Sunday 12 May 2013

[wanabidii] Hofu Ya Ugaidi ( 04)

Na Maggid Mjengwa,

LEO tuangazie kwa karibu kwenye ugaidi wa Kipalestina, maana, tumeshajadili ugaidi wa Kiyahudi. Na juzi hapa tuliangalia ushiriki wa Jenerali Idd Amin katika Ugaidi wa Kimataifa. Na hoja ya Idd Amin katika kuunga mkono ugaidi ilikuwa ni kuonyesha mshikamano kwenye suala la Wapalestina.

Katika kuungalia mgogoro wa Wapalestina na Waisrael na tuangalie kwa karibu harakati za mapambano ya Wapalestina dhidi ya dola ya Israel. Bado tuna kumbukumbu, kuwa chama cha Hamas kimeshinda uchaguzi wa bunge katika uchaguzi uliofanyika katika Palestina miaka michache iliyopita. Hivyo basi, Hamas kimepewa nafasi ya kuunda serikali.

Mara tu baada ya ushindi wa Hamas, Israel ilitamka wazi, kuwa haitashirikiana na Hamas kwa lolote lile . Ni kwa vile Hamas ni chama cha kigaidi, vivyo hivyo Marekani na Umoja wa nchi za Ulaya zilionyesha kutoiunga mkono Hamas. Chama hicho kinashutumiwa pia na taasisi za Umoja wa Mataifa zenye kuhusika na haki za kibinadamu kama vile
Amnesty International na Human Right Watch.

Hamas, jina la chama hicho ni neno la Kiarabu lenye maana ya hamasa au enye kutia hamasa. Bila shaka yeyote, Hamas kama lilivyo jina lake, .... Soma zaidi...http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/2667-hofu-ya-ugaidi-04.html#addcomments

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment