Nijuavyo mimi-Kazi au wajibu wa serikali ni kuongoza na kuwezesha. Kuna Katiba halafu vitu vya misingi (principles) zilizomo ktk Katiba huingia katika Sera. sera hutekelezwa kwa kuundiwa Mikakati ya Sekta (strategies) ambazo huwa na mpako kazi wenye malengo, shughuli na viashiria na bajeti ambayo hupitishwa na bunge. Halafu yote hayo principles na sera hulindwa na Sheria ya sekta hiyo husika-mfano Haki za binadamu (sheria ya ndoa, mirathi; sheria ya mtoto etc). Kuna sheria ya ardhi nayo hutaja haki; sheria ya misitu, wanyamapori, marine parks, bahari na uvuvi; mifugo; madini; mazingira; maji; usafi wa mazingira, afya, uraia etc. Lakini waswahili husema-unaweza kumswaga Punda mpaka mtoni ila huwezi kumlazimisha-kunywa Maji. Weka sera, mikakati na Vision (Dira) zake; weka sheria mfano sheria itambue uwepo wa imani wa kuabudu na dini tofauti hata za kimila; itambue na ardhi ya kimila. Kwa Mtanzania (binadamu) vyote hivi vinapinda au kupindishwa. Unamuongoza mtu na kumwambia-elimu ni ufunguo wa maisha-soma usiozeshe mapema; ukimwi unaua usiwe na mpenzi zaidi ya mmoja (sikio la kufa anaoa mitala eti dini inaruhusu na ana vimada na wakezake wana mabwana pia); panda mti ukatapo mti (anachimbua mti hadi mizizi) hapandi; fuga mifugo kisasa, punguza mifugo unaharibu mazingira unayotegemea umezidisha beyond carrying capacity kwamba ardhi haiongezeki bali watu na wanyama huongezeka. Unaweka ni nvyuo vya kilimo, vya mifugo na mifano ya mifugo na kilimo cha mazao, unawapeleka study tour, una extension staff wa kuwaelekeza. Watakaoiga 1 kati ta 10 na huyo mmoja watamuibia. Kuwa na mingi ni cultural definition ya wealthy class hiyo ndio priority. Unawaeleza kuwa -Eneo hili ni la kulima mtama mtama sio mahindi ukilima utakosa chakula-Lima mtama na ufuta ni almasi uuze ununue mahindi na mchele. Analima ekari na ekari za mahindi na mpunga-anakosa kabisa. Kisha-serikali haitujali kutupa chakula cha misaada cha njaa-kila mwaka atalima hilo hilo bado. Na wale wamabondeni-mafuriko hadi kila mwaka na kupoteza familia na mali-sihami au nitahama nikilipwa fidia-alikuambia nani ukae bondeni? wakipewa kiwanja na mabati wajenge-anauza plot na mabati na hema linachoka linaishia anakuwa na tabu zaidi-anarudi bondeni. Mifano michache ya kuwajibika. Jee uwachape fimbo watu wazima? uwafunge-jela kubwa kiasi gani unayo na kuweza kuwalisha daily? Pita vijijini uone-utalia kama unaipenda nchi yako. Unaambiwa usivue kwa baruti unaharibu mazalia ya samaki-miamba na mazingira yake; vua kwa nyavu tundu kubwa-hataki; chandarua kuzuia malaria, lalia daily-anaokotea chupa tupu, anafunikia mchicha-halalii anaogopa kupungua nguvu za ulijari. unamwelimisha, kumuwezesha, kuweka vikoba, mikopo, leseni za wazawa vheap-hajiungi kkt vikundi; anaua albino na kukata watu viungo atajirike sio mikopo usemayo na kujiunga. Umfanye nini? Haki zako ni wajibu wako pia. Huwezi kudai haki ikiwa hutimizi wajibu. Serikali ni nani? Mfanyakazi serikalini ni mwanao, nduguyo, jirani yako. Ni yule unayetoa kodi akalipwa ujira, akawa mwizi wa mali ya umma katika umri mdogo maana anapenda anasa, anayemlipa fidia anayebomolewa nyumba ipite barabara kizee wa watu anatakiwa alipwe milioni 20 yeye anampa milioni 2. anayetoa plot moja kwa watu zaidi ya mmoja; anayefungua zahanati akapeleka dawa za CHF huko na akikamatwa unamuwekea wakili na mnajazana mahakamani kusikiliza kesi. Ni yule anayempa mimba mwanafunzi akiwa bosi halafu mzazi unafuta kesi unachukua kitu kidogo. Hapa nawe ni serikali maana unatakiwa usimamie utendaji bora kama mwananchi na sheria ya ubakaji ipo ale miaka 35 wewe unakubali kupokea milioni 5 na huitumii kimaendeleo. Unapompigia kura kiongozi anayeshutumiwa kwa ufisadi, udini, ukabila na anashinda kura-haki yako na wajibu wako umeuharibu na umeharibu majukumu ya viongozi na watawala wa serikalini ambao wanausimamizi mwema hawapendi uovu. Ukimlinda mtumishi kibaka hata awe mumeo, mkeo, mwanao unaona anafanya magendo, ananunua magari kibao kazi kaanza jana-unaficha mwizi hutimizi wajibu wako. Kwani serikali ni nani na raia ni nani? Mbona mkuu wa wilaya, mratibu kata, bwana/bibi kilimo ni mume/mke na ndugu wa mtu? Mbona wakikosea nyumbani hatuwaweki kitako kifamilia au kimila wajirekebishe mpaka wanafungwa? Tunalindana. Mbona ukeketaji wasichana unaendelea ndani ya familia Kisiri-tunakiuka haki na sheria iliyopo baba na mama na ndugu? Yatima anadhulumu nani na sheria iliyotungwa ba serikali kuhusu mirathi ipo? serikali ni wewe, mimi (Raia) na walioajiriwa na kuchaguliwa, viongozi wa mila na dini, wote tunawajibika. Kiongozi uwe mfano Jimboni kwako kwanza na kijiji chapo kiwe super tuje tujifunze huko sio kupiga kelele tu bungeni, vijijini maeneo yako kila kitu kipo hakuna lolote ufanyalo kuhamasisha kikaonekana. Tukifika 50% hawana vyoo, maji wanakoga hapo hapo, kufua na kuchota. wakichanga elfu 2 kijiji chote kila mtu utapata hela za kuchimba borehole kadhaa ukaweka handpumps-hufanyi hivyo ila-maandamano! ushindwe na ulegee kiongozi wa namna hiyo. kama mtumishi wa umma na wa GVT- Wajibika Raia asipozingatia sheria mfano ya ujenzi, viwanja vinapimwa, anabananisha nyumba na kuziba njia eti anaganga njaa-mji unakuwa makorokoro. Kisha moto ukiwaka, njia ya kupita kuzima moto hakuna-inakula kwake. anapata hasara na asipojirekebisha-utawaka kila mara na kumrudisha kimaendeleo. anaona hapo jirani kunauzwa gas, kuna pharmacy na viripuka, kuna kuranda mbao na vyumbi la mbao, yeye hapo jirani anaweka welding ya vyuma inayorusha cheche za moto. haoni au haujui moto? Mtu mzima aonyeshwe mifano mingapi ya moto na kufa mbona anaiona. kiziwi na kipofu. Ikija timu ya kubomoa-wanatoka na mapanga, pakiungua-serikali haina wajibu kwa raia, haitimizi wajibu wa usalama kwa raia wake? Kichwa hicho kizima? Nawashangaa hata wanawake, mume au bwana kabaka mwanae wa kuzaa au mtoto wa kambo-msameheni mume wangu, tutakula wapi. Hili kwanza ni kosa lake la kwanza. anafanya mbinu kufuta na kukana ushahidi atoao mtoto, wanahonga wapimaji watoe vithibitisho sivyo. doctor wa awali kaandika alibakwa na uthibitisho, wa majuu anaonyesha vingine kinyume. haangalii kuathirika kwa mtoto ila pensi na kula ambapo anaweza kujitegemea. Na mume akitoka hapo-anawakimbia anahamia mbali. Mjini Shule-tunasomeshana kila mtu na msimamo wake, wangu ni huu. --- On Tue, 4/6/13, Rashid Maalim <rashid.o.maalim@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment