Monday 13 May 2013

[wanabidii] Mkutano Mkuu wa OIC kufanyika Zanzibar

CHUO Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA kinatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani OIC ambao utafanyika Septemba 2, mwaka huu. Mkutano huo wa kimataifa utafanyika Zanzibar kwa mashirikiano ya Nchi ya Omani, Umoja wa OIC na Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA.

Taarifa hiyo imekuja kupitia Ziara ya siku nne ya Maafisa wa Nchi ya Omani walioambatana na Maafisa wa Jumuiya ya OIC iliyoanza leo mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kumbumbuku na Nyaraka ya Nchi ya Oman Dkt. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy amesema Zanzibar imepata nafasi hiyo kutokana na kuwa na Mahusiano mema na Nchi nyingi ulimwenguni na hasa katika nchi za kiarabu.

Amesema Historia na Utamaduni wa Kiislamu wa Zanzibar na namna ulivyotumika katika kusambaza Uislamu Nchi nyingine umekuwa kigezo muhimu cha Zanzibar kupata nafasi hiyo.

"Kwa vile Zanzibar ina historia nzuri katika kusambaza Uislamu nchi nyingine tunaimani kuwa hata malengo ya Mkutano wetu huo yatafikiwa kwa kiasi kikubwa " Alisema Dkt. Al Dhawiyaniy ambaye pia ni Mkuu wa Msafara huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa OIC katika Kitengo cha Utafiti na Utamaduni Dkt. Halit Eren amesema Mkutano huo utakuwa fursa adhimu kwa Zanzibar kujitangaza katika mataifa mbalimbali na kuendelea kujiongezea umaarufu Kimataifa.

Amesema kwa vile Watakuja Washiriki kutoka Mataifa mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya OIC, Zanzibar itakuwa ni nafasi yake muhimu kufahamika kimataifa na kujipatia nafasi za masomo Duniani.

Amefahamisha kuwa Watoa Mada 164 kutoka Nchi mbalimbali tayari wameshapeleka maombi yao ili kuwasilisha katika Mkutano huo na kuwataka Wazanzibari nao kupeleka Maombi yao.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha SUZA Dkt. Haji Mwevura Haji amesema Vyuo mbalimbali kutoka nchi tofauti viliomba kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo lakini Chuo cha SUZA kimeamuliwa kuwa Mwenyeji kutokana na historia ya Zanzibar.

Amefahamisha kuwa licha ya Zanzibar kutokuwa Mwanachama wa Jumuiya ya OIC lakini kigezo hicho hakiizuii Zanzibar kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo wa Kimataifa.
Amegusia kuwa Mkutano huo unaweza kuwa fursa Adhimu kwa Zanzibar kunufaika kupitia Jumuiya hiyo kama ambavyo Nchi ya Uganda ilifaidika kwa kujengewa Chuo Kikuu cha Mbale.

"Wenzetu Uganda walifaidika na OIC kwa kujengewa Mbale University nasi pia tuna matarajio mengi ilikwemo kuitangaza SUZA na kupata Scholarships duniani" Alisema Dkt. Haji

Dkt Haji amewahakikishia Maofisa hao ushirikiano wa kutosha ili Mkutano huo uweze kutimiza malengo yaliyopangwa.Umoja wa Nchi za Kiislam Duniani OIC unajishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemo kusaidia Nchi wanachama wa Umoja huo katika huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa Taasisi za Kielimu, Afya na Miundombinu ambapo Mkutano mkuu uliopita ulifanyika Nchini Omani.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment