Tuesday 7 May 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: Ya Arusha Na Kamba Inapokatikia...

Deo, 
Awe ametoka uarabuni au china....ni gaidi tu....
Kwa sasa sio busara kusema kwa hakika kwamba hao wasaudi wanahusika ama la....na kuhusika sio kuleta bomu tu....hata kuwezesha utengenezaji!


2013/5/7 Deogratius J. Koyanga <deokoyanga@gmail.com>
kaka Mjengwa, hakuna tukio la ugaidi Tanzania, bomu gani la kigaidi lile? tutafakari hata uwezo wa bomu lenyewe tusipotoshe jamii. Mtu atoke uarabuni hadi Tanzania kuja kurusha Bomu ambalo haliwezi hata kudhuru watu 10?  mimi ninaamini walioliterngeneza bomu na kulirusha ni watanzania wenzetu na wapoa hapa hapa tusiwasingize waarabu. tunapotoshwa sana na kusukumwa na hoja za wazungu kuaminishwa kuwa kila mwarabu ni ghaidi. kila  mlipuko umetoka uarabuni. ni upotoshaji huo.

Tumsake mchawi wetu hapa nyumbani na tukomeshe huu unyama.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
"Ufalme wa Mungu umekaribia, Tubuni na kuiamini Injili..."Mark 1:15


2013/5/7 Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>


 

Ndugu zangu,

 

HAYA ni moja ya maandiko yangu muhimu katika  kazi yangu ya uandishi na uelimishaji jamii.

 Ni kwa kutambua ukweli, kuwa nchi yetu imepatwa na shambulizi la kigaidi. Imetokea Arusha, ingeweza kutokea popote pale katika ardhi ya nchi yetu. Tunawapa pole wahanga wa tukio hili. Ni msiba wetu sote.  Tuwe sasa na mioyo ya ustahamilivu.  Tusikimbile kunyosheana vidole. Tuwaache tuliowapa dhamana ya kuchunguza waifanye kazi yao. Wajibu wetu wa kizalendo ni kutoa ushirikiano.

 

Naam, kama nchi, tunapitia sasa kwenye kipindi cha majaribu makubwa. Huu ni wakati wa kuizunguka bendera yetu ya taifa. Ni wakati wa kuonyesha umoja, uzalendo  na mshikamano wetu kama taifa. Umoja, uzalendo  na mshikamano wetu ni silaha muhimu na kubwa kabisa Watanzania tumeendelea kuimiliki tangu enzi na enzi. Ndio silaha tunayoendelea kuimiliki hadi sasa. Tuna lazima ya kupambana hadi risasi ya mwisho kuhakikisha adui hatupokonyi silaha hii.

 

Ndugu zangu,

 

Hii ni Nchi Yetu. Ni nchi yetu sote, Watanzania wa imani zote. Tutambue sasa, kuwa kwenye safari tunayokwenda kama taifa, mbele yetu kuna  mawimbi makubwa. Kwa pamoja tutavuka, kwa kugawanyika tutazama.

Wahenga wetu walisema; kamba hukatikia pabovu. Watanzania wa imani tofauti tuna historia ya kuchanganyika na kuishi kwa amani na upendo. Hatuna hulka ya kubaguana. Tukianza sasa dhambi ya kubaguana, basi, itaendelea kututafuna.

Na siku zote, uzoefu ni mwalimu mzuri . Mathalan, uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto,  ni kazi ngumu sana.

Ona, moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza kijiji kizima. Na tangu utotoni tumetahadharishwa hatari ya kucheza na moto.

Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.

Na ningependa hapa  tuyakumbuke maneno ya busara na hekima nyingi kutoka kwa Bi. Joy Mukanyange ( Pichani). Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa Rwanda nchini Tanzania. Mama huyu aliyatamka maneno haya miaka 13 iliyopita, takribani miezi sita kabla ya kifo cha Baba wa Taifa. Bi. Joy Mukanyange alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona. Ni kama vile alikuwa mtabiri, maana, alichokisema mama yule leo ndio tunaanza kukiona. Siku ile ya Aprili 6, 1999, katika iliyokuwa Kilimanjaro Hotel, Bi Joy Mukanyanga aliyatamka haya;

 " Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha maauji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994." Alisema Balozi yule wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ndio, Bi Joy Mukanyange alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona.

 

Na tutafanya makosa makubwa, kama hata sasa, tutajifanya kuwa hatukioni kile ambacho Balozi Joy Mukanyange alikiona . Watanzania tukubali sasa kuwa tumepatwa na bahati mbaya sana ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini.

 Hili ni jambo la hatari sana. Ni hulka ya mwanadamu, anapokuwa matatizoni kumtafuta kondoo wa kafara. Mtu mwingine wa kummyooshea kidole kwa matatizo yake. Hali duni ya uchumi wa nchi, hali duni za maisha na umasikini wa watu wetu isiwe chachu ya kuanzisha vurugu za kijamii.

Maana, taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwapo na WAO.

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la wengi wetu kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi, ufahamu mdogo wa historia yetu. Hivyo basi, kupelekea hali ya kutojitambua kama taifa.

Ndio, uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana. Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda. Historia ni kama maji ya mto, yakipita hayarudi. Historia ni wakati, ni muda. Kihistoria jana ni sawa na zamani.

Karne nyingi zilizopita wahenga wetu walitafsiri muda kama mkusanyiko wa matukio ya zamani na sasa. Waliamini kuwa yaliyotokea zamani na yanayotokea sasa ndiyo yenye kusaidia kubashiri yatakayotea kesho, yataamua mustakabali wetu.

 Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa. Tuliopata bahati ya kutumia kalamu zetu hatuna budi kuliweka hili hadharani. Ni wajibu wetu wa kizalendo.

Narudia, Hii ni Nchi Yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu ambao hawana nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda heshima na hadhi ya nchi yetu. Mengine yanayofanyika sasa sio tu yanaitia doa nchi yetu, bali, yanaiaibisha nchi yetu.

 Ndugu zangu,

Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya dini, ukabila na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe. Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz.

 Na dini hizi za kimapokeo zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na kuzikuta dini zetu za asili, na bado tunazo. Na hakika, Afrika hatugombanii matambiko. Afrika kila ukoo una tambiko lake, hivyo basi, dini yake. Kamwe hutasikia Waafrika wanagombania matambiko. Hutasikia Waafrika wakigombana kwa tofauti za matambiko yao.

 

Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.

Naam; kamba hukatikia pabovu. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania.  Nahitimisha.

Maggid Mjengwa,

Msamvu, Morogoro.

0754 678 252, http://mjengwablog.co.tz

 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 



--

Martin Mkenda


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment