Nimekuelewa. Poa. Ila unapojiripua, ukakatika miguu bila ya kufa ukakaa hai, hao waliokutuma na Imani iliyokuganda hawakusaidii/haikusaidii. Unabaki unasota saidia baba, saidia mama!! Walioahidi kuilipa familia yako kama utafanikiwa kujiripua, kuua na kufa-wanalala mbele- hawalipi hela. Hii tumeisoma katika magazeti na taarifa mbali mbali nayo ipo. Hao mabikira saba utapewa kweli na peponi hakuna ngono? Hakuna aliyekwenda peponi akarudi anyway akatueleza kama huko kuna ngono hadi hao mabikira saba iwe issue. Zipo dini duniani za waumini kutembea bila ya kuvaa nguo na ktk mahekalu kuharibu vichanga kwa ngono. Nao wana Mungu wao na Imani yao inayotaka kutembea bila ya nguo iwe haki ya binadamu na kuabudu lolote kwa Imani yako iwe haki. Dini ni OPIUM, Imani ndio kitunguu saumu chake. Hata Kinjikitile Ngware aliwaambia watu wake kuwa bunduki ya mzungu itageuka maji na akiipiga ikalia semeni 'Maji' tutashinda na vita ya Maji maji ikamaliza watu na ni mfano mmojawapo wa Imani. Magazeti yanatangaza Imani za waganga na waganga wa kienyeji hufanikiwa kurubuni watu wakaamini na kuuana, kuua albino, kuchomeana nyumba kwa imani ya kichawi.Utajiri wa harakaharaka bila masharti, hela za jini chuma ulete, dawa ya kupasi mtihani ukawa wa kwanza hata kama umefeli, kumshika mume asitoke na akupe kila utakacho; dawa ya kufuta kesi mahakamani; kufanikiwa maishani, dawa ya biashara (sio usome ujasiriamali- no). Issue ya Imani ni tatizo hasa kama Imani yenyewe ni POTOFU. Na ndio maana nikahoji-unapoua unataja allah, unaingia nyumba ya mtu adui yako unamkomoa kwa 'kubaka akina mama, visichana, akina baba'-Imani ya Allah na kwenda uwinguni ipo hapa? Huu ni Ubinfasi, dini na Imani yake 'Kisingizio'. Hebu ona Mzee Karume alivyouawa Msikitini-Nyumba ya Mungu. Ona kazi aliyofanya. Majumba aliyoanzisha kama ya Libya yamemaliziwa juzi baadhi yake miaka yote yalikaa hivyo maendeleo aliyokuwa ameanzisha. Ona Libya-wamepata nini na imani uisemayo? Ona Misri. ilikuwa mfano. Imesomesha madaktari wapo dunia nzima, utalii masaa 24 maduka Cairo hayafungwi usiku, mchana. Sasa hebu ona. Rais aliyeingia alivyo mkali kukemea na kutawala kimabavu ili awaweze. Bado hayajaisha pamoja na kuua na kuuana. Watu wasio na hatia unawaua, umasikini palepale au kuongezeka. Kwani vita inachagua. Kama Boko Haram na Janjaweed na wengineo ni Imani ya uwingu inawasumbua-mbona jamaa zao wakipata nafasi ya kukimbia nchi nchi wakimbiliazo ni zile zenye katiba ya 'msalaba?' Hii ndio ninahoji kama ukristo ni tatizo kwao. Chakula cha kuganga njaa kinatoka huko misalabani na mpaka sasa wamefikia kulisha watu chakula cha mifugo. Bora mtu asife ale hiki cha mifugo kisicho madhara kuliko afe kabisa kwa kukosa kula na unawaona wamepanga foleni. Imani ndio inaponza lakini mifano mbona mingi kama hata ya Kibwetere-Uganda na ya nchi ambazo sasa ni maghofu? Unaona hasa kama imani imewababaisha, nchi maghofu na kila mtu anatengeneza hela zake na kuvamia misafara kupora ili kuishi; kuvamia walimu wanaofundisha wasifundishe na huwakata mikono wakabaki nchini na vilema wengi wakakosa nguvu kazi. Kama issue ni Imani-na kwenda kwa Mungu, kwa nini ukisha kuua unajificha hujitokezi uuawe hadharani ili uende mbinguni? unajificha na ukikamatwa unaweka mawakili huku ukiwa umeua au kuhusika na kuchoma hekalu. Unakana hatia? Hii ni imani ya Mungu au UBINAFSI. Ungejitokeza ukasema ni mimi, nipigeni risasi-wewe unakana japo umehusika. Hata rais wa Liberia aliyeua alikana pia Idd Amin, Sembuse Boko-Haram. Hawaui kwa kujionyesha ili nao wafe waende peponi. DINi Kisingizio-ubinafsi tu. Na ndio maana Mungu kajificha, angejitokeza aseme ukweli wangeaibika wengi kuona kuwa wanachoamini si Kweli, wameongezea chumvi kwa tamaa zao. Kila roho inahaki ya kuishi na kumcha Mungu, Usiue, usizini. Dhambi ya kuua kwa makusudi -haina msamaha. Tulinde Amani Yetu TZ, tupendane bila ubaguzi. Tuchape kazi ili tuondoe visingizio vya aina yote vitakavyofanya kuoneana. Hii ndio hoja kuu yangu-Adios Amigo!! --- On Mon, 20/5/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment