Yaani Lucas Haule Kisacha kalikosea tena jina langu anaita 'ganda' badala ya 'garda.' apelekwe Mtwara huyu akale mkong'oto. Taarifa mbaya: Wanakijiji wa wilayani Bunda wameua wanawake 3 na kuchoma nyumba zao 4 huko bunda kwa kisingizio cha uchawi (ITV taarifa ya habari saa 2 usiku jumapili). Mganga wa kienyeji kawaambia wamemuua kijana aliyepata ajali ya pikipiki na kuwa wamemuweka ndondocha ndani ya nyumba yao. Hawa wameua makusudi na kuharibu mali. Lakini risasi ikifyatuka katika kujilinda na mishale na mikuki-Serikali haina haki za binandamu.Ukipitishwa msako wa manyaunyau wa kutambua wachawi au kupiga ramli na wananchi wakachoma majumba, mashamba na kuchoma washukiwa-hatulindwi? Serikali hailindi raia. Utamjuaje anayepanga njama kati ya familia na familia na wanakaya au kijiji kushiriki kisiri kisha kutoroka au kula jiwe kujificha wasitajane? Pengine ni wivu wa maendeleo tu ya hiyo familia ya wanawake 3 tupi mama na wanawe wameamua kuidhulumu uhai. Hawa waganga lambalamba ndio wanatakiwa na Baraza la Tiba Asili la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Association of Traditional Medicine (ATME) na vyama vingine vya Tiba Asilia na Tiba Mbadala vya Tanzania na Barala la Utamaduni wawashughulikie. Wote mganga na wateja wake washitakiwe kifo kwa kuua labda ndio wataacha kusababisha mauaji. --- On Fri, 24/5/13, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment