LINGONET LINDI
Kwa aina ya polisi tulionao na kwa jinsi wanavyofanya kazi kwa hasira na kulipiza kisasi naamini inawezekana. Tumeshuhudia haya maeneo mengi ya nchi hasa panapokuwa na maandamano au shughuli nyingine za kisiasa hasa zinazowahusu wapinzani. Lkn wasipokuwepo polisi mkutano au maandamano yanaweza kufanyika pasipo vurugu yoyote ile.
Lakini pia na nyie waandishi wa habari kwa nini mnatoa taarifa bila kuzithibitisha? Eti daraja limevunjwa, huwezi kuingia wala kutoka Mtwara lkn hakuna hata picha inayoonesha daraja hilo lililovunjwa. Mara ooh watu wengi wameuawa, jamani kwa nini tunafanya kazi kwa kubahatisha kwa kiasi hiki kana kwamba hawa waandishi sio professional???
Na hii sharia ya kumuingilia mtu ndani na kumpiga na kumkamata polisi wameitoa wapi? Unavunja duka au mlango wa nyumba eti ili umkamate mhalifu au uibe mali zake??? Na ulijuaje kama ndani ya hiyo nyumba kuna mhalifu wakati vurugu inaendelea nje???
Tuna kazi kubwa ya kuvitengeneza vyombo vyetu vya dola hasa polisi kufanya kazi kitaalamu bila kutumia nguvu kubwa kiasi hiki katika kudhibiti vurugu.
Ni maoni yangu tu. Nawasilisha.
From: LINGONET Lindi <lingonetlindi@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, May 25, 2013 12:03 PM
Subject: Re: [wanabidii] Ujumbe Muhimu kwa Wadau wa Habari
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, May 25, 2013 12:03 PM
Subject: Re: [wanabidii] Ujumbe Muhimu kwa Wadau wa Habari
wandugu vurugu za mtwara zimetawaliwa na habari za kishabiki sana ,nadhani hii ni moja ya mambo yanayokoleza sintofahamu katika kadhia yote ya gesi kusini mwa tanzania ,kwa bahati mbaya hata serikali imejiingiza katika kutumia propaganda kukabiliana na yanayojiri mtwara ,iliyofikia kuandaa vipindi maalumu kwa ajili ya kueneza uongo ili wananchi wa kusini waonekane ni wahalifu,waziri mkuu alikwenda mtwara akaongea na wananchi na kufikia makubaliano amabyo mpaka leo hajayatekeleza inayomwia vigumu tena leo kwenda mtwara kwa sababu hana majibu ya maswali atakayoulizwa kufuatia makubalano yao. lakini turudi katika vurugu za tarehe 22/5/2013 wananchi walibaki majumbani mwao ama kutekeleza wito wa vipeperusi au kwa hofu ya vurugu na biashara zote zilifungwa,ni askari tu waliokuwa wanaranda mjini na kupiga mabomu ya machozi bila ghasia zozote,kitendo kilichoamsha makundi ya vijana kuwarushia mawe kama hujuavyo katika jambo lolote kuna watu wanaoshabikia fujo,lakini la msingi walioanzisha vurugu ni polisi,baada ya kuzidiwa na gari ya kurusha maji ya kuwasha kushindwa kufanya kazi,wanajeshi waliingia kusaidia na maeneo yote ambayo jeshi waliwajibika hakukuwa na madhara makubwa kama yale ambayo polisi walikuwepo kwa kukamata wanaume na kuvunja maduka na kupora vitu,kwa bahati mbaya sana vyanzo vya habari vilizusha taarifa zisikuwa na ukweli na kueleza kuwa daraja la mikindani limevunjwa na huwezi kuingia mtwra jambo ambalo si sahihi,siku ya pili ya tarehe 23/5/2013 ndipo polisi walipofanya fujo kubwa sana katika maemeo ya magomeni,chipuputa,mangowela mdenga na tandika.maeneo yote ya madukani shangani railway ambayo wanajeshi walikuwepo hakukuwa na vurugu kwa vile wanajeshi walikuwa wanafanya kazi bila kupora mali wala kuingia majumbani kuwachomoa watu. hivyo dhamira yangu hapa ni tujitahidi kueleza hali halisi ilituweze kupata muafaka huku tukijitahidi kuondoa tabia ya wananchi kufanya vurugu wakati wakudai haki na kuwa na jeshi la polisi linalofanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria wakati waandishi wa habari kama huna chanzo cha habari usizushe taarifa ambayo inaweza kuharibu amani yetu,mwandishi amekimbia fujo amejificha kuogopa kupigwa lakini anasema daraja limevunja bila kuona haya ndio mambo yanayozidisha sintofahamu
|
0 comments:
Post a Comment