Thursday 16 May 2013

Re: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa

Mngonge,
Ni Mfumo Kristo na mawakala wake.

Walewale.

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, May 16, 2013 6:31 PM
Subject: Re: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa

Nyaronyo alichosema yuko sahihi kiasi fulani. Kuendesha taasisi kubwa kama dhehebu la dini fulani inahitaji uelewa mkubwa na mikakati. Ni kweli wamissionari walipoingia hapa kwetu ili kuwavutia wateja (waumini) walianzisha vitu vya kuwavuta. Ni nyayo hizo hizo zinazofuatwa na kanisa katoliki hadi leo. Kwamba ili dini iweze kukubalika na jamii pamoja na kutoa huduma za kiroho lazima uunganishe na huduma nyinginezo za kijamii.

Historia inatuonyesha kwamba utawala wa kwanza ulio imara ulianza kuonyeshwa na rumi (kanisa katoliki) na hadi sasa wanayaendesha makanisa yao kwa misingi imara ya utawala na hivyo ni rahisi kwao kupanga na kufanikiwa.

Ndugu Amour si kweli ninaongelea kitu ambacho niko blind kama ulivyoona wewe. Ninaposema vijana waliteka misikiti na kuwatimua wazee nina ushahidi toka mkoa wa Dar es salaam wala siyo simulizi.

Kiserikali dini ni taasisi zinazosajiriwa kama NGOs sioni sababu ya kuendelea kugombana kwa sababu ya mambo ya kiimani. Kama uongozi wa taasisi ya dini unakinzana na waumini ni vyema kurudi kwenye maandishi yaliyoisajiri taasisi hiyo na haki kupatikana badala ya kukaa tukilalamika. Mchawi anayezuia waislam wasiungane pamoja kuunda chombo kinachokubalilika  kuliko BAKWATA ni nani? Hapo ninaomba kuelimishwa

2013/5/13 amour chamani <abachamani@yahoo.com>
Kicheere,
Ninavyojua mie anchokifanya Rostam si kitu kizuri una maana gani kulinganisha na Kanisa Katoliki?

Walewale.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, May 12, 2013 9:39 PM
Subject: RE: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa

Dah! Mjomba Nyaronyo, hii makala niliikosa, nashukuur umetufanyia hisani kwa kuiweka hapa. Uliipiga, siyo mchezo.
Naomba uilete ile ya ulipobadili jina lako. Naisikia tu.
 
Date: Sat, 11 May 2013 12:47:12 -0700
From: kicheere@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa
To: wanabidii@googlegroups.com

bandugu na hasa mabwana zito kabwe, mngonge, juma abdala na paul;
 
nadhani tatizo siyo bakwata bali tatizo ni waislamu wenyewe. nadhani kukidhi kiu ya kwa nini nasema tatizo ni waislamu wenyewe soma makala yangu hii ya zamani kidogo niliyoandika kwenye mwanahalisi ikiwa na kichwa cha habari rostam aziz anacheza kama pele.

Rostam Aziz anacheza kama Pele
Rostam bwana, noooma!
Na Nyaronyo Kicheere
Rostam Aziz, yule mtuhumiwa wa ufisadi aliyejiuzulu nyadhifa zake zote katika CCM kwa sababu hapendi siasa uchwara, anajua kucheza kama Pele na kupanga mipango na mikakati kama Kanisa katoliki.
Nimeanza na msemo huo hapo juu kwa kufahamu kwamba tangu dunia imeumbwa hakujatokea mchezaji wa mpira wa miguu aliyevuma na kufunga magoli mengi kama alivyowahi kufanya Edson Arantes dos Nascimento "PELE".
Nimeambiwa na wapenzi na washabiki wa mpira wa miguu au soka (soccer) au kabumbu au gozi au futiboli kama wanavyouita wengi mchezo huo kuwa katika uhai wake, Pele, mchezaji mweusi mzaliwa wa Brazil, alifunga zaidi ya magoli 1500, Na rekodi hiyo haijavunjwa hadi leo.
Nimeambiwa pia kuwa, Pele alicheza fainali za kombe la dunia mara tatu katika miaka ya sabini akiwa na wataalamu wenzake wa kusakata gozi au kabumbu akina Garincha,….
Na mtu pekee ninayeweza kumlinganisha na Pele hapa nchini lakini yeye akisakanya kutafuta sabuni ya roho, yaani kitu pesa, ni mbunge wa zamani wa Igunga na mweka hazina wa zamani wa CCM na mmiliki wa makampuni zaidi ya kumi nchini, Rostam Aziz.
Rostam Aziz anapotafuta pesa, anapowekeza, anapofuatilia noti, hucheza kama Pele! Akikuacha bega tu, utakuta katengeneza milioni wakati wengine hata ndururu hamjapata.
Huyo ndiye Rostam, lakini hayo tisa kumi ni jinsi anavyojua kupanga na kupangua, akiweka mikakati ya kupata noti. Katika hili, taasisi pekee tunayoweza kumlinganisha nayo ni Kanisa Katoliki, lile Kanisa alilowahi kuliandikia Paulo Mtume wa Mungu, akiwahubiria Wagalatia, Wakorintho na Warumi.
Hapa sikaribishi ubishi, angalia tu mambo yanavyoliendea vizuri Kanisa Katoliki hapa nchini. Na siku zote si kwa kupendelewa , la hasha, ni kutokana na Kanisa hilo kupanga mipango, mikakati na kutabiri vema mwenendo wa uchumi na utawala wa nchi utakavyokuwa. Hakuna Padiri wala Mchungaji kihiyo. Bila digirii nenda kafuge ngurue, hupati Upadiri.
Wewe tazama mambo ya Kanisa Katoliki halafu uamue. Wakati Wapagani wanatambika kwenye mapango na mapori ya Nyamongo, Namanyere, Nakapanya na Nyalikungu, Wakatoliki wanajenga makanisa mijini na kuruhusu wote waje kusali misa na rosari takatifu.
Wakati Waislamu wananunua maspika, maikrofoni na kukodi magari ya kubeba wahubiri kuwathibitishia waja wa Mwenyezi Mungu subhana wa taala kuwa Yesu yule Mnazareti siyo Mungu wao Wakatoliki wanajenga Chuo Kikuu na kuruhusu wote waje kupata shahada na stashahada pale.
Wakati waungwana wanapiga kampeni nchi nzima wakitaka serikali iwaanzishie mahakama yao peke yao kwa ajili ya kuwatatulia migogoro ya mirathi, wakfu na mambo ya talaka wao Wakatoliki wanajenga Hospitali ya Rufani na kuruhusu yeyote atakaye aende kutibiwa pale.
Wakati wengine wanalalamikia serikali kwa kutowajengea barabara wao Wakatoliki wanaomba na kupewa maeneo makubwa ya ardhi mbali na barabara huko maporini kwa ajili ya makanisa yao, mashule yao, seminari zao, vyuo vyao, shule zao za chekechea, msingi na sekondari. Narudia huko maporini!
Hebu jiulize kuna barabara kuu inapita Mbagala Spiritual Centre? Kuna barabara kuu inapita Kurasini Episcopal Centre? Jiulize tu kama kuna mgogoro wa eneo la kanisa barabara kuu za Kilwa, Nyerere, Morogoro, Bagamoyo au Kawawa, Mandela na Sam Nujoma jijini Dar es Salaam? Nasema Kanisa Katoliki siyo vikanisa!
Hilo ndilo Kanisa Katoliki. Kila mwaka wanakutana mara moja wale maaskofu wakubwa wa kanisa hilo na kupanga mipango, mikakati na kutoa maelekezo kwa mapadiri wao. Na mikutano yao hakuna wandishi wa habari na hayatangazwi maazimio yao.
Mtaona tu katika pori fulani wameomba eneo jirani na kijiji, mji au manispaa. Wakilipata eneo hilo wanaanza kujenga kanisa, linafuatiwa na zahanati, inafuatiwa na shule ya watoto wadogo (chekechea), inafuatiwa na shule ya msingi, inafuatiwa na shule ya sekondari ambayo inafuatiwa na chuo cha ufundi.
Haujapita muda mnashangaa kijiji, mji au manispaa inakua kuelekea walipo Makatoliki wale kwa sababu wamewekeza katika vitu vinavyotakiwa na jamii. Mnapozinduka kuwa Yesu awe Mungu au asiwe Mungu ni hoja inayowahusu wanaoamini hivyo tayari Makatoliki wamefikisha vyuo vikuu saba.
Mtakapogundua kwamba dini na maamrisho yake yapasa kutekelezwa na wale wanaoifuata dini hiyo na kwamba mahakama ya kidini yapasa kuanzishwa na wafuasi wa dini hiyo mtakuta tayari Makatoliki wamejenga hospitali 20 au zaidi zinazotumiwa na serikali kama hospitali za wilaya. Ukiugua unataka utakwenda hutaki utapelekwa na nduguzo ukatibiwe huko.
Narudia, mtu pekee nchini anayeweza kucheza kama Pele na kupanga mipango ikapangika na mikakati ikatekelezeka kama Kanisa Katoliki ni mfanyabiashara maarufu Rostam Aziz. Mimi simsifii hivi hivi tu, hebu fuatilia mafanikio yake.
Waziri wa sasa wa Nishati na Madini, Mheshimiwa sana, William Ngeleja, aliwahi kuwa mwajiriwa wa Rostam Aziz. Yaani hapo mwanzo, Ngeleja alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Kampuni ya Vodacom ambayo mmojawapo wa wamiliki wake ni Rostam Aziz. Upo?
Kabla ya Rostam kuanza kuwekeza kwenye nishati na madini, alimsaidia William Ngeleja, kugombea ubunge wa kwao sengerema na kushinda. Mimi nasema alishawishiwa kugombea na wale waliomhitaji na Ngeleja aliposhinda ubunge akapewa Uwaziri wa Nishati na Madini.
Na sasa kampuni ya Richmond/Dowans imeshinda tuzo kwenye mahakama ya kimataifa na inatakiwa kulipwa fidia na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), nasikia mabilioni ya shilingi lakini kabla pesa hizo hazijalipwa mkuu wa kitengo cha sheria cha Tanesco aitwaye Subira kaondolewa!
Hebu bashiri nani kaletwa kuchukua nafasi ya Subira kama Mkuu wa kitengo cha Sheria cha Tanesco wakati huu ambapo Tanesco inatakiwa kumlipa mmiliki wa Richmond/Dowans ambaye mimi nimedokezwa na wanoko wa mjini kuwa ni Rostam Aziz?
Ndiyo umebashiri vizuri. Ni mwanasheria mwingine kutoka Vodacom, ile kampuni ya Rostam Aziz! Kumbe atoke wapi? Kudadeki, Mzaramo kalonga au kasema: kalaga baho na ubozi wako!
Nanachokiona hapa ni msomi mtaalamu wa sheria wa Rostam kapelekwa Tanesco ya serikali chini ya mwanasheria mwingine wa Rostam (Ngeleja) kusaidiana kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa kumlipa haraka iwezekanavyo mmiliki wa Richmond/dowans  ambaye ni Rostam.
Tena mengi hapa sikuyasema, nimeambiwa hata wanasheria walioendesha kesi ya Richmond/dowans walikuwa wapangaji wake Rostam Aziz hapo zamani! Nyie mnaona watu wanashinda tu. Mmeula wa chuya.
Ni mipango, mikakati na uwezo wa kuona mbali. Cheza kama Pele na panga mipango kama Kanisa Katoliki. Usichezee shilingi chooni, usimrudishie mpira golikipa mbele ya adui. Wenye kujua wanachukua viwanja visivyo na migogoro mbali kabisa maporini, faida yake itakuja kujulikana miaka 20 baadaye.

--- On Sat, 5/11/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, May 11, 2013, 3:31 AM

Uzoefu unaonyesha tatizo lipo kwa waislam wenyewe zaidi kuliko serikali. Kwani tatizo ni nini kama waislamu wote kwa ummoja wao wakaamua kuunda ummoja mwingine ambao unakubaliwa na pande zote, na kuiambia serikali kwamba ndicho chombo wanachokitambua
?
Nasema tatizo lipo kwa waislam wenyewe kwa sababu vipo vikundi vyenye sera ambazo wanajua fika ni zao wenyewe na wala hawakubaliani na wenzao. Vikundi hivi ni vidogo lakini vina nguvu kuliko waislam wote na ndivyo vinavyolalamikia BAKWATA. Hadi unaonekana kama mchezo wa madaraka zaidi kuliko haki za waislam. Ilifika mahali misikiti ikaanza kutekwa na vijana na kuwaweka pembeni wazee. Kijana unateka msikiti ambao hujui ulijengwa namna gani hadi ufike hapo ulipo kwa sababu gani? kama siyo kwamba kuna harufu ya vifedha vya kuwaamasisha vijana ni nini? Waislam kuweni macho na watu hawa wenye malengo yao lakini wanataka kutumia mgongo wa uislam. Mambo gani ya kugombania madaraka kwenye huduma za imani?

2013/5/7 Juma abdallah <juma.abdallah@huawei.com>
Paul;
Mi sikuisikiliza huo mchango wa Zitto ila kama kaongea hivyo yuko sahihi kabisa na huo ndo ufumbuzi sahihi.Kwa muda mrefu serikali imeng'ang'ania kuitambua Bakwata pekee kama chombo cha kusemea waislamu wote wakati Bakwata hakikubaliki na asilimia kubwa ya waislam.Matokea yake serikali inapokuwa imekubaliana na Bakwata katika utendaji na maamuzi yanayohusu waislam,matatizo yanaibuka kwa waislam kupingana na maamuzi hayo.Ukweli ukubalike kwamba si waislam wote wanaongozwa na Bakwata,kuna vyombo vingine na kwa serikali kukataa kuvitambua matatizo haya ya mkaranganyiko wa makubaliano utaendelea milele.Ifike mahala taasisi nyingine zitambulike Zitto yupo sahihi.
Ushauri wangu usichanganye mambo,UAMSHO si taasisi ya Kiislam ina mambo yake haiusiani na waislam,pili unaposema vikundi vya kigaidi na kuusisha uislam unapoteza muelekeo na kuwa kama umekurupuka au taja taasisi ya Kiislam unayoiona wewe ni ya Kigaidi..Taasisi za Kiislam na Mihadhara ni vitu tofauti jipange unyooshe maelezo,unachanganya habari.
//Maoni yangu binafsi.
 
From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of paul chilewa
Sent: Monday, May 06, 2013 8:06 PM
To: wanabidii blog
Subject: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa
 
Nimekusikiliza ukichangia budget ya mambo ya ndani, mwanzoni nilikuelewa uliposisitiza umuhimu wa viongozi hasa wa kisiasa kutoa matamko yanayo wagawa wananchi hasa kuwagawa kidini,ulichonichanganya ni pale ulipo sema serikali inakosea kuongea na BAKWATA kwani sio chombo kinachokubalika na waislamu wote,inawezekana ni kweli kutokana na utafiti wako lakini pengine unguzitaja taasisi nyingine zilizo omba kuongea na serikali sikakataliwa na ni kwa masuala yapi kwani kama sijakosea nadhani ni serikali hiyohiyo iliyoongea na waislamu ambao sio BAKWATA na kuwapa chuo cha TANESCO kama sija kosea na kuwa chuo cha kiislamu Tanzania.Mimi nadhani ungetoa mfano wa tasisi hizo badala ya kuitaja BAKWATA kutokubalika na kuacha kutaja taasisi nyingine zilizonyimwa haki hiyo ya kuongea na serikali.Vilevile unaposema serikali isijihusishe na masuala ya kidini hukufafanua najua muda  wa dakika tano hautoshi lakini nivizuri ukawaeleza watanzania kujihusisha kivipi ili tupate tafsiri sahihi.Mimi binafsi serkali kusaidia taasisi ya kidini kama ya kiislamu kupata eneo la kutoa huduma za kijamii kama elimu(Chuo cha kiislamu ni sahihi) lakini kwa uendeshaji dini pengine inaweza isiwe sahihi.Nahisi badala ya kusaidia kutatua tatizo wewe ndio unamwaga petroli Mh tueleze hata muamsho na vikundi vingine vya kigaidi navyo vipewe nafasi mimi binafsi nadhani sio sahihi,Mwisho tuambie grievancies unazotaka serikali kushughulikia nizipi au ni zile tunazosikia kila siku kwenye mihadhara?
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment