Monday 27 May 2013

Re: [wanabidii] Wajibu wa kuleta amani

Dada Anna
 
Umenifurahisha sana kwa hii "makala" yako. Kwa bahati mbaya name si mwandishi wa habari ila ni mpenzi wa kusoma makala za waandishi habari mbalimbali hasa ndugu yangu Majjid Mjengwa. Hii uliyoandika hapa nafikiri si makala bali ni ripoti. Ulikuwa  unajaribu kuripoti kile ulichokiona ama kilichokuwa kikitokea. Good starting point. Naamini wataalamu akina Mjengwa, Muhingo na wengineo watakufundisha na utahitimu your online learning.
 
Salum
Kalgoorlie
WA

From: anna nyanga <luguanna@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, May 26, 2013 10:05 PM
Subject: [wanabidii] Wajibu wa kuleta amani

Mimi sio mwanahabari, nataka nijifunze fani hii leo kwa kuwaletea makala yangu ya kwanza:
 
Jana katika miji ipatayo 330 duniani kulikuwa na matembezi (march) ya kupinga jitihada za kampuni moja inayoitwa Monsanto.
.
Haya matembezi yalilenga kupinga jitihada za kampuni ya Monsanto na washirika wake.  Kuhusu matumizi ya mimea ambayo chembe hai zake zimefanyiwa marekebisho (genetical modification).  Kwenye mji ambao naeleza kusanyiko hili, mkusanyiko umefanyika kwenye eneo moja wapo la chuo kikuu cha kilimo.  Wadau wanafikilia kuwa kampuni hizi zinawafanya watafiti wa chuo kikuu cha kilimo kufuata matakwa ya makampuni na sio utafiti huru. Karibu na chuo hiko kuna makampuni ambayo yanashilikiana na Monsanto na kuona kuwa tatizo la njaa hapa duniani litamalizwa na technologia ya kufanya marekebisho ya chembe hai za mimea yaani (Biotechnology)!!.
 
Wadau , wanaona kuwa kampuni inaondoa haki ya walaji, wakulima na sekita ya kilimo kwa ujumla. Hayo ni maono yao.
 Hapa kuna pande mbili moja inaona umuhimu wa technolojia hii na upand mwingine unaona madhara zaidi.
 
Mji mzima wenye hilo tukio, umejaa skari polisi ambao walionekana kabisa wapo tayari kivita. Kwa wale ambao mlipitia JKT kivita (field battle). Pale eneo la tukio kulikiwa na askari kama 30 hivi, na kila mita kama kumi hivi kulikuwa na askari wa msaada watano na gari.
 
Kwa gharama hii ya kuwaleta askari wengi hivi eneo la tukio, sidhanai kama serikali inafurahia. Lakini ili kuleta amani, kuwapa faraja watu wake imetoa ulinzi ili waeleze walichonacho moyoni. Na polisi wamefanya wajibu wao, kuweka amani mahala pale.
 
Ili kuleta amani ambayo inataka kupotea nchini, watoa huduma inabidi kuangalia namna gani tunaweza kuileta amani. Kama tutafikia hatua ya kukubali tunapokosea, uneweza ukawa mwanzo mzuri wa kuleta amani. Amani haiwezi kuja yenyewe, amani inatafutwa na kulindwa.
 
Mwanahabari mwanafunzi
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment