Wednesday 15 May 2013

Re: [wanabidii] Unamfahamu msichana wako wa kazi ?

Thankx napata fundisho hapa kwa hawa wafanyakaziwa ndani wana mengi sana ambayo tunaokuwa hatupo nyumbani tunakosa kujua. wengine walishakuta mtoto karundikwa kwenye friji na mfanyakazi katembea, unafahamu kuwa mtoto anayelia sana wafanyakazi wa ndani  huwapa kilevi ili walale.


2013/5/15 Jane Mwakalukwa <mwakalukwa@gmail.com>
Kuna familia moja ndio kwanza walikuwa wameoana na wanamtoto mmoja hii
familia ilihitaji msichana wa kazi kwasababu wote walikuwa ni
wafanyakazi ili aweze kukaa na mtoto, basi tafuta huku na kule siku
moja yule mama akaambiwa kunamsichana wa kazi kijijini singida tuma
hela apakiwe kwenye gari aje, basi kwavile yule mama naye alikuwa na
shida wa msichana kweli kwa haraka bila kuchelewa akatuma hela yule
msichana akapakiwa kwenye basi baada ya siku tatu akawasili dar.

Yule mama akampokea na kukaa naye vizuri kama ndugu yake yani hakuna
ambalo jema hakumfanyia yule msichana maana yule dada kweli alikuwa
anajituma sana katika kazi zake yani watu walioingia ile nyumba
walimtamani sana yule dada, miezi sita ikapita yule dada wala
hakubadilika katika utendaji wake wa kazi.

Basi siku moja hivi yule mtoto wa mama mwenye nyumba akaumwa ghafla
wakamkimbiza hospital, walipomfanyia uchunguzi wakabaini alikuwa ana
food poison ndio maana alikuwa anaumwa sana mpaka kuishiwa nguvu maana
anatapika sana pia, basi akapata matibabu na kupona lakini cha
kushangaza yule mtoto alikuwa akipata hayo matatizo kila mwezi mara
kwa mara, wazazi wake wakiwa hawaelewi ni kwa nini.

Kumbe bwana matatizo yote anayasababisha dada wa kazi yule dada
alikuwa anamtindo kila mwezi akiwa katika hedhi hukamulia damu zake za
hedhi kwenye chakula cha mtoto (hayo ni maagizo aliyopewa kutoka
nyumbani kwao singida) na hayo aligundua jirani ambaye alisikia mtoto
akilia bila kunyamazishwa kumbe dada alikuwa busy na kazi yake kwahiyo
yule mama kuchungulia dirishani ndio kumuona dada akifanya hayo, japo
walimueleza mama wa mtoto yeye hakuamini aliona ni wivu tu na maneno
wanayompa kuhusu msichana wake ili aondoke maana wanajuwa jinsi
alivyomchapa kazi.

Basi ugonjwa wa mtoto kila mwezi ukawa unaendelea wameshamaliza
hospital za kila aina, lakini wakati wote huu yule mama bado alikuwa
anawaza maneno ya yule jirani yake aliyomwambia, siku akamuuliza dada
kwani lini huwa unapata hedhi maana nataka nikununulie pedi, dada si
anajuwa hamna anayejuwa siri yake akamueleza yule mama kweli kesho
yake akamletea pedi sasa akawa anasubiri na yeye ajionee kama ni
kweli.

Basi akaomba likizo ofisini kwake ya wiki na kupewa lakini nyumbani
akawa anaondoka asubuhi kama anaenda kazini lakini alikuwa akiishia
kwa yule jirani ikafika saa sita muda ambao mtoto hula chakula cha
jioni, kama kawaida yule mtoto akaanza kulia wakachukuana kwenda mpaka
kwenye dirisha la sitting room na kuchungulia yule mama alivyoona
msichana wa kazi anachokifanya akazimia hapohapo ndio dada kushtuka na
kwenda nje baada ya kusikia kishindo.

Mara kumuona boss wake akaanza kupiga kelele kwamba anataka watu
wamsaidie ndio watu kuja pamoja na jirani kumchukuwa kumpeleka
hospital, yule mama akamwambia dada abaki amlishe mtoto wakati huo
dada bado hajui kama alishaonekanika yule mama akatibiwa na kurudi
jioni na mumewe njiani akawa ameshamuhadithia mumewe ile story nzima
na akamwambia kama alishaambiwa na yule mama jirani sema hakuamini,
yule baba alijawa na hasira sana na kutaka kwenda kumpiga yule
msichana lakini wakashauriana kwasababu yle hajui kama tunajuwa basi
tusimuendee kwa vurugu tumuite na yule mama shahidi tukae na yule dada
tumuhoji.

Walipofika nyumbani kwa kujikaza wasipandwe na hasira wakamuita dada
pamoja na yule mama jirani wakamueleza dada yote wanayoyajuwa, basi
yule dada ndio akaanza hekaheka za kuogopa, na kuomba masamaha
walipomuuliza kwanini alifanya hivyo na kwa muda gani ndipo akawaambia
kwamba tokea siku ya kwanza mtoto alipoanza kuumwa, na kwanini
alifanya hivyo akawaambia ndio alivyofundishwa na mama yake mdogo huko
kijijini aliyemlea ambapo huyo mama naye alikuwa msichana wa kazi
kwenye nyumba ya watu akawa anafanya kazi vizuri na kupendwa sana na
wenye nyumba na baadaye mpaka kutamaniwa kimapenzi na baba mwenye
nyumba ndipo alipoamua kufanya hivyo akawa anakamulia damu yake ya
hedhi kwa mtoto mara kwa mara yule mtoto akaumwa mpaka kipindi akafa,
na mtoto wa pili pia ikafika wakati akawa anapika chakula tofauti
kwakuwa baba mwenye nyumba alikuwa anachelewa kurudi nyumbani kwahiyo
chakula chake huwekewa kwenye hotpots zake mpaka akija ndio hutengewa
basi chakula anachokula mama naye akamfanyia hivyohivyo na baadaye
kumuwekea sumu na kufa na kwakuwa chakula cha wenye nyumba na watu
wengine wa kazi kwenye ile nyumba huwa hakipikwi pamoja basi ilikuwa
rahisi sana kwa yeye kufanya vile kwahiyo akabaki yule baba kwakuwa
walishaanza uhusiano wa kimapenzi akageuka sasa kuwa mama mwenye
nyumba huko singida na mpaka leo kwahiyo alivyopata yeye kazi dar es
salaam alishauriwa kufanya hivyo na yeye apate nyumba
yake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mmmeona balaa za hawa wadada jamani, basi yule dada akapelekwa polisi
akafunguliwa mashtaka na baadaye mahakamani akafungwa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment