Friday 17 May 2013

Re: [wanabidii] Re: UJERUMANI INAHUSIKA NA MGOGORO WA GESI MTWARA

Huu ugonjwa wa kufanya kitu na kuwatuhumu wengine (kutafuta machawi
nje) utatuchukua muda mrefu kuutibu. Unakuta mtu anaua halafu
anayelaumiwa kwa mauaji ni Marekani. Mtu anaiba na kufanya ufisadi
halafu wanaolaumiwa ni wazungu kwa kutuletea ukoloni. Unakuta tunaamua
kuua elimu yetu iliyokuwa nzuri, halafu wanaolaumiwa ni wafadhili kwa
kutotupa fedha, ambazo hata hivyo zinaishia kutotumika vizuri licha ya
fedha zetu kuzitumia vibaya. Witch finding won't help us develop, my
friends!

On 5/18/13, Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com> wrote:
> Yona,
> Mimi nilidhani baada ya ile PhD ungepunguza au kuondoa uropokaji, kumbe
> hakuna kilichobadilika!
> Tunashindwa kutimiza wajibu halafu tunasingizia nchi nyingine. Hiyo ndiyo
> tabia ya watu wazembe na wavivu, kwao kila tatizo linasababishwa na
> mwingine. Kama hujui, katika jamii yoyote, wakati wote kutakuwa na matatizo,
> ni wle tu wenye vichwa vizuri na mbinu sahihi za kukabiliana nayo ndiyo
> hufanikiwa na kusonga mbele. Wale ambao kila wakipata tatizo hukimbilia
> kuropoka na kutafuta visingizio ndiyo hubakia kama tulivyo Watanzania.
>
> Yona, kale kamsemo ka kiswahili kanakosema, 'Mbaazi akikosa maua husingizia
> jua', unakafahamu na kufahamu maana yake? Hiyo inaonesha kuwa siku za kale
> kulikuwa na wenye akili kuliko tulivyo wengi siku hizi. Hawa walikwishajua
> wakati huo kuwa kuna watu ambao watashindwa kutimiza wajibu au kwa makusudi,
> uzembe au kwa kutokuwa na uwezo, kwao siku zote jibu la mattizo ni
> kusingizia wengine.
>
> Sent from Yahoo! Mail on Android
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment