Saturday 18 May 2013

Re: [wanabidii] Re: UJERUMANI INAHUSIKA NA MGOGORO WA GESI MTWARA

Mkinga,
Watu wenye mawazo kama ya Yona ni wa kuwaogopa sana. Naanza kuogopa kila kitu sasa katika nchi hii. Maslahi hayo ya Ujerumani ni yapi mbona hayatajwi? Nijuavyo mimi kwa kuishi kwangu Mtwara kwa zaidi ya miaka 20 ni kwamba kuna wamissionari wengi wa Kijerumani katika shirika la Benedictine Fathers ambao ndiyo wanaendesha hospitali za ndanda iliyopo Masasi na Nyangao wilaya ya Lindi. Shirika hili linafanya shughuli nyingi za uzalishaji mali. Wanalima, kufuga, wana magereji ya kuaminka, makarakana ya uchongaji chuma, mawe na seremala, wanajenga nyumba, wanatengeneza wine kama vile mabibo, mango nk. Tokea kale shirika hili lenye idadi kubwa ya raia wa Kijerumani limekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi. Siku ya nyuma walijihusisha sana na uchongaji wa vinyago vya mpingo ambavyo walikuwa wanavisafirisha kwenda Ulaya. Baada ya kifo cha Father maarufu sana kwa Mtwara na Lindi (Father Idelfonce) shughuli za vinyago zimesimama. Huyu ndiye mtu aliyetoa msaada wa kivuko cha kwanza cha mto Ruvuma kwenda Msumbiji kupitia Kilambo.
Hili ni shirika la dini hata kabla ya uhuru. Yona anataka kuchochea masuala ya dini. Afanye uchunguzi wa kina kabla hajaropoka. Kuna shirika lingine la kiroma ambalo pia lina raia wengi wa kijerumani linaitwa Salvatorian fathers likiwa migogo, lukuledi, lupaso kwa mheshimiwa BW Mkapa na nanjota masasi. Hawa makao makuu yao yapo Tunduru. Wajerumani wenye maslahi na gesi ya Mtwara wanaishi wapi? Suala la gesi ya Mtwara si suala la kujiingiza kichwakichwa tu kuliongelea, Yona lazima awe makini. Hili ni suala zito si sawa na yale anayotuletea kila siku juu ya kina Slaa na wenzake.

--- On Fri, 5/17/13, Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com> wrote:

From: Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: UJERUMANI INAHUSIKA NA MGOGORO WA GESI MTWARA
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Yona Maro" <oldmoshi@gmail.com>
Date: Friday, May 17, 2013, 10:00 PM

Yona,
Mimi nilidhani baada ya ile PhD ungepunguza au kuondoa uropokaji, kumbe hakuna kilichobadilika!
Tunashindwa kutimiza wajibu halafu tunasingizia nchi nyingine. Hiyo ndiyo tabia ya watu wazembe na wavivu, kwao kila tatizo linasababishwa na mwingine. Kama hujui, katika jamii yoyote, wakati wote kutakuwa na matatizo, ni wle tu wenye vichwa vizuri na mbinu sahihi za kukabiliana nayo ndiyo hufanikiwa na kusonga mbele. Wale ambao kila wakipata tatizo hukimbilia kuropoka na kutafuta visingizio ndiyo hubakia kama tulivyo Watanzania.

Yona, kale kamsemo ka kiswahili kanakosema, 'Mbaazi akikosa maua husingizia jua', unakafahamu na kufahamu maana yake? Hiyo inaonesha kuwa siku za kale kulikuwa na wenye akili kuliko tulivyo wengi siku hizi. Hawa walikwishajua wakati huo kuwa kuna watu ambao watashindwa kutimiza wajibu au kwa makusudi, uzembe au kwa kutokuwa na uwezo, kwao siku zote jibu la mattizo ni kusingizia wengine.

Sent from Yahoo! Mail on Android

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>;
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] Re: UJERUMANI INAHUSIKA NA MGOGORO WA GESI MTWARA
Sent: Fri, May 17, 2013 2:01:40 PM

Mimi sijataja CCM Kwenye habari yangu na nisingependa kuingia kwenye
ushabiki wa vyama , hivi mtu akiwa na mawazo tofauti na yako lazima
awe CCM ?AU serikalini ndio mnachofundisha vijana hicho ?

Huko mtwara kuna mgogoro unaochochewa na Ujerumani ambao wanalinda
maslahi ya uwekezaji wao ili gesi izalishwe huko kwa maslahi yao

On May 17, 2:56 pm, Emmanuel Muganda <emuga...@gmail.com> wrote:
> Hivi, ninyi CCM mtaendelea kutafuta mchawi mpaka lini? Mmeshindwa
> kuipakazia Chadema sasa mnakuja na singo ya Ujerumani.
> Hivi mnadhani Watanzania ni mazuba kiasi hicho? Watu wamechoshwa kunyonywa
> na ubinafsi wa serikali ya CCM.
> em
>
> 2013/5/17 Yona F Maro <oldmo...@gmail.com>
>
>
>
>
>
>
>
> > Ndugu zangu
>
> > Kwa taarifa ambazo sio rasmi na ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi
> > usiku na mchana sasa hivi kidole cha uhusika wa vurugu kadhaa
> > zinazohusiana na gesi mkoa wa mtwara na lindi kinanyoosha  kwa taifa
> > la ujerumani na maslahi yake kwa gesi na mafuta katika maeneo ya
> > mwambao na karibu na huko .
>
> > Ombi langu ni kuwataka watanzania wenzangu kutokuingia kwenye mitego
> > hii .
>
> > --
> > Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> > ukishatuma
>
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> > consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> > presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> > to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > ---
> > You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> > "Wanabidii" group.
> > To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> > email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> > For more options, visithttps://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment