Monday 20 May 2013

[wanabidii] RAIS JAKAYA KIKWETE : MNAOTAKA URAIS MSIKIVURUGE CHAMA

MWENYEKITI wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete amefungua milango kwa
kuwataka baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowania URAIS mwaka
2015 kuendelea na mchakato huo.

Rais Kikwete amewatahadharisha watu hao kuendesha kampeni zao kwa
ustaarabu pasipo kuibua chuki wala kujenga makundi ambayo alisema ni
hatari kwa kuwa yanaweza kukipasua Chama. Rais aliyasema hayo katika
mkutano wa ndani wa wabunge wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi
wa CCM (WHITE HOUSE) mkoani Dodoma.

"Tuangalie makundi ya URAIS 2015 yasishambuliane kwa kuvunja Chama,
wenye nia hiyo ya kugombea waendelee na mikakati yao bila kujenga
chuki kwa makundi mengine.

"Katika hatua hiyo pia mkumbuke kuwa katika kambi hizo za URAIS
zinatakiwa kujitazama wao na wafuasi wao maana wafuasi wengine
hawaaminiki", alisema Rais Kikwete..

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment