Friday 17 May 2013

[wanabidii] HALI YA MTWARA 17/05/2013

Ndg wanabidii
Niwajuze walao kwa kifupi hali ya Manispaa ya Mtwara leo. Ni kwamba Mtwara kumekuwa kama kumekumbwa na msiba mkubwa sana. Hakuna duka lililofunguliwa, hakuna mabasi wala boda boda kusafirisha abaria. Sokoni nako kulinuna kabisa. Meza zilifunikwa maturubali au masalfeti yaliyounganishwa. Kijumla Mtwara leo kumenuna.

Sababu yake ni kwamba; ilijulikana kwa wengi kuwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itasomwa leo. Na kulikuwa na vipeperushi vilivyohimiza watu kusikiliza kwa makini. Na kama habari ya Gas Mtwara haitaeleweka tuanze vitu vyetu. 

Hali hiyo ilizua hofu kwa watu wote na ndiyo maana Mtwara leo kumenuna. 

nawakilisha.

0 comments:

Post a Comment