Thursday 13 June 2013

Re: [wanabidii] Katiba Mpya!

kaka una mawazo mazuri sana tatizo ni hao jamaa wa zanzibar hawataki kabisa serikali ya umoja wanataka wao wawe na dola yao sasa katika hali kama hiyo ni n gumu kuwa na mfumo wa serikali mbili maana ndo tulizonazo lakini zimezaa ugaidi kule zanzibar. wale jamaa wanayoyafanya mimi nahusianisha sana na fukuto la wao kutaka dola kamili japo si mpango wa serikali ya mapinduzi kuleta shinikizo kama lile. Sasa huu mfumo wa serikali3 utafaa japo una gharama maana heri gharama hizo kuliko machafuko au gharama zaidi za kiulimzi/usalama Zanzibar ikijitenga sababu ya kulazimishwa kwenye mfumo wa serikali 2 au 1 ambazo wao zanzibar hawataki hata kuzisikia


From: Pius Makomelelo <makomelelopius@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, June 12, 2013 11:02 AM
Subject: [wanabidii] Katiba Mpya!

Naililia nchi yangu Tanzania. Sijaishi upande wa visiwani nikajua fika matatizo waliyonayo wenzetu hawa kuhusiana na mfumo wa utawala tulio nao. Ninachojua Zanzibar siyo koloni la Tanganyika. Natafakari, naona kama kuna kosa vile lilifanyika. Kama Tanganyika ilifutwa kutoa nafasi kwa nchi ya muungano inayoitwa Tanzania, kwanini pia tusifikilie kuondokana kabisa na hizi serikali ndani ya serikali!! Hivi Muungano huu ni wa nani? Kama si wa wachache, kwanini tusitangaze tu uwepo wa serikali moja ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania yenye kuongozwa na serikali moja na si mbili wala tatu!!. Tupeni basi nafasi tupige kura kama kusikilizana kwa kawaida imeshindikana. Hapo tutapata maoni sahihi ya kila upande. Hivi Tume ya Katiba kwanini wanapata kigugumizi kutoa pendekezo hili kama kweli muungano huu tunaupenda sote? SITAKI kufikia mahali kulazimika kuomba uraia wa Tanganyika au Zanzibari kama tokeo la shinikizo la mabadiliko toka kwa watu wachache wenye uchu wa madaraka!! Najaribu kutafakari!!! 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment