Tuesday 14 May 2013

Re: [wanabidii] Nyuki Kufukuza Tembo Rombo

Khildegarda umenifurahisha na stori ya Nyegele!! Ahsante kwa kunijengea ufahamu

Sent from my iPhone

On May 14, 2013, at 2:49 PM, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:


Ninachangia kusema-sidhani kama watu wa Rombo hawajui kuwa nyuki hufukuza tembo na wanyama pori wengine hasa akiingia ndani ya mkonga wa tembo humo ni kiama kwa tembo. Ila huenda kuna tatizo au matatizo mengi kwa nini hawaweki mizinga hata ya kienyeji.

Mimi nimekaa vijiji around Mkomazi Game reserve sasa National Park kwa mwaka + katika research. Nimejifunza mengi kutoka kwa wazee kuhusu jinsi ya kukwepa wanyama pori kila mnyama na mbinu yake. Jinsi wanavyozuia wanyama pori n.k

Huko Upareni mizinga ya asali ya nyuki waumao ilianza kutumika toka wahamie maeneo hayo.

Mizinga ya nyuki na uuzaji asali ndio iliyotajirisha matajiri wa awali, asali inaheshimiwa sana na ina matumizi mengi. Wanavijiji ktk mila na desturi zao wanaelewa kabisa kama nyuki hufukuza tembo na wanyama wengine waharibifu wa mazao na huweza kuua mifugo-ngombe, mbuzi. Hivyo, maeneo wanakoweka mizinga hakufanyiki shughuli za kilimo na kupitisha mifugo ni mwiko kabisa kwa sababu harufu ya mbuzi, ng'ombe itatimua nyuki ziwaume. Huruhusiwi kupaka perfume halafu upite karibu na mizinga-utaumwa na nyuki. Moshi wa kuchoma mashamba unaua ufugaji na kufukuza nyuki. Kwenye mizinga no kuchoma majani na mizinga ya nyuki waumao huwekwa mbali na makazi ya watu na mashamba. 

Hivyo mizinga ya nyuki huwekwa maeneo maalum na wana maeneo ya misitu na vilima maalum na aina ya miti maalum pa kutundika kama common pool resource. Mzinga unaheshimiwa pia nyuki wanaheshimiwa sana sana.

Mnyama anayewapa shida katika mizinga ni Nyegele huyu huua nyuki. Hupatnda mti uliko mzinga, kujambia na akijamba nyuki hufa, kisha huuangusha mzinga na kula asali. Hewa chafu ya nyegele (ushuzi) unaua nyuki. Wafugaji nyuki huchukua asali na kubakiza kiasi ya matoto ya nyuki na malkia na nyuki wafanyao kazi kutwa.  Hawaimalizi yote na kuua kila kitu kama kijambo cha nyegele kifanyavyo au wezi wa asali mizingani.

Nyegele ni deadly animal kwa wafugaji nyuki maana anaweza sio tu kukuumiza vibaya na ngozi yake akituna kuwezi kumpiga hata mkuki, anaua nyuki. Kwa sasa binadamu wanaogopa sana wezi wa asali kuliko nyegele kwani wezi ni waharibifu kuliko nyegele. Huangusha mzinga, kuupasua, kuuiba, kuchoma nyuko kwa moto na moshi hawajali kulinda matoto na malkia n.k.na wakikukuta watakuumiza au kukuua usiwataje.
Hakuna tena heshima ya mizinga kama private property na miti ya kutundikia mizinga kama common pool resource free for all and protected. Miti kama Mfune (mirefu kupanda tabua kiasi) hukatwa, Mibuyu pia na mingineyo hardwood trees ni ya kutundika mizinga huchakachuliwa.

Nimeona Southy Pare jinsi gani wakulima Mkomazi hujenga chaga juu ya miti ya kukaa mtu juu kuangalia tembo wajapo kisha kuvuta kamba ambayo imeunganishwa na makopo ambayo hupiga kelele. Mmojawapo akiwaona wanyama hao hupiga mbinje na kila mmoja huvuta kamba yake. Tembo hapendi kelele-hugeuza njia na kwenda kwingineko. Wakisikia harufu ya nyuki ktk mizinga-hawapiti huko wanapita mbali kwani hawawezi kula juu ya mti, kuvunja matawi wala kuuangusha. Mbinu nyingi za kienyeji za kupambana na wanyama tumeziacha, hata za ulinzi wa mazingira. Mbinu nyingine ni kuchimba mabwawa ya maji nje ya kijiji karibu na mbuga zao. Hizi ni irrigation canals au furrows (Mifongo) ambayo ni toka enzi za babu ikinywisha mifugo (ng'ombe, mbuzi etc) na wanyama pori. Mfereji Wizara ya Maji ime document ni ya 1860s ikiitwa-Mfereji wa ng'ombe. Leo hii mifereji hiyo imeachwa imeharibika hata mifugo na wanyama pori kuingia kunywa maji mashambani na kuharibu mazao. Mingine imemomonyoka imekuwa canyon maji yakiingia yanayokomea. hii ni kutokana na wingi wa mifugo kutoka maeneo mbalimbali kutegemea chanzo kidogo, bado wanyama pori. Huko Monduli sio tu Tembo, mpaka simba ameonekana aking'oa bomba za chuma za maji ya kunywa ili apate maji. Huduma hafifu za watu wa national parks both tanzania na Kenya-kuchimba mabwawa ya maji ndani ya Park ndio inafanya spillover ya wanyama kuwa kubwa kutoka mbugani kwenda mashambani kutafuta maji na kula mazao. Hivyo, mizinga isipozunguka maeneo makubwa ya kijiji-watatafuta upenyo wataingia tuu kutafuta maji na kula mazao.

Tatizo la wazee Rombo kutokuweka mizinga mashambani kuzuia Tembo halitokani tu na wao kutokujua maana hili. Hii siidhani kama ndio sababu pekee kwani mizinga ya nyuki ndio mila yao Kilimanjaro Region!! Pia  traditional irrigation system ambayo hupatia nyuki maji ili wafanye kazi yao waache kutembea mbali kusaka maji. Kila baada ya miezi 3 mtu huvuna asali kama kuna maji na misitu haikuchakachuliwa, mazao yamechanua maua na miti pori pia. Asali kwa wachaga, wapare, wasambaa na makabila mengi ikitumika kama sehemu ya kulipa mahari; kutengeneza pombe ya asali na nyinginezo, kutibu maradhi na kunywa chai. Ufugaji mifugo, uzuiaji wanyama pori na utundikaji mizinga-wanajua.

Ila kwa sasa-Rombo inatumika sana kama njia ya mkato kupitisha magendo mchana na usiku kwenda Kenya. Pilikapilika za mashambani na kuweka mizinga ya nyuki inakuwa tatizo. watoto nao wasiosikia huenda kupiga manati mizinga. Ile mizinga ya kisasa-watu huiiba na kuchukua hayo masanduku na kuzeuza ya kuweka nguo na vifaa vinginevyo. Hivyo, wazazi huogopa kuweka mizinga mashambani au jirani na nyumba ili kusitokee maafa ya nyuki kwa sasa population kubwa kuliko zamani na watiifu wachache.

--- On Tue, 14/5/13, Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com> wrote:

From: Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Nyuki Kufukuza Tembo Rombo
To: "Ahmad Michuzi" <amichuzi@gmail.com>, "Augustine Mgendi" <mgendi2004@yahoo.co.uk>, "Henry Mdimu" <mdimuz@gmail.com>, Haki.yako@gmail.com, "Cathbert Kajuna" <cathbert39@gmail.com>, johnbukuku@gmail.com, "Jestina George" <jestinageorge@googlemail.com>, "Josephat Lukaza" <josephat.lukaza@gmail.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Subi Nukta" <subi@wavuti.com>, "Sigfred Kimasa" <kingkif07@gmail.com>, "zainul mzige" <zainul.mzige21@gmail.com>, "Maggid Mjengwa" <mjengwamaggid@gmail.com>, "Bashir Nkoromo" <nkoromo@gmail.com>, "John Badi" <badijohn30@yahoo.co.uk>, uwazi@hotmail.com, "Othman Michuzi" <othmanmichuzi@gmail.com>, "MUHIDIN MICHUZI" <issamichuzi@gmail.com>
Date: Tuesday, 14 May, 2013, 8:28


Wilaya ya Rombo Kutumia Nyuki Kupambana na Tembo Wavamizi

Na Thehabari.com, Rombo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Rombo imeanza mipango ya kutumia ufugaji wa nyuki kukabiliana na tembo waharibifu ambao mara kadhaa huvamia baadhi ya makazi ya wananchi maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kufanya uharibifu wa mazao pamoja na kuua au kujeruhi wakazi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Judethadeus Mboya alisema tayari halmashauri hiyo imetengeneza mizinga ya nyuki ambayo imesambazwa maeneo kadhaa ili kukabiliana na tembo waharibifu eneo hilo.

"Unajua nimetembea mbuga mbili za Kenya ikiwemo Tsavo ambazo tumepakana nazo eneo hili sehemu ambayo tembo hutokea huko na kuvamia maeneo yetu, sehemu hizi wao wamedhibiti uvamizi wa tembo...wamefuga nyuki wengi sana na maeneo mengine wametumia hadi teknolojia kuwazuia tembo kuvamia makazi ya raia hivyo hawapati madhara kama yetu," alisema Mboya akifanya mazungumzo na gazeti hili ofisini.

Alisema kwa sasa tayari wametengeneza mizinga 50 ya nyuki na kuifunga ukanda wa chini wa vijiji kama Chala, Ibukoni, Ngoyoni na maeneo mengine ambayo tembo huyatumia kama njia kipindi cha uvamizi na kwa sasa mizinga mingine 100 ya nyuki inaandaliwa kuenezwa maeneo mengine kukabiliana na tembo hao hatari.

Alisema viongozi wa halmashauri hiyo pia wametoa elimu kwa wanakijiji maeneo husika ya kuhamasisha uvugaji nyuki katika vikundi ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tembo hao waharibifu ambao idadi kubwa hutokea nchi jirani ya Kenya na kufanya uharibifu pamoja na kutishia maisha ya wanavijiji upande wa Tanzania.

Aidha kiongozi huyo alisema tembo hao mbali na kufanya uhalibifu mkubwa wa mazao ya wanavijijini kipindi cha uvamizi wakati mwingine wamekuwa wakiuwa raia jambo ambalo ni hatari zaidi kiusalama.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini uvamizi wa wanyama hao umekuwa kero kwa maeneo mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo, kiasi ambacho unatishia shughuli za maendeleo ya wananchi kama kilimo pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Akizungumzia hali ya uvamizi wa tembo na athari za elimu, Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Tanya, Shuma Himidiel alisema miezi ambayo tembo huanza kufanya uvamizi huingilia ratiba za masomo na mara kadhaa kusimama kutokana na hofu ya wanafunzi na usalama wao hasa wanapotoka na kuja shuleni.

"Kimsingi wanyama hawa wanapoanza usumbufu kijiji kizima huwa na heka heka na wakati mwingine hata wanafunzi wanashindwa kuja shule kuhofia maisha yao...hata wazazi huwazuia watoto wao kutoka hadi hali ya hatari inaporejea kuwa ya kawaida.

Akifafanua zaidi mwalimu Himidiel alisema mara ya mwisho tembo kufanya uvamizi katika Kijiji cha Tanya waliua mtu mmoja walipokuwa wakidhibitiwa na askari wa wanyamapori eneo hilo. 

*********************************************************
Maelezo Picha

Mashamba-
Baadhi ya mashamba ya wananchi eneo la Rongai, wilayani Rombo ambayo mara kadhaa huvamiwa na tembo waharibifu.

Shule-
Pichani ni baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Rongai, wilayani Rombo. Shule hii ni miongoni mwa maeneo yanayoathiriwa na uvamizi wa tembo waharibifu ambao huathiri taaluma shuleni hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya akizungumza na mtandao wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo.
________________________________________________----------------------------________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment