Sunday 19 May 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu....

Lema alipojaribu kutuliza vurugu za chuo cha uhasibu harusha nini
kilimtokea? Huwezi kuzungumza na wahuni wa serikali kama una akili
timamu. Ukombozi wa nchi hii hutakuja kwa mazungumzo ya kuhailisha
matatizo

On 5/19/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Kinachotokea Iringa, tafsiri yangu…
>
>
>
> Ndugu zangu,
>
>
>
> Leo saa mbili na nusu asubuhi nilifika Jengo la NSSF nikitokea kufanya
> jogging yangu ya asubuhi. Nilifika hapo kuwahi kununua magazeti.
>
>
>
> Hali ilikuwa shwari kama ilivyo kawaida ya Iringa Jumapili asubuhi. Kunako
> saa tatu asubuhi nilipokuwa nyumbani nikisoma magazeti, ndipo niliposikia
> mlio wa kwanza wa bomu la machozi. Idadi yake ikaanza kuongezeka.
>
>
>
> Nikiwa na kamera yangu nikajisogeza hadi katikati ya mji kufahamu zaidi
> kinachotokea. Nilichokiona ni vurugu kati ya Wamachinga na Jeshi la
> Polisi.
>
>
>
> Tatizo?
>
>
>
> Ni dogo sana, lakini linakuzwa kwa vile siasa imepelekwa mbele badala ya
> kutanguliza hekima na busara. Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya
> biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge
> wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa
> kwa
> kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge
> wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya
> Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio
> siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha
> matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi.
>
>
>
> Kinachotokea Iringa kwa sasa ni doa kubwa kwa mji wetu wenye sifa ya muda
> mrefu ya utulivu. Kina athari kubwa kiuchumi pia. Pale Iringa mjini
> nilichokiona leo ni kama mji ulio katika mapigano ya kivita. Watu ni
> wachache na wenye hofu.
>
>
>
> Biashara nyingi zimesimama. Niliziona Daladala zikitoka Kituo cha Miyomboni
> bila hata abiria, watoke wapi? Wakati kwa sasa walio nje ya mji wameambiwa
> na jamaa zao walio katikati ya mji kuwa wasijaribu kufika mjini, kwamba
> hali imechafuka.
>
>
>
> Nimeongea na mwuza nyama ya bucha aliyeniambia kuwa mgomo wa Daladala wa
> hivi karibuni ulimfanya apate hasara kubwa kwenye biashara yake ya nyama
> kwa vile wateja wake wengi wanatoka nje ya mji. Na anachokiona leo ni
> hasara nyingine kwa vile hakutakuwa na biashara nzuri. Je, ni
> wafanyabiashara wangapi watakaoathirika na hali hii ya leo?
>
>
>
> Na kwa kuwa mkweli, kisiasa kinachotokea Iringa kwa sasa kinaweza kuwa na
> athari hasi kwa Mchungaji Msigwa badala ya kumjenga kisiasa, kwani, wengi
> niliozungumza nao katikati ya mji wanamwona Mchungaji Msigwa kuwa ni mtu
> ambaye angeweza kuiepusha hali hii kama asingeyatumia majukwaa ya siasa
> kuwahamasisha Wamachinga kuendelea kufanya biashara, na hivyo, kutokutii
> amri ya Manispaa.
>
>
>
> Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu.
> Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye
> Harambee pale Tumaini University.
>
>
>
> Kama Mchungaji Msigwa angejibu simu yangu, basi, ningemwambia haya
> ninayoyaandika hapa.
>
>
>
> Maggid Mjengwa,
>
> Iringa.
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment