwanaume na anawerza kujiua au kufeli mitihani. Na ikiwa huyo ni bwana wake wa kwanza aliyemtokea-ndio haoni kabisa kipofu, hasikii na anaweza akaharibu masomo au kazi kama ataachwa ghafla. Hivyo anapata tabu kuamua aachane naye anaona kama mbingu itashuka imuangukie, bora avumilie hivyo hivyo baadae kicha kinakuja kuchanganya.

Mwenzake huyo alizoea siku nyingi ila alikuwa anamlia time tu amzoee ili amwambie. Yeye-alishindwa kugundua au kutambua alama za nyakati.

Ndio hao wanawake wasio maamuzi. Mume anabaka housegirl anatia mimba, anambaka mdogo wake anayeishi naye au mwanae wa kufikia anawazalisha wote bado mke yup radhi kuficha evidence amwache aende jela naye akasulubiwe huko eti anampenda, hataki afungwe kama amekosa amemsamehe. Hapo ndio sheria za nchi zinatakiwa zimkamate na huyo mama msicha siri akalale ndani na mume pia.
Akikataa uchafu huo eti mume analeta bibi wa nje  kwa vile yeye hataki hiyo Tigo na anamlazwa chini au mke unalala na watoto chumba kingine na bado upo.

Tujifunze ujasiri na kuweka kuwa na maamuzi. Atakapokubali na kuharibika ataachwa pia atatafuta mwingine. Madhara ni mengi sana pamoja na kuambukizwa magonjwa ya zinaa, kuchubuka maana huko hakukuumbika kwa kazi hiyo na mengine kisaikolojia.

Zipo study nyingi sana za sexual violence, sexual abuse na extent of sodomy in Tanzania zilizofanywa na wadaktari na wengineo Muhimbili, NGOs.

Binafsi nimefanya ya sexual abuse kwa wanafunzi Kilosa, Lindi, DSM na ya Extent of Sodomy TZ sample dar, bagamoyo, ZNZ na kujumlisha na ile ya sodomy kwa wanafunzi. Sodomy ni tatizo ktk ndoa. 1% ya ndoa huathiriwa na suala hili. Wanafunzi mashuleni sexually active waliofanya sodomy tulipata ktk sampo yetu 67% wanaongoza kwa hiyo Tigo. Hufanya jambo hili kuzuia mimba. Wanaume mpaka wa umri wa 26 waliripoti kubakwa/kulawitiwa. Wanaume (2%) walitoa taarifa ya kufanyiwa mchezo huu na waajiri wao mpaka baba mwenye nyumba kwa vijana houseboys au waajiri wenye maduka anakofanya kazi (hawa umri mdogo). Wanaobakwa umri mkubwa huwa ni mpango na ushindani kibiashara, kugombania mwanamke/msichana, kufumaniwa. Unasukiwa zari ili uhame eneo la ushindani au umuache mwanamke mnayegombania baada ya kukutumia vijana bangi bangi wanakutesa na kukupiga picha na kukutishia kuziweka hadharani; au kukutangaza na ukipita watu wanakucheka au ulitendewa ukaachwa hoi ukaokotwa huna nguo na umechafuka.

Wanaume tuliowahoji ambao walitoa taarifa za kubakwa tuligundua kuwa ndio waundao magenge ya ubakaji. walipoulizwa  kama wataendelea na sodomy walisema 'Yes'. why? alijibu-anapomfanyia hivyo mtu 'me' au 'ke' anapata ahuheni au nafuu kisaikolojia kuona kwamba amemuadhibu mtu kama yeye alivyoadhibiwa kwa kumfanyia hiyo Tigo. hawa wanaume hawapati ushauri nasaha na hawajitokezi kama wanawake wabakwao. Yupo baba mmoja Dodoma alibakwa akitoka kulewa pombe alifariki kutokana na depression ya kufanyiwa tendo hilo. Yupo yule aliyetolewa ktk gazeti ambaye alikuwa akibaka wake za watu (Dodoma). akawamaliza mjini eneo lake na akaanza kuwafanyia wanaume (Kiuchawi) akakamatwa nyumba ya mlokole mmoja anayesali sana uchawi ukaishia hapo. Ndipo aliposimulia yote aliyofanya. Wapo wengine wana mapepo na wapo watumiao uchawi wasionekane bali wanafanya uchafu majumbani mwa watu na mashuleni. Hawa wana laana. wapo wanafunzi wanaofanyiana wenyewe kwa wenyewe au kuonea wale wadogo kuwaingiza machakani, mabanda mabovu etc. Fundisha mwanao vizuri aepuke haya.

Wapo ndugu unaokaa nao na kuwalaza na watoto wako wadogo hao ndugu au mgeni aliyekuja, au kulala na houseboy, shamba boy/mfuga mifugo wako wa dairy cattle DSM-hawa tazama weka onyo kwamba ukimsikia na kupata taarifa kwa mtoto utamfunga tu. waelimishe na watoto ambao hutishiwa na kuhongwa visent, kaka anampenda sana na kumlea vizuri kumbe anamuharibu wewe hujui. kagua watoto me na ke mbele na nyuma ili nao waogope na hao waishio nao. Usichanganye watoto wakubwa na wadogo ktk malazi kutokana na uhaba wa vyumba na kuchanganya watoto wa umri tofauti-wengi wameharibika na ndio chanzo cha ushoga-anazoea.

Wapo changudoa ambao ni Toigo na Voda kwa bei tofauti hawa huharibu waume za watu. Anapozoea-inakuwa tatizo ktk ndoa. Tulipowahoji wale ambao walifanya mchezo huu mbaya kimila na maadili ya kiafrika na kidini:-wale walioanza na wasichana mambo ya Tigo-HAWAKUWAOA HAO WALIOFANYA NAO HAYO. WALIOA WENGINEO AMBAO HAWAKUENDELEA NAO HAYO. Wasichana/wanawake walioanza mambo hayo shuleni walipoolewa-hawakufanya na waume zao ambao hawakuomba suala hilo na wala mume hakujua kama huyo alishafanya hivyo. Ni wachache sana waliolazimisha wake zako kufanya tendo na kutishia talaka, moto unawaka daily na anakwenda nje anamaliza mambo yake anarudi apendavyo. kama wewe hutaki, wenzako wanataka-bye-anatoka!!

Utafiti huu tulifanya 1997 na tuliangalia kama mchezo huu mtu alianza kwa sababu ya kuwa pwani (sample, DSM, Bagamoyo, ZNZ). Utafiti haukuona uhusiano wa kuwahi kuja au kuishi Dar na kupenda upotofu huu wa Tigo. Mtu alianza akiwa Songea, Iringa, Mwanza, Mbeya. Ni pale yalipomkuta maisha na matatizo hayo akiwa dar au popote pale kwani tuliangalia alizaliwa wapi Tigo, kabila lake na Dar, Bgmoyo, ZNZ kafika lini. Mazingira  ya maisha ni muhimu zio kuwa Pwani au visiwani. yupo ambaye aliweka alama ya vema kuonyesha akiwa mwanaume-ameolewa, ameoa, ametalikiwa na ametaliki. Hii ilituchanganya. Lakini alikuwa na bwana (sodomy-kama gay) akaachwa na bwana; akaoa akaona haimfai akamuacha mke -akataliki.

Utafiti tumeuendeleza kila mwaka alipopatikana mtu au kikundi cha masuala haya hadi sana. Tumeongea na bisexuals, gays, transgender na lesbians. Tumeangalia pia alianzaje akiwa wapi na circumstances, anaishije, maisha na matatizo. Tusijidanganye, matatizo ni makubwa sana na source 80% ndani ya familia kunatoka watu hawa. Sasa wale ambao ndio wateja wa gays wamebadilika sura na gays wanakotoka imebadilika sana kidini (imechanganyika) na kikabila uelekeo umebadilika na huwezi kuamini. sitoongea hapa.Aina za gays na lesbians ni nyingi pia sio moja tu. Ndani ya familia (ndoa) na mahusiano kwa sasa kuna usumbufu zaidi wa watu kupenda haya unayoongea hapa tracy pamoja na kuwepo ukimwi na elimu juu ya magonjwa ya STDs na cancer za koo kutokana na watu kufanya mila iliyokataza. sio sigara tu kuleta cancer au viroba na mengine yaingizayo virus kooni. Waafrika hatupendi kuongea ukweli-tunajidanganya lakini nyuma ya pazia-ndio wenyewe.
Tukazane na maadili ya kiafrika katika mahusiano. Kiafrika mume akitaka Tigo ilikuwa ni leseni ya ndoa kuvunjwa. wapo wanaowafundisha wasichana wasiojua kuwa hiyo ni njia ya kawaida ya mapenzi nao wajinga hawajui. watu wa race nyingine hutumia Tigo kama uonevu na kukomoa kuchezea hao masikini si unampa hela. Wanawapangia vyumba/nyumba lakini akirudi kwake unamuona kama mtu safi mheshimiwa lakini amempangia shoga hata kama home hafanyi hivyo na mkewe.

Siku mke akimfumania mumewe na shoga marafiki wakimtonya-anamvaa shoga na kumpiga mume anamuacha-analinda ndoa na penzi. Yawezekanaje kakijana kadogo kamlazimishe baba mtu mzima ambaye ni mumeo umemfumania lakini humpigi? unaleta umma kumpiga shoga? shoga wamelalamika mengi wanapokamatwa na kuwekwa korokoroni. Sitosema hapa.

Huenda kitabu kitatoka kabla mwaka kuisha ili tujione katika kioo chetu wenyewe tuavche unduma kuwili. NGO yetu imetibu kwa kujitolea watoto wanafunzi wanaobakwa majumbani na njia ndefu ya kwenda wenye STDs (kilosa) na kujaribu kufikisha mahakamani baadhi ya kesi za ubakaji-ikashindikana kutokana na rushwa; mila za kiafrika za usiri kufanya mke, ndugu kuzuia na viongozi wa kijiji kutokutoa ushirikiano.

Asiyefahamu afahamu haya ni ya ukweli si porojo. Chunga wanao na vijana wako, akizoea anakuwa anataka haya ktk ndoa.


--- On Wed, 5/6/13, Tracy John <tracykwetu@gmail.com> wrote:

From: Tracy John <tracykwetu@gmail.com>
Subject: [wanabidii] MPENZI ANATAKA NYUMA....
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, 5 June, 2013, 13:43

kuna dada mmoja amenihadithia jambo akiomba ushauri anasema ana mpenzi wake wanaopendana sana wamekuwa pamoja kwa miaka mitano sasa, kila siku ya maisha yao haijawahi kutokea akajutia kuwa na huyo mpenzi wake..

kwa muda huo wote walikuwa wakikutana kimwili kwa njia ya kawaida tu ile ambayo inaruhusiwa kihalali na wala kulikuwa hamna tabu wala hamna mtu ambaye hakuridhika na starehe ambayo mwenzake anampa..

anachoshangaa yeye ni kwamba mwezi wa tatu huu sasa jamaa ananuna hataki hata kwenda nyumbani kwa huyo dada kisa jamaa amechoka kula mbele peke yake anataka kanga igeuzwe upande wa pili..

huyu dada alikataa na kumwambia hiyo siyo sahihi kwake, kitu mpenzi wake alichomjibu ni kwamba kwani wewe upo nji gani wasichana wenzako siku hizi wengi huwapa wapenzi wao upande wa pili kwa nini wewe hutaki kunipa? kama hutaki inamaana utaanza kumpa mtu mwengine ama unaona mimi sifai?

yule dada kwa uchungu anasemakila siku alikuwa anampigia simu mpenzi wake akilia akimuomba aachane na hayo mawazo, lakini kijana bado anadai anataka, anasema sasa umekuwa ugomvi mkubwa sana kati yao na anahisi wataachana kinachomuuma nikwamba anampenda sana mpenzi wake huyo, na mpenzi wake haelewi somo lengine kabisa huyu dada sasa hajui afanye nini...

akiomba ushauri kwa rafiki zake wengine wanamwambia ampe tu huyo mpenzi wake kwani atabadilisha wanaume wa ngapi? wengine wanamwambia hiyo ni dhambi kubwa lakini akitaka anaweza tu kumpa kwani dhambi ngapi amefanya tokea amezaliwa iwe hiyo moja? wengine humshauri kwamba siku hizi mpaka machangu wengi hutoa nyuma ama unataka aende akachukue kwao akileta magonjwa je?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment