Sunday 19 May 2013

Re: [wanabidii] Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu....

Maggid,
 
Heri yako wewe uliyeona hivi, lakini wengi kwenye mitandao ya kijamii ukiitembelea utaona ni siasa tupu isiyo nakichwa hata miguu. Haitawezekana hata siku moja kuwa na watu wasiotaka taratibu zifuatwe, hawapo kabisa katika ulimwengu wa leo.
 
Mbunge kwa tataribu za Serikali za Mitaa ni Mjumbe wa Kmatai za Fedha na Utawala za Halmashauri na pia ni Mjuumbe wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa.
 
Kama ni hivyo, sasa alishindwa/ ameshindwa vipi kuwashawishi wenzie (Madiwani wa Manispaa ya Iringa) kwenye vikao iliwasipistishwe azimio la kuwaondoa hao wamachinga eneo hilo na kuwapeleka sehemu nyingine? Au tuseme ndio hajui huo utaratibu au haudhurii vikao vya Halmashauri yake ili kujua nini kimeamuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa yaani manispaa ya Iringa.
 
Wanasiasa wa namna hii wenye siasa za kiharakati kila wakati, bila kujali maslahi ya wananchi bali kupata mtaji wa kisiasa ni hatari sana. Ninachojaribu kufikiri kwa makini sana hapa ni kwamba anajaribu kukusanya watu wengi wawe upande wake baada ya Kinana kumtishia kumshitaki.
 
Ngoja tuangalie lakini kwa kweli siasa nyingine hazina utamu bali uchungu tupu.
 
K.E.M.S.
From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, 19 May 2013, 2:18
Subject: [wanabidii] Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu....

Kinachotokea Iringa, tafsiri yangu…
 
Ndugu zangu,
 
Leo saa mbili na nusu asubuhi nilifika Jengo la NSSF nikitokea kufanya jogging yangu ya asubuhi. Nilifika hapo kuwahi kununua magazeti.
 
Hali ilikuwa shwari kama ilivyo kawaida ya Iringa Jumapili asubuhi. Kunako saa tatu asubuhi nilipokuwa nyumbani nikisoma magazeti,  ndipo niliposikia mlio wa kwanza wa bomu la machozi. Idadi yake ikaanza kuongezeka.
 
Nikiwa na kamera yangu nikajisogeza  hadi katikati ya mji kufahamu zaidi kinachotokea. Nilichokiona ni  vurugu kati ya Wamachinga na Jeshi la Polisi.
 
Tatizo?
 
Ni  dogo sana, lakini linakuzwa kwa vile siasa imepelekwa mbele badala ya kutanguliza hekima na busara. Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa  kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano  ingali wazi.
 
Kinachotokea Iringa kwa sasa ni doa kubwa kwa mji wetu wenye sifa ya muda mrefu ya utulivu. Kina athari kubwa kiuchumi pia.  Pale Iringa mjini nilichokiona leo ni kama mji ulio katika mapigano ya kivita. Watu ni wachache na wenye hofu.
 
Biashara nyingi zimesimama. Niliziona Daladala zikitoka Kituo cha Miyomboni bila hata abiria, watoke wapi? Wakati kwa sasa walio nje ya mji wameambiwa na jamaa zao walio katikati ya mji kuwa wasijaribu kufika mjini,  kwamba hali imechafuka.
 
Nimeongea na mwuza nyama ya bucha aliyeniambia kuwa mgomo wa Daladala wa hivi karibuni ulimfanya apate hasara kubwa kwenye  biashara yake ya nyama kwa vile wateja wake wengi wanatoka nje ya mji. Na anachokiona leo ni hasara nyingine kwa vile hakutakuwa na biashara nzuri. Je, ni wafanyabiashara wangapi watakaoathirika na hali hii ya leo?
 
Na kwa kuwa mkweli, kisiasa kinachotokea Iringa kwa sasa kinaweza kuwa na athari hasi kwa Mchungaji Msigwa badala ya kumjenga kisiasa, kwani, wengi niliozungumza nao katikati ya mji wanamwona Mchungaji Msigwa kuwa ni mtu ambaye angeweza kuiepusha hali hii kama asingeyatumia majukwaa ya siasa kuwahamasisha Wamachinga kuendelea kufanya biashara, na hivyo, kutokutii amri ya Manispaa.
 
Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu. Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye Harambee pale Tumaini University.
 
Kama Mchungaji Msigwa angejibu simu yangu, basi, ningemwambia haya ninayoyaandika hapa.
 
Maggid Mjengwa,
Iringa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment