Saturday 25 May 2013

Re: [wanabidii] Ujumbe Muhimu kwa Wadau wa Habari

Nijuavyo mimi, fani ya uhandishi wa habari ina maadili yake. Lakini kama huyu mwandishi wa habari amelipwa au amewezeshwa ili kuandika propaganda hapo ndipo maadili yanapoharibika na tunapoteza mwelekeo kabisa. 
 
Waandishi wa habari watafanya kazi kwa uhuru iwapo watajilipa wenyewe. Kwa namna khali ilivyo sasa sijui kama ndugu zetu watakuwa na uhuru na utashi wanaotakiwa kuwa nao. Inafika mahala wanakubali hata vitu ambavyo sio vyenyewe, ili mradi mwenye mbwa kasema. Uhuru wa fikira utatoka wapi?  Nawaza kwanguvu tu!

From: LINGONET Lindi <lingonetlindi@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, May 25, 2013 11:03 AM
Subject: Re: [wanabidii] Ujumbe Muhimu kwa Wadau wa Habari
wandugu
vurugu za mtwara zimetawaliwa na habari za kishabiki sana ,nadhani hii ni moja ya mambo yanayokoleza sintofahamu katika kadhia yote ya gesi kusini mwa tanzania ,kwa bahati mbaya hata serikali imejiingiza katika kutumia propaganda kukabiliana na yanayojiri mtwara ,iliyofikia kuandaa vipindi maalumu kwa ajili ya kueneza uongo ili wananchi wa kusini waonekane ni wahalifu,waziri mkuu alikwenda mtwara akaongea na wananchi na kufikia makubaliano amabyo mpaka leo hajayatekeleza inayomwia vigumu tena leo kwenda mtwara kwa sababu hana majibu ya maswali atakayoulizwa kufuatia makubalano yao.
lakini turudi katika vurugu za tarehe 22/5/2013 wananchi walibaki majumbani mwao ama kutekeleza wito wa vipeperusi au kwa hofu ya vurugu na biashara zote zilifungwa,ni askari tu waliokuwa wanaranda mjini na kupiga mabomu ya machozi bila ghasia zozote,kitendo kilichoamsha makundi ya vijana kuwarushia mawe kama hujuavyo katika jambo lolote kuna watu wanaoshabikia fujo,lakini la msingi walioanzisha vurugu ni polisi,baada ya kuzidiwa na gari ya kurusha maji ya kuwasha kushindwa kufanya kazi,wanajeshi waliingia kusaidia na maeneo yote ambayo jeshi waliwajibika hakukuwa na madhara makubwa kama yale ambayo polisi walikuwepo kwa kukamata wanaume na kuvunja maduka na kupora vitu,kwa bahati mbaya sana vyanzo vya habari vilizusha taarifa zisikuwa na ukweli na kueleza kuwa daraja la mikindani limevunjwa na huwezi kuingia mtwra jambo ambalo si sahihi,siku ya pili ya tarehe 23/5/2013 ndipo polisi walipofanya fujo kubwa sana katika maemeo ya magomeni,chipuputa,mangowela mdenga na tandika.maeneo yote ya madukani shangani railway ambayo wanajeshi walikuwepo hakukuwa na vurugu kwa vile wanajeshi walikuwa wanafanya kazi bila kupora mali wala kuingia majumbani kuwachomoa watu.
hivyo dhamira yangu hapa ni tujitahidi kueleza hali halisi ilituweze kupata muafaka huku tukijitahidi kuondoa tabia ya wananchi kufanya vurugu wakati wakudai haki na kuwa na jeshi la polisi linalofanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria wakati waandishi wa habari kama huna chanzo cha habari usizushe taarifa ambayo inaweza kuharibu amani yetu,mwandishi amekimbia fujo amejificha kuogopa kupigwa lakini anasema daraja limevunja bila kuona haya ndio mambo yanayozidisha sintofahamu--- On Thu, 23/5/13, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Ujumbe Muhimu kwa Wadau wa Habari
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 23 May, 2013, 17:49

Hamna justification ya violence Salum Mkango. Kuna tofauti sana kati ya justification na explanation.
 
Mimi rai yangu kule mabadiliko imekuwa ni kutafuta suluhu ya kweli kwa hizi pande mbili zinazotofautiana kutafuta a common ground. Yaani kila upande ujaribu kuelewa kwa nini upande mwingine unayachukulia mambo tofauti na wao wanavyoyachukulia. Busara itawale, huu sio wakati wa kuonyeshana umwamba.
 
Two wrongs don't make it right nafikiri..................
2013/5/23 salum mkango <salumkango@yahoo.com>
 
Ndugu yangu Juma Mzuri naona sasa tunakuja kwenye point yenyewe haswaa. Kaka yangu Makwaiya wa Kuhenga hupenda kusema "Hapo patamu hapo". Madhara ya kushabikia wanaojichukulia sheria mkononi ndiyo hayo sasa. Haijalishi ulikuwa unadai haki yako ama ya mwenzako lkn kuharibu mali za wengine, kudhuru au kujeruhi eti kwa kisingizi cha jazba haikubaliki na hakuna sheria inayoruhusu uhuni huo. Kusema 'eti wa kulaumiwa serikali' ni ujinga kwani serikali ndiyo inayowaambia wachome moto na kuumiza watu?
 
Hatua kali za kisheria zichukuliwe ili iwe fundisho kwa wengine wanaoshabikia uvunjifu wa amani kwa visingizio vya kudai haki. njia za kudai haki zipo na wanazifahamu. 
From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, May 23, 2013 6:56 PM
Subject: Re: [wanabidii] Ujumbe Muhimu kwa Wadau wa Habari
Nani ni mwandishi wa hii makala? Ni wewe "Juma Mzuri"?
Nakumbushia tu umuhimu wa kuweka vyanzo vya taarifa mbalimbali.....................
2013/5/23 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Ndugu zanguni
Kwanza kabisa napenda kuelezea masikitiko yangu juu ya tukio lililomkuta Mwandishi mwenzangu veteran wa tasnia hii Kassim Mikongoro. Nampa pole sana kwa sababu yaliyomkuta katika ghasia za Mtwara sio tu yamempa hasara ya Mali bali pia yamemuathiri kisaikolojia yeye na familia yake. Niwe mkweli hata mimi nimeathirika kisaikolojia kutokana na tukio lilimkuta Kassim. Na kwa mara nyingine Pole sana Kassim.

Haya yamemkuta Kassim lakini mimi naamini yanaweza kumkuta mwandishi wa habari mwingine yeyote, nasema hivi kwa sababu nina shauku ya kuamsha mjadala utakaosaidia kuangalia mustakabali wa waandishi wa habari katika usalama wao na familia zao. Najua kwa yaliyomkuta Kassim kila mtu anaweza kusema la kwake lakini ni vizuri kukumbushana kuwa tukiweka kando hisia hizo zote Kassim ni mwandishi wa habari kama alivyo mwandishi wa habari mwingine yeyote.

Nionavyo mimi swali hili tunapaswa kujiuliza sote wadau, nikiwa na maana waandishi wa habari wenyewe, wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri wa habari, mamlaka za kiserikali na wananchi ambao tunawahudumia. Kwa namna yoyote ile si haki kuwashambulia waandishi wa habari, tena wasihukumiwe kienyeji namna hiyo. Tukifikia hapo na kwa kuwa Mhimili wetu sio rasmi basi naona huku mbeleni itakua kila asiyeridhishwa na kazi zetu anatuadhibu kwa namna alivyoadhibiwa Kassim. Atabaki nani?

Ni vizuri tulijadili hili kwa weledi na busara na wananchi wajue tuna maana gani. Mimi ni miongoni mwa waandishi wa habari walikutana na mikutuo ya kutishiwa, wakati mwingine kushambuliwa na hata kupigwa kutokana na kazi ya uandishi wa habari. Nakumbuka wakati nasoma chuo kikuu Mwalimu wangu aliwahi kuniambia kuwa siku zote Ukiandika habari hasa yenye sifa na mvuto wa kuwa habari wapo utakaowafurahisha na wapo utakaowakwaza. Nilivutiwa sana na somo hili na nikajiridhisha pasipo mashaka kuwa kumbe kwa waandishi wa habari kukwaza watu kila siku ni sehemu ya maisha yetu katika kazi hii. Matharani ukiandika habari juu ya mpango mzuri wa kuwawezesha wakulima kuzalisha chakula cha kutosha kwa namna yoyote utakua umewafurahisha wakulima lakini pia utakua umewakwaza wafanyabiashara ambao biashara zao zinategemea wakulima wakose chakula cha kutosha ili wao waingize chakula kutoka nje ya nchi na wapate mapesa lkuki ya faida. Hali kadharika ukiandika habari inayohimiza nchi kuishi kwa amani utakua umewafurahisha wanaopenda amani na utakua umewakwaza wanaotamani amani ipotee ili mipango yao ifanikiwe. Ipo mifano mingi. Yaliponikuta ya kushambuliwa wakati nikifanya kazi ya kuripoti hali ya vituo vya kura kuwa shwari baada ya zoezi la upigaji kura ilihali kuna watu walitaka kusiwe na amani kengele iligonga kuwa hizi ndio changamoto za uandishi wa habari.

Sasa mimi najiuliza swali hivi kama kila mtu ambaye hafurahishwi na habari zetu atachukua jukumu la kutushambulia kama ilivyokua kwa Kassim Mikongoro, atabaki nani?

Saa chache baada ya nyumba ya Kassim Mikongoro kuchomwa moto, nimeongea nae kwa njia ya simu, nilishindwa kujizuia na machozi yamenitoka pale kaka yangu huyu ambaye ametumikia kazi hii kwa karibu miaka 40 tena kwa habari, vipindi, makala na ripoti nyingine mbalimbali za kuelimisha wananchi juu ya maendeleo yao ya Kilimo, ustawi wa jamii nakadharika aliponiambia kuwa yaliyomkuta yamesababisha aanze kufikiria kuanza maisha upya kwa sababu kila kitu kimeteketea kwa moto na nilipokua nikizungumza nae ameniambia amebakiwa na pensi na shati moja tu alivyovaa. Imeniuma saaaana saaaana.

Ikaniuma zaidi aliponithibishia kuwa kwa kuwa alijua kuwa ajenda ya gesi imekaa vibaya, katika ripoti zake aliepuka kujihusisha na habari zinazohusiana na gesi. Kwa kuwa alijua hatakua salama endapo atajihusisha na jambo hili. Sijajua waliomhukumu walitumia vigezo gani na wamemhukumu kwa kosa gani Kassim, mtu ambaye amekua mstari wa mbele kuwapigania wakulima wa korosho wa Mtwara, kupigania hali mbaya ya miundombinu ya Mtwara, aliyetengeneza makala kadhaa za kutangaza fursa za Mtwara, ambaye amekua tayari kufanya kazi Mtwara mahali ambako waandishi wa habari wengi hukataa kupangwa huku kufanya kazi kutokana na changamoto za maisha za Mtwara. Siwezi kusema yote hapa. Ila itoshe kusema POLE SANA KASSIM MIKONGORO.

Anyway wadau tuliangalie hili.

Na kwa wakati huu naomba tusisite kumchangia mwenzetu Kassim Mikongolo ili maisha yake yaendelee, tumchangie fedha Jamani na napendekeza tuwe na utamaduni huu ili tutiane moyo kwa kuwa usalama wa waandishi wa habari katika nchi yetu umejaa maswali mengi. Na tukumbuke nchi yetu inatajwa kushika nafasi ya tatu barani Africa kwa waandishi wa habari kuwa hatarini

Pole sana Kassim, nipo na wewe katika wakati huu Mgumu and Please be strong brother.
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
  Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.    
--
Wasalaam,
 
Denis Matanda,
Mine Planning Supt,
Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.    

0 comments:

Post a Comment