Thursday 13 June 2013

Re: [wanabidii] CCM DHIDI YA SERIKALI 3

Exactly Comrade Salum;
Kuwa na Serikali tatu kutaendelea kuleta nyufa katika muungano kwa maana upande mwingine wenye kuona hakuna sababu za msingi za kuwepo muungano utakuwa na nguvu ya serikali (SOVEREIGN POWER) ambayo still itakuwa threat kwa future ya muungano labda waendelee CCM kutawala huko kwenye maji otherwise itakuwa issue tu.

Halafu jamani,unawezaje kusema upo kwenye ndoa yenye amani na upendo na familia yenye furaha kama Baba na Mama wanalala kila mutu chumba chake?Serikali moja ndo amani ya Muungano otherwise kila mutu achukue mbao zake.

Reuben



--- On Thu, 6/13/13, salum mkango wrote:

> From: salum mkango
> Subject: Re: [wanabidii] CCM DHIDI YA SERIKALI 3
> To: "wanabidii@googlegroups.com"
> Date: Thursday, June 13, 2013, 2:40 AM
> Kwa aina ya viongozi
> tulionao na mfumo wa serikali kuwahudumia mpaka mahause boy
> wao, serikali tatu ni mzigo mkubwa kwa taifa. Kama
> tumeungana kwa nini tusiwe na serikali moja na wengine
> wabaki kama majimbo tuuuuu????
> From: Gikaro Ryoba
>
> To:
> "wanabidii@googlegroups.com"
>
> Sent:
> Thursday, June 13, 2013 12:31 AM
> Subject:
> [wanabidii] CCM DHIDI YA SERIKALI 3
>
>
>
> CCM
> DHIDI YA SERIKALI 3
>
> Chama
> tawala
> nchini Tanzania, CCM bado kinaonekana kuendeleleza sera yake
> ya kupinga muundo
> wa serikali tatu ambao hivi sasa unapendekezwa pia katika
> rasimu ya Katiba Mpya
> iliyowasilishwa mwanzoni mwa wiki iliyopita. Itakumbukwa
> kwamba hapo kabla tume
> mbili zilizoundwa zilipendekeza mfumo wa serikali tatu
> katika muungano kati ya
> iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar lakini mapendekezo yao
> hayakutekelezwa .
>
>  
>
> Rasimu
> ya Katiba
> Mpya imezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi wa Tanzania
> ambao ndio wenye
> maamuzi juu ya hatima ya nchi yao. Tume ya Nyalali na Jaji
> Kisanga zilipata
> maoni kutoka kwa wananchi, ambao ndio waliotaka uwepo wa
> serikali tatu. Inasikitisha
> kwamba CCM wanataka kuwaamulia wananchi aina ya serikali
> wanayaoitaka wao. Huku
> ni kusigina demokrasia na ni dharau kubwa kwa wananchi. Siku
> zote CCM inadhani
> kwamba wananchi ni mazezeta na kwamba hawawezi kujiamulia
> mambo yao wenyewe. Sasa
> ikiwa wananchi ndio wanaotaka serikali tatu, iweje kikundi
> kidogo cha wanachama
> wa CCM wajifungie chumbani huko Dodoma na kuazimia
> kuchakachua maoni ya
> wananchi?
>
>  
>
> Nchi hii
> ina
> jumla ya watanzania million 45. Wanachama wote wa CCM
> hawazidi million 5! Iweje
> kikundi cha watu million 5 watake kuchakachua maoni ya
> watanzania million 45? Hii
> ndiyo demokrasia kweli? CCM wanataka kubaka maoni ya
> wananchi kwa manufaa ya
> mafisadi wachache kama walivyozoea kuwatumikia mafisadi huku
> wakiwaacha solemba
> wananchi. Hii haikubaliki hata kidogo. Ifike wakati wananchi
> waone kwamba CCM
> haiweki maslahi ya wananchi mbele isipokuwa wanalinda
> maslahi ya wachumia tumbo
> wachache ndani ya chama na serikali. Hii maana yake ni
> kwamba serikali haina
> nia njema na ustawi na mustakabali wa wananchi bali
> inawatumia kama ngazi ya kutimizia
> haja zao za kiutawala na kinyonyaji!
>
>  
>
> Maoni
> yaliyozaa
> rasimu ya katiba hii yalitolewa na wananchi wote bila kujali
> dini, kabila,
> kanda, vyama, jinsia au hali zao. Kwa hivyo, sio busara hata
> kidogo kwa CCM
> kuwaelekeza wanachama wake wakatae muundo wa serikali 3
> wakati ni wanachama hao
> hao ndio waliohojiwa na kukubali kuwa na muundo wa serikali
> 3! Kufanya hivyo ni
> sawa na kuwashikia akili watanzania na kuwaona kama hawakuwa
> na akili nzuri
> wakati wanatoa maoni ya kuwa na serikali 3. Na nitawashangaa
> sana wananchi na wanachama
> wa CCM watakaokubali kushikiwa akili na kubatilisha maoni
> yao ya awali ya kuwa
> na serikali 3.
>
>  
>
> Tujiulize ni kwa
> nini tume zote tatu (Tume ya Warioba, Jaji Kisanga na
> Nyalali) waliamua
> kukusanya maoni ya wananchi badala ya kuwaachia CCM
> wawaamulie wananchi kama
> wanavyotaka. Kama hali ni hiyo basi ni bora tume hizi
> zisingeundwa na kutumia
> mamilioni ya walipakodi katika kusaka maoni ya wananchi.
> Basi tungewaachia CCM
> (wajuzi wa kila jambo) wajifungie ukumbi wa Chamwino huko
> Dodoma watuamulie watanzania
> aina ya katiba tunayopaswa kuwa nayo—jambo ambalo ni
> kubaka demokrasia
> waziwazi.
>
>  
>
> Enyi
> wanaCCM/wananchi,
> akili za kuambiwa changanya na za kwenu. Saa ya ukombozi ni
> sasa. Msikubali kamwe
> kulamba matapishi yenu wenyewe. Acheni msimamo wenu wa kuwa
> na serikali 3 ubaki
> hivyo hivyo. Nina imani kwamba kipindi mnatoa maoni yenu
> mlikuwa watu wazima na
> mlikuwa na akili timamu. Wapuuzeni hao wanasiasa wanaotaka
> kuchakachua maoni
> yenu kwa maslahi ya mafisadi na wachumia tumbo wachache.
> Wekeni maslahi ya nchi
> mbele ya maslahi ya chama. Vyama vinazaliwa na kufa lakini
> taifa la Tanzania litadumu
> milele. Tafakari, chukua hatua!
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>  
>
>  
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>  
>
>  
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment