Sunday 19 May 2013

Re: [wanabidii] KUTOKA TANGA - Makanisa mawili yachomwa moto


Dawa ni kwa makanisa na wenye biashara kuweka Cameras kuzunguka majengo yako zikiangalia na kurekodi pande zote masaa 24. Poa kuweka smoke and heat detectors
ambazo zitapiga king'ora mara smoke na heat level inapoongezeka zaidi ya kawaida. Tatizo letu pia ni kutokuzingatia building regulations ambazo zinataka uweke smoke detectors majengo ya nyumba wakazi wengi, taasisi, maghorofa n.k.

Wakristu wajengao mahekalu kama mahema yakiwa wazi maeneo ya juu na milango kukaa wazi kutwa wajue design hizo sasa zimepitwa na wakati kwani ni rahisi kuwashwa moto. Budi sasa kujenga nyumba za hekalu za kusalia zikiwa na milango na zenye kufunguka milango kwa kutumia code maalum ili wasipate urahisi hao wahuni kuingia na kuchoma vitambaa, vitabu etc.

Pili kujenga kwa materials ambazo zitachukua angalau nusu saa kuwaka moto. Hii itatoa mwanya kwa watu kupata satua ya kutoka au kukimbia kabla moto haujazingira na kuita msaada mara moto unapoonekana kabla haujatanda.Mbao zinaweza kufanyiwa treatment against moto kama ilivyo kwa vifaa ndani ya ndege vichukue muda kabla ya kuwaka haraka.

Sheria ichukue mkondo wake. Sheria ya ujenzi imekiukwa maeneo mengi. Kati ya nyumba za squatter areas za mbanano watu wanaweka hekalu kusali kutwa kucha tena kwa makelele. Eti kujenga hekalu katikati ya wauza mitumba na Bar inategemewa inaweza kubadili watu na kujiunga na kumwomba Mungu. Fika mwenge uone hekalu adjacent bar ambapo watu wanalewa chakari. Ni hivyo Kinondoni Mkwajuni, Mikocheni, Ubungo Darajani, Ubungo kilimani kutoka Tanesco na Maji juu etc. Watu huona kero. Loud speakers huku adhana msikiti kelele upande mwingine, huku mikesha na mahubiri hekalu la kanisa, upande wa pili beer bars na midundo ya miziki kutwa kucha. Hivi nchi hii kulikoni? Mbona tunakosa nidhamu ya ujenzi na tunafanya hivi wenyewe.

Hebu tuangalie location ya haya majumba ya ibada versus makazi ya watu na biashara. Kama makanisa yangekuwa mbali ilivyokuwa zamani na uwanja mkubwa fenced, camera zipo juu ghorofani na yupo mtu hapo 24 hrs anafanya monitoring au recall ya camera kuangaliwa-unawaona wakija au waliokuja. Tuwe modern. Mbona wachina wamejaza electronic security gears madukani? Ndio daima yatachomwa makanisa akiwa anaonekana ndio adui lakini adui ni malengo na mfumo wako wa maisha, jinsi gani unajituma, kukazania elimu dunia, kuzalisha mali mali asili na ardhi ipo unauza hovyo bila ya kuwa na malengo. anakuja mhindi, Mkenya, Mchina, Msomali anakulimisha kwa jembe la mkono ktk ardhi yako mwenyewe. Hoteli yake saa kumi na mbili unapata chai na chapati tena anapika huyo mwenyeji on-time kwa kusimamiwa na huyo msomali. lakini hoteli yake mswahili fika kupata kitu 40 min+ na akija anasema-hiki hakipo, unaagiza kingine-hakipo na alikupa menu. Ikija sahani na kikombe-vichafu na ukimsemesha anajibu kiburi. Matokeo kukosa biashara au mwenye hoteli kuajiri wageni-from Malawi etc.

Kama tatizo ni ukristu, hata yachomwe makanisa/mahekalu yote bado matatizo yatakuwepo. Kama wachomao ni waislamu wa kundi fulani-mbona Somalia, Syria, Afganistan, Mali wanakopigana wenyewe kwa wenyewe, vitengo vya madhebu vya dini moja licha ya kuwa nchi nzima ni dini hiyo hayaishi? Sasa jiulize-Kanisa ndio adui? Mbona huko ambapo dini ni hiyo moja wanapigana vita na miji kuwa maghofu tupu?

Wanakokimbilia kujiokoa na kuomba kusaidiwa nchi zina katiba za dini ya kikristu? Wakiachwa-wanalaumu kuwa hawasaidiwi na nchi hizo kama USA, UK etc? Hapa kuna mengi yanajificha. Labda sio dini dini inatumika tu. Labda ni kuikomoa serikali wasiyoitaka kuwa wanaona ngumu kuiangusha.

Kama tatizo ni dini, weka wivu muige anayechanga hela hekaluni na kujiletea maendeleo nawe changa kwa malengo. Kama unamuonea wivu virani yako kaendelea kakuzidi-muige jitahidi kujituma kama yeye. Ukimvambia umuharibie ili umkomoe-ipo siku Mungu atajibu au sheria itachukua mkondo utaumia. ukisha kumuharibia, jee wewe unakuwa umeendelea na kuvuka kiwango kinapanda juu?

Lingine la kuchangia ni Msongamano wa majumba.
Tujikanye wenyewe tusingatie upimaji na ramani za viwanya. Tuache feeder roads ziwepo tusizifunge kwa kuweka kibanda cha biashara, kuziba kuweka gate na kubananisha viwanja/majengo. Moto huu uwakao utufundishe `kuwa-tunapoendelea kuziba mapito-tunajikaanga moto uwakapo. Vile vile miji inakuwa ugly shunty towns in cities. Maana, hata hule kulikopimwa viwanja kukajengwa nyumba na NHC-kote kuko hovyo msongamano, makorogoro kila kona. Watu wamejenga mpaka kwenye mabwawa ya kinyesi na wanakesha hapo mabibo, vingunguti kutwa kucha hawaogopi hata mbu wa matende na mainzi. Licha ya kuishi na uchafu, huu msongamano tunaoutengeneza mijini na vijijini ni hatari kwa moto na hatufundishiki ila lawama tu kwa serikali ambapo sisi wenyewe ni viburi waharibifu. Tuone sasa kama serikali ya CCM haijui kazi ije hiyo ya Chadema etc ianze kuwabomolea waliokiuka sheria za ujenzi halafu waiona Chadema nzuri inafanyakazi njema kwa kuwabomolea ili mipango miji ikae sawa. Au tuseme ndio wataruhusu msongamano na ukiukaji mipango ardhi/miji/nyumba ili eti kuganga njaa? Hawatoangalia tahadhari za moto huu ulioanza kuripuliwa majumbani, matairi barabarani ambayo yanaweza kuleta madhara makubwa?
Thinking aloud-Mungu Tusaidie.

--- On Sun, 19/5/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] KUTOKA TANGA - Makanisa mawili yachomwa moto
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 19 May, 2013, 10:51

Makanisa mawili yamechomwa moto usiku wa kuamkia leo huku bila
mafanikio watu wasiofahamika wakijaribu kuteketeza kwa moto banda moja
la kuoneshea picha za video.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alisema tukio la
kwanza lililotokea majira ya saa 8 usiku katika Kanisa la Betham
lililoko eneo la Donge ambapo wahusika waliteketeza kwa moto jengo la
Kanisa dogo lililokuwa likitumika zamani na kisha kuingia ndani ya
Kanisa kubwa la sasa na kuviwasha kwa moto vitambaa vilivyokuwa
vimefunika madhabahu.

Massawe alisema:
Kanisa lililoteketezwa hapo lilikuwa la zamani ila sasa linatumiwa na
waumini wa Betham kwa ajili ya kufundisha watoto lakini ibada zote
zinafanywa kwenye jengo hilo jipya ambalo ndilo lililochomwa vitambaa
vilivyokuwa vimefunika madhabahu.
Aidha, alisema taarifa za kuchomwa Kanisa hilo zilitolewa na Sauli
Taminola mmoja wa waumini hao ambaye analala hapo Kanisani ambaye
anadai alishtuka kutoka usingizini mara baada ya kuona moto ukiwaka
madhabahuni ndani ya Kanisa.

Tukio jingine la usiku huo huo alisema liliripotiwa kuhusisha Kanisa
la Miracle Revival lililopo eneo la Makorora majira ya saa 9 za usiku
ambapo watu walidai walishituka usingizini na kuona moto ukiwaka
kwenye nguzo za Kanisa hilo ndipo wakapiga kelele za kuomba msaada.
Mchungaji ambae anaishi jirani na kanisa alisema aliona watu wakiwasha
moto magurudumu (matairi) ya baiskeli na kuyafunga kweney boriti za
kanisa ili ziweze kuungua moto lakini baada ya kuwakurupusha jaribio
hilo lilishindwa kwakuwa moto ulidhibitiwa na watu pasipo kuleta
madhara makubwa
alisema Kamanda Massawe.

Akizungumzia klabu ya pombe za kienyeji iliyoteketea usiku huo alisema
tukio hilo lilitokea katika eneo la Kwanjeka kwenye baa inayofahamika
kama 'Bongola' na kudai kwamba chanzo ni shoti ya umeme.

Kamanda Massawe alisema tukio la nne limehusisha banda moja la
kuoneshea mikada ya picha za video huko huko Kwanjeka ambalo nalo
lilikaka kuteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana lakini jaribio lao
halikufanikiwa.

---
Taarifa via Lukwangule Ent. blog


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/05/tanga-makanisa-mawili-yachomwa-moto.html#ixzz2TjbmEoC6

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment