Saturday 25 May 2013

Re: [wanabidii] NIMEAMUA KUKANUSHA: KIGWANGALLA NA UDINI WAPI NA WAPI?

Mhe. Dr. Kigwa',
Nimesoma tamko lako kwa makini, japo sehemu kubwa ni "fagilia tuu" ila kuna moja kubwa la msingi ambalo umeliweka wazi na bila kumungunya maneno. Ni hiyo hoja yako number 4!. Ulichofanya hapa, kuonyesha kuwa wewe kama mwanasiasa, uko bold na unasimama firm kusimamia unayoyaamini ambazo ni sifa njema kwa mwanasiasa yoyote to be bold and take a firm stand on what s/he believes is the right thing, right choice a right stand!, then you stand by it!, if you choice will stand, then you'll stand by it!. if your choice will fall, down the drain, you'll go with it!.

Nilikudhania na wewe uu ,miongoni mwa wana CCM makini ambao wanayo machaguo yao mioyoni mwao, ila wamejinyamazia, wakilisubiri chaguo la chama ndipo watoe misimamo!. Nasikitika sana kukuarifu kuwa kwa msimamo wako huu, jihesabu kuwa wewe ni only one term MP wa Nzega, tena nakushauri don't even try to think to try again, through CCM!,  it will be wastage of your time and resources labda kama utakuwa bold enough to cross!, vinginevyo by now, kwa msimamo huo, you are half dead waiting for complete death 2015!.
Hongera kwa msimamo!, na pole for  the consequences!.

P.
 
Pascal Mayalla
Media Consultant
Press & Public Relations (PPR)
WDC Bldg. Mkwepu Street
Box 5081 Dar es Salaam
Phone : +255 22 2627770
Fax : +255 22 2627770
Mobile: +255 784 270403
E-mail: pascomayalla@yahoo.co.uk

From: Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, 25 May 2013, 8:27
Subject: [wanabidii] NIMEAMUA KUKANUSHA: KIGWANGALLA NA UDINI WAPI NA WAPI?

OFISI YA MBUNGE
JIMBO LA NZEGA
Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Kufuatia taarifa za uzushi zinazosemekana zilitokana na kikao cha wabunge wote wa CCM (CCM party caucus) zilizoenezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na haswa kwenye mtandao wa kijamii na watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu jina zuri la Mhe. Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.) kwa kuchafua taswira yake na heshima kubwa aliyojijengea kwa muda mrefu kwenye jamii, tumeelekezwa kutoa taarifa hii yenye lengo la kukanusha na kuweka kumbukumbu sawia kwa lengo la kuuelewesha umma.
Kwanza, anasema Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.), hana tabia za kuwagawa watu kwa matabaka ya itikadi zao, dini ama makabila yao. Anasema msingi huu wa kuishi kwa kushirikiana na kupendana anautoa nyumbani kwao Nzega alipozaliwa na kukulia, kwa babu yake aliyekuwa Sheikh na muasisi wa Taasisi ya kiislam ya Nusratul qadiriyya (zawia) ambayo ilikuwa na wafadhili wakuu wakristo na kila mwaka walikuwa wakishiriki kwa hali na mali kwenye maulid na dua nyingine mbalimbali; miongoni mwa walezi na wafadhili hao ni pamoja na Hayati Chief Humbi Ziota, Mhe. Lucas Lumambo Selelii (Mb. Mstaafu wa Nzega na Katibu wa Makanisa ya Pentekoste Mkoa wa Tabora), Mhe. Steven Maziku Kahumbi (Mb. Mstaafu wa Bukene), Hayati Mhe. Mzukila (Mb. Mstaafu wa Nzega) – ambao walikuwa ni wa dini ya kikristo. Ni msingi huo uliomfundisha yeye kuwa mstari wa mbele kwenye kuunga mkono jitihada za watu wa dini zote na hata wasio na dini katika shughuli zao za kuendeleza imani zao ama kufanya shughuli za maendeleo bila kuingilia uhuru ama itikadi zao. Ni katika msingi huo huo amekuwa akishiriki kujitolea kujenga makanisa, misikiti na hata kuchangia kazi za wasanii wa kwaya mbalimbali bila kubagua kwa misingi ya udini. Watu wa Nzega ni mashuhuda kwa hili. Na zaidi ya hapo, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb.) hawezi kuwa wa mstari wa mbele kuhamasisha ubaguzi wa kidini, jambo ambalo kila siku analipinga hadharani, na kwamba yeye binafsi ana Ndugu wa damu wenye wazazi wa kikristo, na waliooa ama kuolewa na wenza wenye dini ya kikristo na kuzaa watoto na wajukuu wa dini ya kikristo. Na pia si muumini wa kutafuta umaarufu kunuka unaotokana na kuwagawa watu kwa hoja dhaifu na mfu kabisa za udini.
Pili, Mhe. Hawa Ghasia (Mb.) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), HAKUWEPO KABISA kwenye kikao, hivyo  yote yanayosemwa na wazushi hawa ni ya uongo na hayana msingi wowote. Maana Mhe. Ghasia, asingeweza kumshambulia Mbunge Mwenziye ilhali hakuwepo kabisa kwenye mkutano huo.
Tatu, Mhe. Munde Tambwe Abdallah (Mb.), HAKUZUNGUMZA hata mara moja. Hivyo yote yanayosemwa dhidi yake ni uzushi na uongo wa kupindukia.
Nne, Mhe. Bernard Membe (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ni rafiki yake mkubwa na wa karibu sana na kama ingetokea akasemwa kwa nia ya ubaya ama kumharibia sifa na yeye akiwemo kwenye kikao hicho, bila shaka yoyote ile angesimama kumtetea. Hivyo hili la Mhe. Membe kusemwa, halikuwepo na ni UONGO wenye nia ovu ya kuwagawa wanaCCM katika makundi "hasimu ya kulazimisha" ambayo hayapo.
Tano, anawataka watu wenye mradi wa kumchafua wakome mara moja maana mradi huu ni dhahiri kabisa haujawalipa mpaka sasa na kamwe hautowalipa. Kama ni vita za Urais ama Ubunge basi wasubiri 2015 watapambana. Taarifa hizo za kizushi zilizosambazwa na namna zilivyowekwa ni wazi kabisa zinalenga kumchafua Mhe. Bernard Membe (Mb.), ambaye ni rafiki yake wa karibu na anatajwa tajwa kuwa na uwezekano wa kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015, na kwa maana hiyo haihitaji akili ya Albert Einstein kubaini kuwa ni nani aliye kazini kwenye hili. Ametutaka tuwaambie hao watu kuwa yeye hayuko tayari kamwe kumuunga mkono mgombea wao, mwenye tuhuma za kifisadi, ambazo hazikwepeki na hazisafishiki, mwenye tamaa ya mali na madaraka isiyokoma na kwa kuwa yeye siyo mnafiki, analiweka wazi hili. Na kwamba kama ikitokea kweli Mhe. Bernard Membe (Mb.) akachukua fomu ya kuwania Urais yeye Mhe. Dkt. Kigwangalla atakuwa tayari kumuunga mkono na kumfanyia kampeni ya kufa na kupona kwa kuwa anaamini katika usafi na uzalendo wake, umakini wake na uwezo wake wa kazi. Na kwa kuwa anaamini kuwa kama Mhe. Membe atakuwa Rais, basi nchi itakuwa kwenye mustakabali mwema.
 
Anawasishi wanahabari kusimama kwenye weledi na kuacha kuandika mambo ambayo hawana uhakika nayo na bila hata ya kuwahoji wahusika.
 
Taarifa hii imetolewa leo Tarehe 24/Mei/2013 na;
TeamHamisiKigwangalla
Ofisi ya Mbunge,
Jimbo la Nzega.


--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment