Sunday 19 May 2013

Re: [wanabidii] This is indeed good news to you all!

Dear John,
Tunajua kuwa wewe ni mwenye uhusiano wa jiko na Visiwani na kwahivyo unajitahidi kusaidia, kwa hilo tunakushukuru, lakini kusema yasio sahihi sio sawa. Hii huduma imeanza tarehe 31 January, 2013 na kwahivyo kusema kama imeenea dunia nzima isipokuwa Marekani sio sawa. Huduma hii ipo EU, Australia, New Zealand, Canada na katika hii May itakuwepo UAE. Huenda katika mwaka huu huu ikawepo USA, Oman, Saudia, Singapore  na Qatar.
Kaka Matinyi, hii huduma imechelewa kuwepo USA kutokana na kuwa inabidi kila State iwe applied separately na kwa States 52 kumalizika kwa pamoja sio jambo la rahisi. No amount of jingoism, Bw. Matinyi, would belittle these great efforts of our indigenous bank in Zanzibar trying to extricate fellow  Tanzanians in the Diaspora out of the Westen Union quagmire in which most of them are entangled!
Usiku mwema wa Jumaapili!
 
 
...bin Issa.

 
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>; "nkumbaruko@yahoo.com" <nkumbaruko@yahoo.com>
Sent: Saturday, May 18, 2013 9:45:14 PM
Subject: RE: [wanabidii] This is indeed good news to you all!

John,
 
Tunashukuru kwa taarifa yako lakini pia huko mwisho umeweka fununu isiyo na usahihi kwamba huduma hii ipo duniani pote isipokuwa USA kwa sababu Zanzibar haina ofisi ya konsula (nafikiri ulikosea herufi zake kwa Kiingereza).
 
Ukweli ni kwamba, ukiondoa Marekani yenyewe, hakuna nchi yoyote duniani yenye ofisi za konsula kwenye nchi karibu zote duniani. Hilo moja. Na sidhani kama huduma hiyo ipo nchi zote, labda kama kwako nchi zote ina maana nyingine.
 
Pili, Zanzibar haiwezi kuwa na ofisi ya ubalozi ambayo ndiyo huwa na konsula ndani yake ama ofisi ya konsula peke yake (ubalozo mdogo) kwa sababu Zanzibar si seyada, yaani si dola kamili bali ni sehemu ya dola kamili ya Tanzania. Zanzibar inaweza kuwa na ofisi ya biashara lakini si konsula kwa mujibu wa sharia za kimataifa.
 
Tatu, masuala ya kutuma fedha kimataifa hayana uhusiano na masuala ya konsula. Havitegemeani.
 
Nne, huenda kuna sababu nyingine kwa nini Marekani hakuna huduma hii nzuri ya cheee! Itafute kwa kuanzia na sheria za Marekani za mambo haya na udhibiti wake hivi sasa.
 
Matinyi.
 
Date: Sat, 18 May 2013 06:12:01 -0700
From: nkumbaruko@yahoo.com
Subject: [wanabidii] This is indeed good news to you all!
To: wanabidii@googlegroups.com

Jamani,
Hii sio kampeni bali ni ukweli niliougundua hivi majuzi kupitia mashemeji zangu kutoka ZNZ na ninataka Watanzania wote wanaoishi nje wafaidike. 
Watanzania mnaoishi nje, baada ya kuleta pesa nyumbani kutumia kampuni za kupeleka pesa za nje, there is now another provider in town with the most affordable fees. Huyu provider ni The People's Bank of Zanzibar Limited.
Process yenyewe ya kuleta pesa nyumbani ni fupi sana. Unakuenda kwenye website ya PBZ ambayo ni <www.pbzltd.com> na hapo utaiona item hii - 'SEND MONEY'. Ukii-click hii item itakupeleka kwa wakala wa PBZ ambae ni kampuni moja kutoka UK ya remittances. 
Fees za PBZ za kuleta pesa nyumbani zipo chini sana ukilinganisha na fees mnazolipa hivi sasa kwa hizo multi-national remittance companies. In fact, fees za PBZ ni less than 1/4 of what you are paying right now. Asieamini alinganishe fees mwenyewe kabla hajaleta pesa hapa nyumbani kutoka huko majuu.
Majuzi nilipowapigia simu PBZ Ltd kuwaulizia zaidi juu ya hii huduma yao, nilielezwa kuwa japokuwa hivi sasa mtu wako atapokea hapa nyumbani TShs tu, lakini katika mwezi huu huu wa May huduma nyengine zitaanza ambazo zitamuezesha mtu wako Tanzania kupokea katika any major foreign currencies. Pia, mtaweza kuleta pesa moja kwa moja kwenye simu (mobile money) au katika account ya benki yoyote ile hapa nyumbani. Kupitia PBZ Ltd, sisi tuliopo Tanzania tutaweza kupeleka pesa nje kupitia hii online service yao bila ya kuenda benki kupanga foleni. Kama mwanao anasoma Uganda, Kenya, India, etc basi next time hunahaja ya kuenda kusimama foleni kwa masaa 3 ili kupeleka Dollar 100!

//Nkumba.

N.B.
Nimefahamu kwamba hii huduma ipo nchi zote isipokuwa USA. Nadhani labda kwasababu Zanzibar bado haina councillor office huko Washington!


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment