Sunday 19 May 2013

Re: [wanabidii] KUTOKA TANGA - Makanisa mawili yachomwa moto


Atang'oaje Camera Sulle kama ziikiwa juu ya highest point pande 4 za paa au ghorofa?
 Mbona Ulaya ambako kuna kila aina ya teknolojia hawang'oi? Maana itabidi kwanza apande juu ya paa au aingie ndani huko computer room azime system na hapo inabidi aingine ndani ya fence na jengo au apande ilipo camera aifunike-juu ya jengo!! Kama majengo ya jirani nayo yana Camera-atazima camera ngapi?

Wizi umekua kiteknolojia na wenye mali, majengo nao wakue na milingoti ya umeme/simu barabarani nao police was usalama barabarani, JWTZ watumie hizi teknolojia waweke camera katika milingoti barabarani au majengo yao. Hivi wakitumia google camera muda walipochoma hawatoona huyo mwanga akienda eneo hilo? Usalama wa nchi unakuwaje mpaka kituo cha police kinavamiwa, nyumba ya Mbunge, mahakama etc hakuna hata camera ya solar kama umeme hakuna, betri zipo pia za alternative power? mbona twacheza na usalama? Hata hao FBI wakija-watapiga ramli kwa manyaunyau kujua issue wakati vya kuweka vidhibiti vya monitoring usalama hatuna? Au vipo hatujui ni siri? Sasa tunawasakaje miezi na miaka kama tunavyo na bado hatuwajui?

Watu wamejaa ubinafsi kwani utaona hata kule wanakopigana ambako dini ni moja-wanawake na wasichana wanabakwa sio tu kuuawa. Familia nayo inawaua kwa hadhi ya familia wakijua wamebakwa. Sasa, Janjaweed wa N. Sudan anambaka msichana S. Sudan huku mbakaji anasali kutwa mara 5 na anapigana kwa jila la Allah!  Jee hapa DINi ipo wapi na anabaka? Vitoto vidogo visichana vyeusi Sudan ya Kusini vimebeba vitoto vya kiarabu ktk umri mdogo kutokana na kubakwa! Au anapigana Afghanistan, Syria, Mali-anabaka na kuua anarusha jambia anatoa roho ya mtu na anaua akimtaja Allah!! Mungu gani anakutuma ufanye hivi? Hii haiji akilini kama haya ni mapigano ya KIDINI-ni ubinafsi tu wa binadamu. Ni kama ile ya Mbagala unachoma moto, unaingia kanisani unaiba vifaa unapeleka nyumbani (Unampeleka Yesu unamkaribisha home kumtoa kanisani). Maana vifaa vya kanisa la Yesu umepeleka nyumbani huku umechoma moto kanisa lakini umebeba vitu umeiba. Hii ni Njaa. Ila-mambonde hayo ya Mbagala, Mkuranga, Pugu, Kisarawe huyaoni ukalima na kupata chakula kutwa upo barazani utaranta wa Manchester, simba , yanga, makanisa na uonevu. ukienda Kisiju ardhi bwerere msukuma anahamia na mifugo, kulima na kukuuzia mihogo; mikorosho ipo ktk majani na mabonde ya chepechepe yameota magugu msukuma kaingia anayakausha na mifugo. Anakata miti anauza mkaa anakupa gunia 2 za mkaa uuze; analima mihogo na viazi na kukupa lita ya maziwa daily unaona umeukata. Jitume na somesha. Hakuna dini inayoruhusu uue na ufanye uchafu kwa jina la Mungu. Hawa wachomao makanisa au mahekalu ni njaa tu, bangi na unga umewaharibu akili.

Pamoja na kuwa kuna uwezo wa kutengeneza magobore vijijini lakini wapiganaji wakiona hawapati silaha, chakula na misaada yoyote, hawawekewi hela bank na hao wanaowatuma labda wataacha. labda ukiripua kanisa-bank transfer ya mamilioni inaingia bongo account unaganga njaa. Haya yaangaliwe.

Ufike wakati nchi za ulaya sisipokee wakimbizi, isiwauzie silaha nchi za africa na bara la Asia, UN iache kwenye nchi zipiganazo zijimalize zenyewe bila misaada labda wataacha.
Faida gani miji ya Somalia, Syria kuwa maghofu? gharama ya miaka/karne ya kujenga miji hiyo ya maghorofa kama Libya, Syria na sasa kubomoa. Vizazi vijavyo vinavuta moshi wa sumu-watakuja kuzaa watoto vilema tu. wataijenga tena Syria kwa miaka mingapi? Kwa kumuua mwana maendeleo Gadafi-wamepata nini Libya mbona hakujatulia? wamemuonea tu kijana wa watu ambae alikuwa mwanamapinduzi halisi. Ya Gadafi imeumiza sanasana. laana yake wataibeba maisha yao yote. Mnataka nini watanzania wakati mnaona wenzetu wanavyokimbia na kuacha watoto na wazazi nyuma, anatupa mizigo hajui aende wapi. porini kuna simba, fisi chui watakutafuna. Ubakaji congo HIV/AIDS kila askari kutokana na ubakaji na kila kaya watu wameambukizwa. Ubakaji kwa sasa sio limited kwa wanawake tu-si tunawasikia wasemavyo ni wamama na wababa. tena bora wamama wanapata huduma wababa wanakufa kisaikolojia kujitokeza na kubata huduma. Ndio mwataka haya yote? PUMBA Tupu vichwa vyetu tumendau mapambano ya kivita na kuuana badala ya kujenga nchi. Tu wavivu, hatuna malengo ya maisha yetu. penye kila kitu unakuta tumebweteka ni malumbano kisiasa na kutokuzingatia matumizi endelevu ya raslimali, visingizio kibao. Kichefuchefu.

Nchii hii inataka dictator kuliko Kagame. kama unataka uchaguliwe uwe Rais 2015, usiahidi kutuachia tubweteke-ahidi kuwa utahakikisha kila mtu anafanyakazi, anasoma shule zenye karakana za ujuzi sio kusoma nadharia tu; uwekezaji utatoa direct benefits`kwa vijiji asilimia kadhaa na kutakuwa na auditing vijijini hadi kitaifa; watu watazingatia matumizi endelevu ya ardhi na raslimali zake pende wasipende mpaka kufuga kisasa sio kuzurura na kuathiri mazingira na kilimo; upunguzaji mifugo kuzingatia uwezo wa ardhi itakuwa ni LAZIMA; kutumia vifaa vya kisasa kwa wachimbaji wadogo wadogo na kutumia protective gear LAZIMA au ulazwe ndani na kuchimba madini ni kwa kuunda vikampuni na kuviandikisha ili mpate mikopo. Hii itapunguza uharibifu mazingira, uchafuzi wa maji na uharibifu afya na mikopo itatolewa na kufirisiwa wakilewea pombe wasichimbe madini.Biashara ni kuzingatia misingi yake na mahala palipo ruhusiwa sio kujaa barabarani mpaka mkandarasi anashindwa kuchonga barabara muda unapita tumejitandara na vibanda vyetu hatuondoki kiasi kwamba hata kupiga mitaro ya maji anashindwa. ahidi uzalishaji mali na nidhamu ya utendaji wa kikazi, mazingira na mipango ardji mijini na vijijini. Kusiwe na kuzurura vibaba limebeba sidiria na sumu ya panya kutwa anatembea kilometa 5-50. Angekuwa Ruangwa valley angetumia nguvu hii kulima ekari ngapi? fungua mashamba ya JKT, wape trekta, jenga mabanda na mahema tuwasombe tukalime huko, packaging ya mazao, dege la jeshi linakuja linazoa, yanashushwa KIA yanakwenda kuuzwa nchi zenye njaa. Ukikutwa unazurura mjini ukamatwe. Masoko yalipo mitaani yanafikika. Tuwaondoa hawa wa barabarani wakae mahala walipotengewa ili wakandarasi wafanye maendeleo ua ukarabati miundombinu ikamilike on-time. Bajaji na bodaboda kupita njia ya miguu na biashara kupangwa njia za kupita watu ikishughulikiwa nasi wahusika tukizingatia nidhamu zinazotakiwa hizi chuki za kijinga za kupigana na maofisa afya, mgambo, polisi zitakwisha ili tufanye ya maendeleo.

Kuchoma moto makanisa sio solution ya matatizo tunayoyaanzisha wenyewe.




--- On Sun, 19/5/13, Emmanuel Sulle <esulle17@gmail.com> wrote:

From: Emmanuel Sulle <esulle17@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] KUTOKA TANGA - Makanisa mawili yachomwa moto
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, 19 May, 2013, 21:42

Hizo vifaa si watangoa kabla hawajatekeleza huu uovu?


2013/5/19 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>

Dawa ni kwa makanisa na wenye biashara kuweka Cameras kuzunguka majengo yako zikiangalia na kurekodi pande zote masaa 24. Poa kuweka smoke and heat detectors
ambazo zitapiga king'ora mara smoke na heat level inapoongezeka zaidi ya kawaida. Tatizo letu pia ni kutokuzingatia building regulations ambazo zinataka uweke smoke detectors majengo ya nyumba wakazi wengi, taasisi, maghorofa n.k.

Wakristu wajengao mahekalu kama mahema yakiwa wazi maeneo ya juu na milango kukaa wazi kutwa wajue design hizo sasa zimepitwa na wakati kwani ni rahisi kuwashwa moto. Budi sasa kujenga nyumba za hekalu za kusalia zikiwa na milango na zenye kufunguka milango kwa kutumia code maalum ili wasipate urahisi hao wahuni kuingia na kuchoma vitambaa, vitabu etc.

Pili kujenga kwa materials ambazo zitachukua angalau nusu saa kuwaka moto. Hii itatoa mwanya kwa watu kupata satua ya kutoka au kukimbia kabla moto haujazingira na kuita msaada mara moto unapoonekana kabla haujatanda.Mbao zinaweza kufanyiwa treatment against moto kama ilivyo kwa vifaa ndani ya ndege vichukue muda kabla ya kuwaka haraka.

Sheria ichukue mkondo wake. Sheria ya ujenzi imekiukwa maeneo mengi. Kati ya nyumba za squatter areas za mbanano watu wanaweka hekalu kusali kutwa kucha tena kwa makelele. Eti kujenga hekalu katikati ya wauza mitumba na Bar inategemewa inaweza kubadili watu na kujiunga na kumwomba Mungu. Fika mwenge uone hekalu adjacent bar ambapo watu wanalewa chakari. Ni hivyo Kinondoni Mkwajuni, Mikocheni, Ubungo Darajani, Ubungo kilimani kutoka Tanesco na Maji juu etc. Watu huona kero. Loud speakers huku adhana msikiti kelele upande mwingine, huku mikesha na mahubiri hekalu la kanisa, upande wa pili beer bars na midundo ya miziki kutwa kucha. Hivi nchi hii kulikoni? Mbona tunakosa nidhamu ya ujenzi na tunafanya hivi wenyewe.

Hebu tuangalie location ya haya majumba ya ibada versus makazi ya watu na biashara. Kama makanisa yangekuwa mbali ilivyokuwa zamani na uwanja mkubwa fenced, camera zipo juu ghorofani na yupo mtu hapo 24 hrs anafanya monitoring au recall ya camera kuangaliwa-unawaona wakija au waliokuja. Tuwe modern. Mbona wachina wamejaza electronic security gears madukani? Ndio daima yatachomwa makanisa akiwa anaonekana ndio adui lakini adui ni malengo na mfumo wako wa maisha, jinsi gani unajituma, kukazania elimu dunia, kuzalisha mali mali asili na ardhi ipo unauza hovyo bila ya kuwa na malengo. anakuja mhindi, Mkenya, Mchina, Msomali anakulimisha kwa jembe la mkono ktk ardhi yako mwenyewe. Hoteli yake saa kumi na mbili unapata chai na chapati tena anapika huyo mwenyeji on-time kwa kusimamiwa na huyo msomali. lakini hoteli yake mswahili fika kupata kitu 40 min+ na akija anasema-hiki hakipo, unaagiza kingine-hakipo na alikupa menu. Ikija sahani na kikombe-vichafu na ukimsemesha anajibu kiburi. Matokeo kukosa biashara au mwenye hoteli kuajiri wageni-from Malawi etc.

Kama tatizo ni ukristu, hata yachomwe makanisa/mahekalu yote bado matatizo yatakuwepo. Kama wachomao ni waislamu wa kundi fulani-mbona Somalia, Syria, Afganistan, Mali wanakopigana wenyewe kwa wenyewe, vitengo vya madhebu vya dini moja licha ya kuwa nchi nzima ni dini hiyo hayaishi? Sasa jiulize-Kanisa ndio adui? Mbona huko ambapo dini ni hiyo moja wanapigana vita na miji kuwa maghofu tupu?

Wanakokimbilia kujiokoa na kuomba kusaidiwa nchi zina katiba za dini ya kikristu? Wakiachwa-wanalaumu kuwa hawasaidiwi na nchi hizo kama USA, UK etc? Hapa kuna mengi yanajificha. Labda sio dini dini inatumika tu. Labda ni kuikomoa serikali wasiyoitaka kuwa wanaona ngumu kuiangusha.

Kama tatizo ni dini, weka wivu muige anayechanga hela hekaluni na kujiletea maendeleo nawe changa kwa malengo. Kama unamuonea wivu virani yako kaendelea kakuzidi-muige jitahidi kujituma kama yeye. Ukimvambia umuharibie ili umkomoe-ipo siku Mungu atajibu au sheria itachukua mkondo utaumia. ukisha kumuharibia, jee wewe unakuwa umeendelea na kuvuka kiwango kinapanda juu?

Lingine la kuchangia ni Msongamano wa majumba.
Tujikanye wenyewe tusingatie upimaji na ramani za viwanya. Tuache feeder roads ziwepo tusizifunge kwa kuweka kibanda cha biashara, kuziba kuweka gate na kubananisha viwanja/majengo. Moto huu uwakao utufundishe `kuwa-tunapoendelea kuziba mapito-tunajikaanga moto uwakapo. Vile vile miji inakuwa ugly shunty towns in cities. Maana, hata hule kulikopimwa viwanja kukajengwa nyumba na NHC-kote kuko hovyo msongamano, makorogoro kila kona. Watu wamejenga mpaka kwenye mabwawa ya kinyesi na wanakesha hapo mabibo, vingunguti kutwa kucha hawaogopi hata mbu wa matende na mainzi. Licha ya kuishi na uchafu, huu msongamano tunaoutengeneza mijini na vijijini ni hatari kwa moto na hatufundishiki ila lawama tu kwa serikali ambapo sisi wenyewe ni viburi waharibifu. Tuone sasa kama serikali ya CCM haijui kazi ije hiyo ya Chadema etc ianze kuwabomolea waliokiuka sheria za ujenzi halafu waiona Chadema nzuri inafanyakazi njema kwa kuwabomolea ili mipango miji ikae sawa. Au tuseme ndio wataruhusu msongamano na ukiukaji mipango ardhi/miji/nyumba ili eti kuganga njaa? Hawatoangalia tahadhari za moto huu ulioanza kuripuliwa majumbani, matairi barabarani ambayo yanaweza kuleta madhara makubwa?
Thinking aloud-Mungu Tusaidie.

--- On Sun, 19/5/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] KUTOKA TANGA - Makanisa mawili yachomwa moto
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 19 May, 2013, 10:51


Makanisa mawili yamechomwa moto usiku wa kuamkia leo huku bila
mafanikio watu wasiofahamika wakijaribu kuteketeza kwa moto banda moja
la kuoneshea picha za video.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alisema tukio la
kwanza lililotokea majira ya saa 8 usiku katika Kanisa la Betham
lililoko eneo la Donge ambapo wahusika waliteketeza kwa moto jengo la
Kanisa dogo lililokuwa likitumika zamani na kisha kuingia ndani ya
Kanisa kubwa la sasa na kuviwasha kwa moto vitambaa vilivyokuwa
vimefunika madhabahu.

Massawe alisema:
Kanisa lililoteketezwa hapo lilikuwa la zamani ila sasa linatumiwa na
waumini wa Betham kwa ajili ya kufundisha watoto lakini ibada zote
zinafanywa kwenye jengo hilo jipya ambalo ndilo lililochomwa vitambaa
vilivyokuwa vimefunika madhabahu.
Aidha, alisema taarifa za kuchomwa Kanisa hilo zilitolewa na Sauli
Taminola mmoja wa waumini hao ambaye analala hapo Kanisani ambaye
anadai alishtuka kutoka usingizini mara baada ya kuona moto ukiwaka
madhabahuni ndani ya Kanisa.

Tukio jingine la usiku huo huo alisema liliripotiwa kuhusisha Kanisa
la Miracle Revival lililopo eneo la Makorora majira ya saa 9 za usiku
ambapo watu walidai walishituka usingizini na kuona moto ukiwaka
kwenye nguzo za Kanisa hilo ndipo wakapiga kelele za kuomba msaada.
Mchungaji ambae anaishi jirani na kanisa alisema aliona watu wakiwasha
moto magurudumu (matairi) ya baiskeli na kuyafunga kweney boriti za
kanisa ili ziweze kuungua moto lakini baada ya kuwakurupusha jaribio
hilo lilishindwa kwakuwa moto ulidhibitiwa na watu pasipo kuleta
madhara makubwa
alisema Kamanda Massawe.

Akizungumzia klabu ya pombe za kienyeji iliyoteketea usiku huo alisema
tukio hilo lilitokea katika eneo la Kwanjeka kwenye baa inayofahamika
kama 'Bongola' na kudai kwamba chanzo ni shoti ya umeme.

Kamanda Massawe alisema tukio la nne limehusisha banda moja la
kuoneshea mikada ya picha za video huko huko Kwanjeka ambalo nalo
lilikaka kuteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana lakini jaribio lao
halikufanikiwa.

---
Taarifa via Lukwangule Ent. blog


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/tanga-makanisa-mawili-yachomwa-moto.html#ixzz2TjbmEoC6

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment