Tuesday 14 May 2013

[wanabidii] WATANZANIA WENGI JIJI LA CARDIFF-WALES (UK) WAJIUNGA NA CCM

Katika ufunguzi huo Jumamosi tarehe 11 Mei 2013 ulijaa shamrashamra na nderemo na kuhudhuriwa na viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM Ndg Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti Ndugu Said Sukwa, Katibu Bi. Mariam Mungula, Naibu Katibu Ndugu Albert Ntemi, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Leybab Mdegela, Naibu Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu Mohamed Upete na wanaCCM toka mashina mbalimbali ya CCM UK.

Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM Ndg Maina Ang'iela Owino aliwashukuru Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Ndg Owino aliwakumbusha kuwa uhalali wa shina lao unajumuishwa katika Sera ya nje na matawi yake katika Katiba ya CCM.

Ndg Owino aliwakumbusha kuwa kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.

Aidha Ndg Owino hakusita kuwakumbusha kuwa CCM na Serikali yake inaendelea kujijenga na kuboresha taasisi zake ili kuendana na mahitaji ya kizazi na wakati uliopo na hivyo basi wanaCCM Cardiff wasioneane haya wala kuogopa kuchagua viongozi wenye sifa za kutosheka na wasio tawaliwa na tamaa na watakao zingatia miiko ya uongozi kama inavyoainishwa katika katiba ya CCM.

Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Ndg Owino alichambua na kuainisha kwa kina na kuishirikisha halaiki kufanya tathmini ya wazi ya jinsi CCM imeiongoza serikali kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ya 2005/2010 na mafanikio dhahiri yanayopatika katika kutatua kero za wananchi. Aidha alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko endelevu, kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na kwamba CCM na serikali yake inaendele kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM UK Kuwa mchango wao unathaminiwa na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na kichumi

Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi na ile ya Uchumi na Fedha walitoa machache yanayohusu idara zao na namna zinavyofanya kazi ili kuwapa mwanga wanachama wapya na viongozi katika shina hilo.

Ufunguzi huo ulifuatiwa na uchaguzi wa Viongozi mashina uliosimamiwa na Katibu wa CCM UK, Bi Mariam Mungula.

Viongozi waliochaguliwa katika shina hilo jipya la Cardiff – Wales ni;

  1. Chande Kigwalilo Mwenyekiti wa Shina

  2. Bi. Rosemary Kiputa Katibu wa Shina

  3. Prudencia Kimiti Mjumbe wa Shina

  4. Munde Nyirambo Mjumbe wa Shina

  5. Alen Mguto Mjumbe wa Shina

Mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa shina jipya la Cardiff Ndugu Chande Kigwalilo alitoa machache na kushukuru wajumbe na wanachama kumpa nafasi ya kuliongoza shina na kushukuru uongozi wa tawi kwa kufanikisha ufunguzi huo na kuwakarakibisha Jijini Cardiff.

Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi

CCM TAWI LA UNITED KINGDOM
Website: www.ccmuk.orgccmuk.org/blog, Facebook – chama cha mapinduzi uingereza, Twitter CCM UK. 

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2TFf57bxk

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment