Friday 24 May 2013

Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

My Dada,

Watu huvutiwa  zaidi kusoma hbr fupifupi ... unapoint ila story ndefu mno... hata mimi nilikuwa kama wewe zamani ila nimeona faida za kufupisha
 
Regards,
Mugittu, Zephaniah,
Cell: +255 784 769 481
Fax2Email: 0736605633
Skype: Zephaniah N.N. Mugittu
 
No matter how high one is talented , business acumen still a necessity
"Poverty is a result of attitude ..."
 
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, 24 May 2013, 5:56
Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

Matanda-wala usijali mimi kuitwa kaka. kuna akina mama warembo lakini ni bisexual wamezaliwa hivyo biologically au ni transgender psychologically. Mwache tu aite atakavyo, unaweza ukamuona mtu kavaa gauni au suruali kumbe-kanyaboya. Ni juzi tu mama bisexual huko china amepata haki yake ya kuolewa. Amefanikiwa kufanyiwa operesheni kuondoa umbile la pili na mchumba kamvisha pete. Hapa Tanzania wanaozaliwa hivyo wapo wengi, hawana msaada, wazazi waliwaficha hivyo hawakufanyiwa upasuaji. Wanateseka na kunyanyasika sana mopaka kubakwa ili kushikishwa adabu eti wajiune na kujitambua kuwa wao ni She sio He.
Wapo walioa na kuzalisha naye akiamua anazaa wake. Yaani una watoto mtu kakuzalia halafu nawe una wako umezaa mwenyewe. Bahati ilioje!! Nione ninguunganishe nao uongee nao.

Ila unaweza pia kwenda Google kusoma habari za saint wa jina hilo ukaiona na ukaipata.

Kuchangia ya Mtwara

Ninapenda kuchangia kuwa-nadharia ya education inasema kumuelimisha mtu haimaanishi atafanya ipasavyo. Elimu na kuelimika kukuza ufahamu kuhusu jambo ni muhimu lakini sio mwisho wa tatizo. Umuhimu ni yule anaye elimishwa kubadilika positively kufanya inavyotakiwa. Na ndio maana unaelimisha watu na wanayaona matokeo unayoyasema lakini bado wanafanya watakavyo wao kutokana na mambo mengi-kutokuelimika ndani ya ubongo wao kwa kukubali kwa dhati usemayo; imani potofu iliyojengeka hata usemeje, ushauri wa wengineo (peer influence, wazazi, wazee wa mila, mwenza, ndugu); mila na imani zake na desturi; hali ya kijiologia, sera, upatikanaji/access; livelihoods survival strategies na mengineyo mengi kama sababu. Hivyo baada ya elimu-utekelezaji kuyafikia yasemwayo ni muhimu.Mbinu za uelimishaji na kufikia walengwa directly ni muhimu ili kuepuka matatizo ya mawasiliano ktk kufikisha ujumbe : yaani UJUMBE-njia ya mawasiliano-nani anawasilisha mawasiliano ujumbe....vikwazo...- mpokeaji ujumbe-mrejesho kuwa umefika na umeeleweka.

Juzi tu kuna gazeti moja nchini limeandika kuhusu kabila moja huko kusini na masuala ya ngoma za jadi za kumcheza mwali wa kike na kufundisha vitoto mambo ya kikubwa ya ndoa au kujamiiana na jinsi inavyoathiri elimu. Ikatoa takwimu za utoro shuleni na mimba na idadi waliofaulu na ambao hawakufika sekondari. Na hii elimu ndio ufunguo, inapigiwa kelele kila mara mpaka kuanzisha shule ya vidudu ktk kila shule ya msingi na kuanzisha sekondari za kata pamoja na matatizo yake au ya shule hizo. Je, kwani wazazi hawajui hilo? Mbona hawaandamani wakajichoma wenyewe kwa kukiuka sera nzuri ya serikali ya maendeleo yao wenyewe?

Nilitolea mfano hapa wa mradi sio Mtwara ila Lindi vijijini jinsi tulivyokuwa tunakaa na kupanga pamoja na kukubaliana. mzee mmoja na mwenzake wakatoa ardhi ekari mia nilisha kuzitaja humu mtandaoni kujengwe hiyo shule ya chekechea baadae ije ijengwe primary school watoto wapate elimu. Funded 100 na familia ya marekani wao wagharimie vinginevyo. Wilaya iliahidi kutoa na kugharimia mwalimu. tukakubaliana waanze kulima shamba la shule (ekari 4 hivi), kuuza mazao kuweka hela bank mpaka hapo shule itakapokamilika watakuwa na hela za madeski, mikeka, vikombe vya uji hela ya kulipa mlinzi na mpishi. 'Hela za nauli kwenda kufungua akaunti Lindi Mjini  hatuna, ya akaunti na kupiga picha hatuna; hatutaki viongozi wa kamati ya ujenzi wa shule ya msingi watakula hela' ....Sawa-Ninatoa hela yangu hii hapa mbele ya umma (85,000/= posho ya siku moja) mkafanye tunalojadili, nauli, picha, akiba ya kufungua akaunti. Kisha nikanunua mbegu husika DSM, peleka kupitia mabasi ya Lindi (Sio Mtwara) kusaidia vikundi 2 vya vijana, shule 2 za msingi na hiyo ya chekekea. Shule ya Chekechea kamati ya ujenzi ya kusimamia pia kilimo na mengineyo walioichagua wenyewe--HAIKULIMA. Yakaja maneno mapya. Sio kukataa kamati ya SYMsingi tena.....Tunangojea kwanza shule Ijengwe Ikamilike na mengine mengi ya kutia mtu mwenye nia njema wazimu. Shule imekamilika baana ya mwaka, mkandarasi kaikamilisha ipasavyo-hawakulima, akaunti haina hela, malumbano....

Hapa huyu aelimishwe nini na anaona wasiosoma wanavyokosa ajira au hawajui kusoma na kuandika kama alivyo yeye mzazi hajui hata kusoma kiswahili wenzake wanajua. Anayeoza na kuoa kichanga-haoni matokeo yake. anyway, kasichana kakipata Fistula ataoa mwingine.

Umempeleka mtu study tour ambayo husaidia sana ufahamu. inategemea nani kapelekwa, labda wale wasio wa sekta hiyo na wana mahitaji mengine-kupanda ndege, shopping. Kajichagua au kaenda sio Mtarajiwa karudi ...ana mambo yake. Au, kaenda aliyetegemewa lakini amerudi umemuwezesha aweze kutembea kwa walengwa wa mafao ya GAS awafahamishe ipasavyo? hata usafiri wa kutembea vijijini kila kijiji, au kuitisha vikao vya kata na vijiji. Vijiji vingine ni mbali na makao ya Kata watataka kurudishiwa nauli kwa vile kawaita yeye. Anazo hela na usafiri? Hata kama tatizo si nauli-akiwaita wakaja jee watakayoambiwa hawatayageuza (matatizo katika communication of information). naye aliyeona huko Trinidad na Tobago au Ukraine-atasema alichokiona positively? ana uelewa wa kuwakilisha alichoona bila kupaka mafuta na kukigeuza? Muda wa elimu hiyo na matokeo ya ujenzi. Jee waliohudhuria maelezo ni hao ambao wanaandamana? au waliohudhuria ni wazee, vijana hawakuwepo ndio hao wanaandamana maana hawaendaki ktk vikao vya vijiji. au wote wamepata maelezo ya kuelimishwa lakini kama tulivyo waswahili-kuongeza chumvi na kubadili ukweli, matokeo ni vurugu, kutumia baruti za kuvulia samaki na kubomoa madaraja, kukata miti ya umeme ili umeme wa kutoka Kidatu kwa Wavidunda usiingie Mtwara na ktk majumba ya Waheshimiwa viongozi na wengineo. Nao madreva wa magari ya polisi wakija-tunaweka kivumba, barabara asiione auone shimo aanguke wafe askari wote watakaoletwa Ntwara (Tumesikia mitandaoni dreva kasema aliona bahari sio njia!!). Ni kama ile vita ya risasi kugeuka maji na hivi sasa dreva njia aione haipo, akiona kundi la watu askari aone ni tembo akimbie mwenyewe!!

SERIKALI YA TZ ina muongozo wa kuangalia athari za mradi na jinsi ya kuwafaidisha walengwa. na hii hufanyika chini ya NEMC na Wizara husika hushiriki kikamilifu. Wakitoa tender kampuni ya nje inayobid lazima iwe na kampuni mwenza au taasisi yenye wataalamu hapa nchini. Hawa wanakwenda kufanya studiez zote na kupanga mpango wa kufaidika na wa kuondoa madhara ya mradi (mitigation measures). Report mbali mbali huandikwa na kuwakilishwa serikalini na donor wa mradi kama yupo au GVT tu. taarifa huandikwa kiswahili na kuthibitishwa na wananchi wakatoa michango yao ktk taarifa hiyo ya mapendekezo kabla ya kuwakilishwa. Wananchi hifikiwa kwa vijiji, vitongoji vya mbali, kata; wazee wa mila na wazee maarufu ke na me kushirikishwa, watumishi wa ugani, masirika binafsi na NGO/CBO zilizopo; vikundi vya wazalisha maji; tourist hotels/companies. yani walengwa ni waliopo eneo hilo na sekta zilizopo formal-informal. kikao cha mwisho kila kundi hupeleka mwakilishi kusikiliza. Kunakuwa na public hearing kieneo vijijini wanafuata mikutano ya hadhara na kuambiwa kisha kukaa vikundi kuandika na walichoandika hutunzwa. wakawakilisha na kuchangia vikundi vyote vilivyopo wake kwa waume, vijana na wazee.

Msidanganywe na hearsay, kazi hufanyika, isaidieni serikali na jamii kufanya vya maendeleo sio uharibifu. Unaweza ukasema-HAWANA AKILI kama ikiwa, baada ya kufanya yote ya kuwashirikisha na kuwaelimisha-wanafanya haya wayafanyayo.
Au, waliahidiwa vikao, vikaitwa hawakuja wakagoma, sasa wanaharibu hawataki majadiliano.Hawaambiliki na kushaurika-wanaona wanavyoharibu ila wanafanya tu kutaka misifa. Kama inawezekana. Huo mradi uachwe usimamishwe kionekane. Mbona mafuta yapo mengi sana nchini na mafuta hufuatana na GAS. kuna minara mingi ya mafuta toka Ukoloni na hapo Gas haikosi. Huko nyuma, nilitoa mfano wa Mafia Island na milingoti mingi nchini ambapo imefutika maandishi tunadhania ni mnara wa mipaka au bomba la zambia na mingine tunabomoa tunachukua kokoto na nondo. Tunadhania ni mnara wa kuonyesha madini fulani yapo kumbe ni wa mafuta ya ardhini. Nikaweka minara ya Mafia ambayo watafiti tulikuwa hatuijui ila kasichana toka uingereza kilipewa grid reference na baba yake tukaisaka 9bila kibali cha serikali) tukaipiga picha maana baba yake alitaka ajulishwe kama wameanza watanzania kuchimba mafuta au la. lakini utafiti wa Gas ukiendelea mafia 2008 na ipo nyingi kichizi. Angalia kiambata upate kuona jinsi watumishi wa mshahara mdogo wa GVT yako wanavyoteseka maporini, baharini ktk kutekeleza kukusanya mawazo ya wananchi katika miradi mbali mbali. Huu wa kiambata ni mradi wa International airport wa kusaidia usafiri (ambao ni tatizo Mafia) na wa kukusa utalii. Huu utaunganisha utalii ZNZ, Mafia, Arusha, Kilwa, Mtwara-Mikindani. Hivyo sio Mafia tu kulitembelewa ni Mpaka Rufiji-Nyamisati Kilwa Kisiwani-Mikindani-Mtwara. Mafia ni visiwa saba vinavyokalika vyote vilitembelewa na walishiriki kikamilifu. Ila, tishio la kuhusisha watu kidemokrasia ni wale wasioitaka ili wavune mazao (kuvua ndani na Marine Park, kuvuna Mikoko na kuuza mbao na milingoto Uarabuni) ambao walipokuwa wakiondolewa wakaingiza UDINI mabomu  ya petroli yakaruka kupambana na askari wa doria wa Marine Park, Idara ya uvuvi na mali asili. watafiti tukiwa chambo ktk shughuli isiyohusu hayo yao lakini tungekufa.

--- On Thu, 23/5/13, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 23 May, 2013, 12:23

Hildegarda ni mrembo wa nguvu wewe Lucas.

2013/5/23 lucas haule <kisacha2003@yahoo.com>
Hildegarda, kaka
Tatizo siyo yote unayoyasema, tatzo ni Wanamtwara wangapi walielimishwa kuhusu gesi hiyo? Na kauli ya siku za mapema za mkuu wa mkoa alisema wale hawana akili. Wananchi wakamwambia Pinda nenda na huyu alitutukana, serikali ilifanya nini? Tuna angaika kusema tutadharauliwa, watadharauliwa walioshindwa kuona mpaka wakigawiwa maumivu.
Kama unaipenda nchi wakemee wote ambao huwa wanawabeza watoa taadhari na kuionya serikali kabla ya hatari.
Naumizwa na kuumia kwa watu, vifo lakini njia waliyochukua wananchi, siwalaumu na nailaumu serikali kwa kuzembea.

--- On Thu, 5/23/13, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>

Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, May 23, 2013, 4:35 AM

Tunahitaji watu kama wewe Rwebangila, wenye mawazo chanya.

Enyi watanzania, tunajiaibisha na kudhalilisha utu wetu kimataifa.
Tumekuwa wepesi sasa kuchukua sheria mkononi kuharibu kabla ya kusubiri sheria au mazungunzo/majadiliano. Hii ni mbaya sana sana. Tunaonekama watu wa ajabu.  Ni gharama kwa taifa sote tukemee na tunawajibu kuyazuia yasiendelee.
Haisaidii kabisa kama usemavyo kushabikia mauaji, uharibifu wa miundo mbinu na kuonea wengine. Jee, wewe unayeshabikia uchafuzi huo huko na vurugu ndio njia ya haki ukiwa wewe ndio kiongozimadarakani utaruhusu haya yaendelee hutokataza ukizingatia haki za binadamu?

Kama ni umasikini kote TZ upo. Unaweza kushuhudia vijijini mwetu mtu ana mifugo ya ng'ombe wengi, mbuzi kibao, kondoo, kuku ambao kwa sasa almasi na analima mahindi, pamba lakini nyumba yake ya kimasikini pamoja na mifugo yote na kilimo. Wake zaidi ya wane, watoto 50, tegemezi ya ndugu waliokosa elimu kibao. Wake na watoto kila mmoja analima na kuuza pamba; pombe, maziwa na anapata mifugo kwa kuoza visichana lakini watoto hawasomeshwi. Anavuna madini Mererani-analimbikiza mifugo aonekane tajiri sio kuwekeza kwingine ni wachache sana. Janguo la minazi kauza nazi malori-anatoa mwali kwa gharama hela zinaangamia. Anataka sifa ya ngoma. Anaweza akaja mtu kutoka mbali akagonga kokoto pamoja na wenyeji akauza akajenga kibanda kizuri na akafungua duka mara ana mgahawa, inafika hotel mara ana bajaji na daladala. Yeye yupo hapo kabweteka.

Maendeleo ni mipango na unafanya nini maishani. Umasikini lawama haiwi upande mmoja tu kwani utajiri haushuki kama mvua. Daima sababu ni nyingi na si upande mmoja tu nasi wenyewe tumo.

Kwa sasa imekuwa kama tabia ya kuchoma na kuharibu. Anashukiwa uchawi-choma nyumba, ua. Wakati mwingine si kweli kuwa mchawi ila ni wivu wa maendeleo yake lakini sheria haitumiwi.

Ni hivi pia mashamba ya wawekezaji na mali zao na ya wakulima wengine walioomba na kupewa ardhi kisheria wakaomba mikopo na kuanza kilimo kikubwa kuharibiwa. Kuharibiana mali magomvi ya viwanja. Unaona ktk TV kubomolewa  nyumba zenye kesi mahakamani tena ya vizee mtu anatumia mabaunza kubomoa kwa vile ana hela huenda na za kuhoga.

Wanagombea sehemu ya malisho lakini walijenga na kuchangia sekondari ya kata au shule ya msingi ya kitongoji-inabomolewa ktk kijiji hicho hicho eti ipo eneo la malisho. Shule ya kijiji chao, wamejenga wenyewe ila kuna wachache wakorofi huvunja usiku. Michango na gharama zote kwisha. Tupo kuchangia  umasikini sio ubinafsi. Na ndio maana mh Nyerere alikuacha Butiama kama kulivyo kukajengeka kwa misaada baada ya kifo chake. Daima utajiri wa mifugo na madini Mwanza, Geita, Mwadui, Mwadui ulitumika kitaifa.

Fikiria ingekuwa nyumba ya mzazi wako uliyomjengea ndio imebomolewa kwa vile yeye ni mzee wa Baraza la sheria kata au Mahakamani. Itakugharimu kiasi gani kuanza kujenga upya na wao walimchagua wenyewe awe ktk baraza. Je, kesho unayeshabikia Chama chako kikishika madaraka utaruhusu uhuru wa namna hii wa uharibifu.

Jee ile ya Songosongo tunayotumia DSM na kwingineko walibomoa majengo watu wa huko kwa maandamano. Watu wa Mtwara wakae wasomeshe watoto na kupanga elimu kama sehemu ya mafao na wasome kikweli. Waache zile ngoma za jando zikianza kulia huko miezi sita  inalia daily usiku mpaka unajiuliza mtu huyo akitoka huko ni degree au cheti gani cha ujasiliamali wakipatacho haa watoto?

Wajadiliane na kupanga kipaumbele vya maisha yao badala hayo pungufu waliojenga miaka 50 ya Uhuru. Wanamvunja nguvu mama Kikwete na viongozi wao kitaifa baadhi waliowachagua wenyewe waliowekeza juhudi zao kuboresha maisha huko kusini makwao.

--- On Thu, 23/5/13, Daud Rwebangila <drwebangila@gmail.com> wrote:

From: Daud Rwebangila <drwebangila@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 23 May, 2013, 9:44

Kama kuna mwanasiasa au mtu yeyote anayefikiria kwamba anawasaidia watu wa mtwara kwa kuchochea vurugu zinazoendelea sasa, mi nafikiri atakuwa mwendawazimu.
Suara hili haliwezi kutatuliwa kwa vurugu za kuharibu mali. Na kinachoonekana hapa ni ubinafsi na baadhi ya watu kutaka umaarufu kirahisi kupitia damu za watu wa mtwara.
Ni lazima tudai haki , lakini wakati huohuo tukihifadhi haki za wengine. Ni lazima watanzania tukubaliane kushare raslimali za nchi na wengine. Kwa miaka mingi tangu uhuru baadhi ya mikoa imekuwa mihimili ya uchumi wa Tanzania na watu wa sehemu hizo hawajawahi kulalamika. Kinachotokea mtwara leo ni matunda ya wenzetu wachache wasioitakia mema nchi hii.

Tukatae vurugu na uvunjivu wa amani, tusimame katika kutetea haki zetu na za wengine bila kuvunja haki za wengine.
Daud
 
2013/5/23 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Mchungu,
Ningekufurahia sana iwapo ungeweka sasa uchambuzi kwamba sasa nini kifanyike kuliko kuwachochea tu wanaMtwara. Au kama hii ndio SERA sawa kwamba hauwezi kusema nini kifanyike ili Utakaposhika madaraka uweze kuitumia hiyo Gesi kudanganyia. Hilo linafahamika bora uweke wazi kipi kifanyike ndugu yangu.
 
K.E.M.S.
From: isack mchungu <isackmn1965@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, 23 May 2013, 0:11

Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI
MWAKYEMBE,
  hivi ni kwa nini mtu akisimama kudai haki anayoona haipati anaonekana katumwa? kama mikoa mingine haiwezi kusimama na kudai hali nzuri ya uchumi unategemea Mtwara wawasemee? na kama unadai Tanzania tuna tatizo la kiungozi unategemea nani aseme? Mtwara wao wameliona hilo, yale ya Liwale hata kwenye ushahidi wa wazi wa dhuruma walisema wametumwa ina maana wao hawaoni? au ni kwa vile mmewaona watanzania ni mazezeta hawajui kitu? acheni mtwara wadai kile wanachodai kama wao wanaoni ni haki yao wadai
   kule usukumani dhahabu inachimbwa, matani yanapelekwa ulaya wao wanabaki na umasikini hata watoto wao hawana madarasa ya kusomea, hali kadhalika kule nyamongo, hata kule mfindi ambako mbao zinavunwa kwa wingi nako shule hazina madawati kwa nini? hamjiulizi hilo kw nini? watu wa mtwara wanasitahili kunufaika na gesi kwanza ndo na wengine tufuatae hakuna mzazi aliyetoa chakula kwa watoto wa jirani ilihali wakwake walale njaa!!!
2013/5/23 Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
Ezekiel,
Hatuwezi kuhalalisha yanayotekea Mtwara kwa sababu ya kusahauliwa. Ni Watanganyika wangapi waliokumbukwa na hiyo serikali, vipi kuhusu Rukwa ambao pamoja na kutekezwa lakini ndio wenye kuwalisha hata hao wa Mtwara, vipi kuhusu Tabora, Kigoma, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Katavi, Kagera, nk.
Tatizo la umasikini linawakaba Watanzania wote, watu wameingia Mtwara wakatumia udhaufu wa umasikini wetu na kuchochea vurugu, hapana lazima tukatae vurugu.
Tukumbuke hizi vurugu zimeanza baada ya taarifa za kuwepo kwa hizo rasilimali, ni mazingira hayo hayo yanayozifanya nchi kama DRC, Somalia, Sudan, na nyinginezo kuwa katika machafuko miaka yote.
Tanzania tuna matatizo  ya kiuogozi kama taifa, lakini pia tuelewe kuna nguvu kutoka nje zenye lengo la kutugonganisha ili wajichotee rasilimali hizo bila bughudha wakati sisi akili iko kwenye kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Felix
2013/5/23 Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com>
Maelezo yako dada Hilda mazuri sana lakini yana kasoro za msingi. Baadhi ya sababu ulizozitoa unaweza kuzitafiti tena kuona ukweli wake. Watu wa Mtwara wanalilia maendeleo Yao baada ya kusahauliwa kwa MUDA mrefu. Kwa MUDA mrefu pato la taifa halikugawiwa kwa Haki. Naweza kukupa mifano michache tu: Angelia barabara zinazoenda kusini na zile zinazoenda kaskazini, kwa nini miundombinu  Hii muhimu itofautiane kiasi hicho wakati nchi ni moja hii hii. Ni kweli Kwamba hata watu wa Maganzo kwenye almasi maendeleo Yao hayalingani na utajiri ulio jirani hapo. Ni kweli Kwamba tujikita kwenye majimbo wengine ambao hawana HAYO madini na gesi watafanyaje? Basi kile kinachopatikana kigawiwe kwa haki, wote wapate, ndipo hiyo amani iwe ya kudumu.

wasalaam

On Wednesday, May 22, 2013, Hildegarda Kiwasila wrote:

Radio zimeongea vizuri zaidi zimetoa maelezo makini ya kinachoendelea na uharibifu unaofanyika na waandishi wa habari kuwindwa eti wakiongea wanaipendelea serikali. Kwa hali ilivyo Mtwara sasa, wageni ni wengi sana wanaohusika na utafiti na shughuli za miradi ya maendeleo funded by international devemopment organizations. Ni hatari sana kama watawavamia hawa na kuwadhuru.

Ikiwa suala ni Gas ibaki kwao, basi watu wa Kihansi na huko Ruaha-Mikumi Kilombero, Pangani 1 and 2 Tanga; Mtera, Nyumba ya Mungu dam ambao hata kuvua huzuiwa nao waanzae kukata milingoti ya Miti kuzuia umeme Usije Dar na Maeneo mengine? Mungu atusaidie. Mbona mafao ya National park, Madini tunatumia nchi nzima kama sources za hela za nchi ambapo hata wafugaji na wakulima kando ya mbuga hizo kuingia protected areas wanaadhibiwa?

Kwao hao vijiji vingine vyenye vyanzo vya umeme umeme unapita juu angani ya waya za umeme wao wanamulikia mienge ya moto. Hawana benefits na benefit sharing ni mkakati mpya wa sasa kimataifa kuanzia RIO Summit 1992.

Maji yanatoka Ruvu, wami yananywewa mijini kuko vijijini misitu ni protected wasitumie ili maji ya mto yapatikane kwenye intakes yafike e.g. DSM. Tukifanya hivi kwamba kila mwenye ambako resource ipo azuie hatutofika mbali. Issue ni planning for benefit sharing. Wao watafaidikaje? Kuwe na mpango katika aina zote za resources ambazo zinatambulika kama mali ya umma sio binafsi. Hatutatatua matatizo kwa kuharibu miundo mbinu. Kubomoa daraja na mwenye mimba sasa na hofu ya mapambano uchungu utakuja haraka. Jee, utamsafirishaje unapokataza wasitoke nje na kuharibu miundo mbinu? Kweli tunafurahia haya na wengine kuona kuwa ndio faida ya utawala ni wa kifisadi ambapo mafisadi ni waume na ndugu zetu. Wakishitakiwa-tunaweka mawakili wazito. Na wakirudi home hao mafisadi tunawapigia KURA sisi wenyewe wanashinda tena. Jamani tumrudie Mungu.

--- On Wed, 22/5/13, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 22 May, 2013, 12:25

Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 
Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) 
Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . 
Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
 Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
Matairi  kila  kona  ya mji  yamechomwa  barabarani  polisi  na  zimamoto   wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi
Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)
Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia ovyo ovyo.
watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia
Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi wayapate .
 Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.
Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo.
Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.
Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)
Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.
Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.
2013/5/22 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Askari mmoja na raia mmoja amefariki na ofisi ya ccm na kituo cha mafuta vimechomwa moto
2013/5/22 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Nasikia hata Guest Houses walizowahi kufikia askari wakati wa vurugu za mwanzo zinachomwa moto (Not sure).
 
Hali kama hii haifai kabisa kwa Taifa huru kama hili. Wahalifu lazima wasakwe na wakamatwe na wafikishwe mbele ya mkono wa sheria.
 
Naona hii sio gesi tu kuna kitu cha ziada hapa.
 
Tutajua tu.
 
K.E.M.S.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.--- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.  

Wasalaam,
 
Denis Matanda,
Mine Planning Supt,
Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

0 comments:

Post a Comment