Thursday 13 June 2013

RE: [wanabidii] CCM DHIDI YA SERIKALI 3

Ryoba,
 
Hao CCM they cannot think, they cannot feel, they cannot listen, they cannot sense. They are just out of touch. You cannot help them. The only way to help them is to vote them out. Then, they will go back to the drawing board and shape their thinking. They are outdated, conservatism and they cannot think outside the box. You cannot help them. Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Selemani
 

Date: Wed, 12 Jun 2013 14:31:22 -0700
From: gikaroryoba@yahoo.com
Subject: [wanabidii] CCM DHIDI YA SERIKALI 3
To: wanabidii@googlegroups.com

CCM DHIDI YA SERIKALI 3
Chama tawala nchini Tanzania, CCM bado kinaonekana kuendeleleza sera yake ya kupinga muundo wa serikali tatu ambao hivi sasa unapendekezwa pia katika rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa mwanzoni mwa wiki iliyopita. Itakumbukwa kwamba hapo kabla tume mbili zilizoundwa zilipendekeza mfumo wa serikali tatu katika muungano kati ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar lakini mapendekezo yao hayakutekelezwa .
 
Rasimu ya Katiba Mpya imezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi wa Tanzania ambao ndio wenye maamuzi juu ya hatima ya nchi yao. Tume ya Nyalali na Jaji Kisanga zilipata maoni kutoka kwa wananchi, ambao ndio waliotaka uwepo wa serikali tatu. Inasikitisha kwamba CCM wanataka kuwaamulia wananchi aina ya serikali wanayaoitaka wao. Huku ni kusigina demokrasia na ni dharau kubwa kwa wananchi. Siku zote CCM inadhani kwamba wananchi ni mazezeta na kwamba hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe. Sasa ikiwa wananchi ndio wanaotaka serikali tatu, iweje kikundi kidogo cha wanachama wa CCM wajifungie chumbani huko Dodoma na kuazimia kuchakachua maoni ya wananchi?
 
Nchi hii ina jumla ya watanzania million 45. Wanachama wote wa CCM hawazidi million 5! Iweje kikundi cha watu million 5 watake kuchakachua maoni ya watanzania million 45? Hii ndiyo demokrasia kweli? CCM wanataka kubaka maoni ya wananchi kwa manufaa ya mafisadi wachache kama walivyozoea kuwatumikia mafisadi huku wakiwaacha solemba wananchi. Hii haikubaliki hata kidogo. Ifike wakati wananchi waone kwamba CCM haiweki maslahi ya wananchi mbele isipokuwa wanalinda maslahi ya wachumia tumbo wachache ndani ya chama na serikali. Hii maana yake ni kwamba serikali haina nia njema na ustawi na mustakabali wa wananchi bali inawatumia kama ngazi ya kutimizia haja zao za kiutawala na kinyonyaji!
 
Maoni yaliyozaa rasimu ya katiba hii yalitolewa na wananchi wote bila kujali dini, kabila, kanda, vyama, jinsia au hali zao. Kwa hivyo, sio busara hata kidogo kwa CCM kuwaelekeza wanachama wake wakatae muundo wa serikali 3 wakati ni wanachama hao hao ndio waliohojiwa na kukubali kuwa na muundo wa serikali 3! Kufanya hivyo ni sawa na kuwashikia akili watanzania na kuwaona kama hawakuwa na akili nzuri wakati wanatoa maoni ya kuwa na serikali 3. Na nitawashangaa sana wananchi na wanachama wa CCM watakaokubali kushikiwa akili na kubatilisha maoni yao ya awali ya kuwa na serikali 3.
 
Tujiulize ni kwa nini tume zote tatu (Tume ya Warioba, Jaji Kisanga na Nyalali) waliamua kukusanya maoni ya wananchi badala ya kuwaachia CCM wawaamulie wananchi kama wanavyotaka. Kama hali ni hiyo basi ni bora tume hizi zisingeundwa na kutumia mamilioni ya walipakodi katika kusaka maoni ya wananchi. Basi tungewaachia CCM (wajuzi wa kila jambo) wajifungie ukumbi wa Chamwino huko Dodoma watuamulie watanzania aina ya katiba tunayopaswa kuwa nayo—jambo ambalo ni kubaka demokrasia waziwazi.
 
Enyi wanaCCM/wananchi, akili za kuambiwa changanya na za kwenu. Saa ya ukombozi ni sasa. Msikubali kamwe kulamba matapishi yenu wenyewe. Acheni msimamo wenu wa kuwa na serikali 3 ubaki hivyo hivyo. Nina imani kwamba kipindi mnatoa maoni yenu mlikuwa watu wazima na mlikuwa na akili timamu. Wapuuzeni hao wanasiasa wanaotaka kuchakachua maoni yenu kwa maslahi ya mafisadi na wachumia tumbo wachache. Wekeni maslahi ya nchi mbele ya maslahi ya chama. Vyama vinazaliwa na kufa lakini taifa la Tanzania litadumu milele. Tafakari, chukua hatua!


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment