Tuesday 28 May 2013

[wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!



   MJI MPYA WA KIGAMBONI ! SASA WANANCHI TUPO NJIA PANDA !
   Kauli ya waziri wa Ardhi Bunge inawapa mashaka wakazi wa Kigamboni,

   Mpango wa siri ya kuwafukuza wenyeji wa Dar na kuwaweka wageni ndio
   Agenda ya Wizara ya Ardhi,
   
   Watanzania sasa tuna miaka 51 ya Uhuru,lakini tupoangalia tutajikuta 
   tunaingia katika migogoro ya Ardhi na uvunjivu wa amani utakaosababishwa
   na Ardhi.
   Ni mda mchache tu huko bungeni Dodoma waziri wa ardhi Mhe.Bi Anna
  Tibaijuka ameliezea bunge kuwa nyumba takribani elfu 30 zitajengwa na 
   makampuni ya Dubai na Wachina, na wakazi wa Kigamboni watakuwa na hisa !
   Kauli hiyo ya waziri Anna Tibaijuka inawatia wasi wasi wananchi na kujiuliza
   maswali mengi kama vile kuwa na hisa katika biashara hipi? nani mmiliki wa
   Ardhi? mbona wananchi wa Kigamboni hawajapewa taarifa yoyote!
   hakuna kikako chochote kile kilicho washirikisha wananchi na kujua
   hatima yao ! mbuge wa Kigamboni Mhe.Ndugulile naye kashangazwa na

   TATIZO LA KUWAMILIKISHA ARDHI WAWEKEZAJI LITALETA UTATA,
   Wenyeji wa asili ya mikoa ya Dar-es-salaam na Pwani, wamejawa na unyonge
   na kujiona wapo katika kilio cha kusaga meno kwa kuondolewa katika sehemu
   zao za asili na kutojua wapi watapelekwa,
   Tabia za baadhi ya wajanja kumiliki mashamba makubwa nalo limekuwa ugonjwa
   ulijitokeza katika kumiliki Ardhi.
   
   UVUNJWAJI WA SHERIA ZA ARDHI
   Migogoro mingi ya Ardhi inatokana na uvunjwaji wa sheria zilizopo
   na wizara inahusika kwa namna moja au ingine katika kuvunja sheria hizo,
   Kuna Ardhi zinazomilikiwa kimila,pia na manispaa, lakini Wizara ya ardhi
   imekuwa ikiwanyang'anya wazawa na kuwapa wawekezaji wa kigeni ardhi
   hizo bila ya kuwashirikisha wahusika,wananchi,serikali za mitaa na manispaa.
   Ni juzi tu wakazi wa eneo la Tuangoma, njia panda ya Amani beach huko
   Kimbiji walijikuta wanabobolewa majumba na kulazimishwa kulipwa
  fidia la Sh.700,000 kwa heka ! na muwekezaji wa Kichina ndio kaanza
   kazi? Wanajeshi nao wanajaribu kuwatishia maisha wanye mashamba 
   ili wapate mashamba ya bure.
   Serikali ilitupia jicho tatizo la Ardhi tusije tukawa watumwa katika nchi yetu.


0 comments:

Post a Comment